Rais Magufuli ameguswa na nini hadi kuwakemea waendesha mashtaka kwa kuchelewesha upelelezi kwa watuhumiwa wanaoozea jela?

Rais Magufuli ameguswa na nini hadi kuwakemea waendesha mashtaka kwa kuchelewesha upelelezi kwa watuhumiwa wanaoozea jela?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Kama kichwa changu cha habari kinavyouliza hivi Rais Magufuli "ameguswa" na nini hadi awakenee waendesha mashtaka wanaochelewesha upelelezi wa kesi zilizoko mahakamani, jambo linalosababisha watuhumiwa wengi kuendelea kupata mateso ya hali ya juu, kwa kuendelea kusota rumande kwa kipindi kirefu sana?

Tunajua kuwa wapo watuhumiwa wengi ambao wako mahabusu kwa kesi za kubambika za utakatishaji pesa, ambazo wao waendesha mashitaka wanajua kuwa hazina dhamana, hivyo kuzitumia kama "fimbo" ya kuwatesea watuhumiwa hao ambao hawana hatia.

Hebu tujaribu ku-imagine kwa mfano kesi ya mwandishi wa habari Erick Kabendera, huu ni mwezi wa 8, kila kesi hiyo inapotajwa hapo mahakamani, waendesha mashitaka hao, wanadai kuwa upelelezi hawajaukamilisha!

Hivi inawezekanaje kwa Polisi kupeleka kesi mahakamani, tena ya utakatishaji pesa, wakati upelelezi bado haukakamilika?

Hivi hiyo siyo njia tu ya kuwakomoa watuhumiwa hao wa utakatishaji pesa, kwa vile hao Polisi wanajua kuwa kesi hizo hazina dhamana?

Sasa Rais Magufuli amesema walaaniwe waendesha mashitaka hao, wanaosababisha mateso makubwa kwa watuhumiwa, kwa kuendelea "kuwasotesha" rumande.

Hata kama kwa mawazo ya wengi kuwa walidhani kuwa Jiwe ndiye "mastermind" wa kesi hizo, sasa keshawaruka futi 10,000.

Kwa hiyo kazi kwenu zigo lote la ubaya kawabakizia nyinyi Polisi waendesha mashitaka na akahitimisha kwa kusema mlaaniwe kwa kuwabambikizia kesi hizo za utakatishaji pesa mkiwa na lengo la "kuwakomoa" watuhumiwa hao ili waozee jela!

Nami niongezee kwa kumwomba Mungu wetu ili awalaani na kuwatia "uzezeta" hao Polisi wote wanaowabambikia kesi za utakatishaji pesa watuhumiwa kwa lengo tu la kuwasotesha kwa kipindi kirefu, watuhumiwa hao wasio na hatia.
 
Hajaguswa chochote, ila ni Unafiki tu ili aonekane yeye hahusiki kubambikiza watu kesi na kwa watu walioko mahabusu hajahusika.
Alaa kumbe Mkuu Mkaruka una maana kuwa yeye mwenyewe ndiyo "mastermind" wa hizi adha zote hizi zinazowapata hawa watuhumiwa wanaobambikiwa kesi za utakatishaji pesa?
 
hata siku watu wakipelekwa the Hague watarukana mita kama zote, tukisema mahakama zetu hazina uhuru ndio huko, hebu ona wanavyoshurutishwa wafanye harakaharaka kama watapatikana na makosa wafungwe au laa, ila kwa laani hii wanatakiwa wafungwe na sio kuachiwa eti wamekutwa hawana makosa!
 
Tuna Rais anayejali mno wananhi.
Pongezi kwa Rais kuona hilo, kwa hakika lilikuwa kikwazo kikubwa kwa upatikanaji wa haki za watuhumiwa kwa wakati.
 
Ala
hata siku watu wakipelekwa the Hague watarukana mita kama zote, tukisema mahakama zetu hazina uhuru ndio huko, hebu ona wanavyoshurutishwa wafanye harakaharaka kama watapatikana na makosa wafungwe au laa, ila kwa laani hii wanatakiwa wafungwe na sio kuachiwa eti wamekutwa hawana makosa!
Kumbe Mkuu kigogo warioba, kule kwa yule mama Fatou Bensouda, kushaanza kunukia?

