Rais Magufuli ameguswa na nini hadi kuwakemea waendesha mashtaka kwa kuchelewesha upelelezi kwa watuhumiwa wanaoozea jela?

Hata home mzazi ukiona watoto wanakuja juu kwa hoja nzito - unakunja ndita kutishia ujio wa hoja yoyote ile juu yako...ni moja technique tu za uongozi wa kibabe - hizi hawafundishi kwenye Principals of management..ni wewe tu kujiongeza.
 
Kwahiyo akiwafuta kazi hao uliowataja ndio kesi zitawahishwa na au kuisha mapema?
Huenda ikawa dawa kwa watakaoteuliwa kuzingatia maadili ya kazi zao na kuizingatia katiba kama Sheria mama na au kutoruhusu siasa kuingilia vyombo ya dola na mahakama!
 
Kati ya wale mawakili/ mahakimu watakao kwenda motono Magu yumo.. Akiwa kama mkuu wa nchi ana paswa kukemea hizi kesi za kubambikiza lskini yuko kimya. Sasa nani achomwe wa kwanza?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
POLICE anakubambikia mashtaka, -- Kumfurahisha boss. mwendesha mashtaka anapinga dhamana hata kama kosa lina dhamana -na kuchelewesha kesi kuwa upelelezi haujakamilika ---Kumfurahisha boss-- -. HAKIMU anakubaliana na polisi na mwendesha mashtaka -- Kumfurahisha boss . BOSSS NI NANI ???
JUSTICE DELAYED IS JUSTICE DENIED
 
Well said Mkuu viking

Hivi kwa uzoefu wako ndani ya utawala huu wa awamu ya tano, atawezaje kuliongelea suala hilo ambalo ni very serious issue, halafu IGP aendekee na kazi?

Kama hayo siyo maigizo ya dizaini ya Futuhi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…