Kama kichwa changu cha habari kinavyouliza hivi Rais Magufuli "ameguswa" na nini hadi awakenee waendesha mashtaka wanaochelewesha upelelezi wa kesi zilizoko mahakamani, jambo linalosababisha watuhumiwa wengi kuendelea kupata mateso ya hali ya juu, kwa kuendelea kusota rumande kwa kipindi kirefu sana?
Tunajua kuwa wapo watuhumiwa wengi ambao wako mahabusu kwa kesi za kubambika za utakatishaji pesa, ambazo wao waendesha mashitaka wanajua kuwa hazina dhamana, hivyo kuzitumia kama "fimbo" ya kuwatesea watuhumiwa hao ambao hawana hatia.
Hebu tujaribu ku-imagine kwa mfano kesi ya mwandishi wa habari Erick Kabendera, huu ni mwezi wa 8, kila kesi hiyo inapotajwa hapo mahakamani, waendesha mashitaka hao, wanadai kuwa upelelezi hawajaukamilisha!
Hivi inawezekanaje kwa Polisi kupeleka kesi mahakamani, tena ya utakatishaji pesa, wakati upelelezi bado haukakamilika?
Hivi hiyo siyo njia tu ya kuwakomoa watuhumiwa hao wa utakatishaji pesa, kwa vile hao Polisi wanajua kuwa kesi hizo hazina dhamana?
Sasa Rais Magufuli amesema walaaniwe waendesha mashitaka hao, wanaosababisha mateso makubwa kwa watuhumiwa, kwa kuendelea "kuwasotesha" rumande.
Hata kama kwa mawazo ya wengi kuwa walidhani kuwa Jiwe ndiye "mastermind" wa kesi hizo, sasa keshawaruka futi 10,000.
Kwa hiyo kazi kwenu zigo lote la ubaya kawabakizia nyinyi Polisi waendesha mashitaka na akahitimisha kwa kusema mlaaniwe kwa kuwabambikizia kesi hizo za utakatishaji pesa mkiwa na lengo la "kuwakomoa" watuhumiwa hao ili waozee jela!
Nami niongezee kwa kumwomba Mungu wetu ili awalaani na kuwatia "uzezeta" hao Polisi wote wanaowabambikia kesi za utakatishaji pesa watuhumiwa kwa lengo tu la kuwasotesha kwa kipindi kirefu, watuhumiwa hao wasio na hatia.