Kumbe ndiyo sababu ya kuwaruka wenzie umbali wa futi elfu kumi?
 
Kuna mambo ya siasa ila hili si la siasa,haki ya mtu ni stahiki yake halali anayostahili kuipata kwa mda na mahali sahihi, niliwahi zungumza yakuwa mfumo wa mahakama wa tanzania ni mbovu sana unahitaji marekebisho makubwa,pia nguvu ya askar ni kubwa sana.

Na hii ndio tanzania yetu kila kiongozi kumlaumu aliyeko chini au juu yake,
Karibu tanzania!
 
Mystery,
Cha kujiuliza unamkamata mtu kwa hisia maana huna ushaidi. Unakamata kwa hisia halafu unakwenda kupeleleza huone kama ana kosa ndio muanze kesi.

Kwa hiyo muda wote umemfunga na labda mwisho wa yote unamuachia kwamba hana kesi ya kujibu ( nolle prosequi). Kweli hiyo ni haki.

Serikali nyingine angalau mtu anaweza kuwa compensated au mtu akafungua civil case kwa kuwekwa ndani bila makosa. Lakini si serikali hii
 
Ameguswa na EU & WB
Hata Mimi naona.

Hivi vichapo vya siku mbili hizi, mmmh.

Huku Marekani wampiga pini Mkuu wa mkoa wa Dar, Paul Makonda, asikanyage ardhi ya Marekani.

Huku world Bank wazuia mkopo wao wa matrillion..........

Na huku IPU, umoja wa mabunge Duniani wasikitishwa sana na vitendo vya uonevu wa hali ya juu anaofanyiwa Tundu Lissu........

Hata kama ulikuwa mtu jasiri kiasi gani, ni lazima unywee tu
 
Walijipendekeza sana kwa mheshimiwa Rais Magufuli lakini ameshtuka the same as Kangi Lugola case
Kama kichwa changu cha habari kinavyouliza hivi Rais Magufuli "ameguswa" na nini hadi awakenee waendesha mashtaka wanaochelewesha upelelezi wa kesi zilizoko mahakamani, jambo linalosababisha watuhumiwa wengi kuendelea kupata mateso ya hali ya juu, kwa kuendelea kusota rumande kwa kipindi kirefu sana?

Tunajua kuwa wapo watuhumiwa wengi ambao wako mahabusu kwa kesi za kubambika za utakatishaji pesa, ambazo wao waendesha mashitaka wanajua kuwa hazina dhamana, hivyo kuzitumia kama "fimbo" ya kuwatesea watuhumiwa hao ambao hawana hatia

Hebu tujaribu ku-imagine kwa mfano kesi ya mwandishi wa habari Erick Kabendera, huu ni mwezi wa 8, kila kesi hiyo inapotajwa hapo mahakamani, waendesha mashitaka hao, wanadai kuwa upelelezi hawajaukamilisha!

Hivi inawezekanaje kwa Polisi kupeleka kesi mahakamani, tena ya utakatishaji pesa, wakati upelelezi bado haukakamilika?

Hivi hiyo siyo njia tu ya kuwakomoa watuhumiwa hao wa utakatishaji pesa, kwa vile hao Polisi wanajua kuwa kesi hizo hazina dhamana?

Sasa Rais Magufuli amesema walaaniwe waendesha mashitaka hao, wanaosababisha mateso makubwa kwa watuhumiwa, kwa kuendelea "kuwasotesha" rumande.

Hata kama kwa mawazo ya wengi kuwa walidhani kuwa Jiwe ndiye "mastermind" wa kesi hizo, sasa keshawaruka futi 10,000.

Kwa hiyo kazi kwenu zigo lote la ubaya kawabakizia nyinyi Polisi waendesha mashitaka na akahitimisha kwa kusema mlaaniwe kwa kuwabambikizia kesi hizo za utakatishaji pesa mkiwa na lengo la "kuwakomoa" watuhumiwa hao ili waozee jela!

Nami niongezee kwa kumwomba Mungu wetu ili awalaani hao Polisi wanaowabambikia kesi za utakatishaji pesa watuhumiwa kwa lengo la watesi hao la kuwasotesha kwa kipindi kirefu, watuhumiwa hao wasio na hatia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom