Rais Magufuli amnyooshea kidole Mwele Malecela asema alitumiwa na mabeberu kutangaza ugonjwa 'hewa' wa Zika

Hivi Tanzania mamlaka huwa zinafanyaje kazi?

Mathalani kama kuna mlipuko wa ugonjwa mkubwa kama Zika, si kwamba kabla ya kujulikana kwa wananchi Rais inabidi afahamishwe na waziri husika?

Ilikuaje Mwele kutangaza tamko kubwa kama lile pasipo kuwa na backup ya waziri wake?
You got the point
 
Yule Mwele kwa hakika alitumiwa.
Inaonekana uelewa wako ni mdogo sana katika masuala ya afya.

Dr. Mwele hakuwahi kusena kuwa Tanzania kulikuwa na ugonjwa wa zika bali alitoa taarifa ya matokeo ya tafiti ambapo ilionekana kwenye sample za zilizochukuliwa kwa baadhi ya watu kuna vimelea vya vijidudu vinavyosababisha ugonjwa wa zika.

Tusiwe wendawazimu wa kujifanya tunaelewa kila kitu. Na wala tusiwe wapumbavu wa kudanganywa na maneno ya wanasiasa laghai.
 
Akielezea ni kwa namna gani humpelekea kufanya kazi hadi usiku Rais Magufuli amesema katika vita hasa ya kiuchumi adui mbaya zaidi hutoka ndani kwa maana ndiye huwa kiungo wa maadui wa nje.

Ametolea mfano wa aliyekuwa Mkurugenzi wa NIMR TANZANIA Bi Mwele Malecela alilazimika kumfuta kazi baada ya yeye kutoa taarifa za uongo kwamba wakati ule kulikuwa na ugonjwa wa Zika ilhali haikuwa kweli.'Je huo ugonjwa wa Zika ulionekana tena!?'alihoji Mheshimiwa Rais!

Amesema hali hiyo ya Mwele kuutangazia uongo Ulimwengu kuhusu uwepo wa zika Nchini Tanzania ilimkwaza sana na dhahili alionekana kutumiwa na washindani wa vita ya kiuchumi na Nchi yetu.

'Na ndiyo maana baada ya kumfuta kazi wiki moja baadae waliomtumia walimpa kibarua kingine'alisema Mheshimiwa Rais.
Ile ttheory inaitwaje?
Mwele ni mama mlezi wa Mange Kimambi.
Mange Kimambi alikuwa shabiki mkubwa wa JPM wakati wa kampeni lakini baada ya pale akawa adui nambari wahedi.
Mwele alijitosa kuwania U raisi kupitia CCM (???)
Nawaza tu!
 
Inaonekana uelewa wako ni mdogo sana katika masuala ya afya.

Dr. Mwele hakuwahi kusena kuwa Tanzania kulikuwa na ugonjwa wa zika bali alitoa taarifa ya matokeo ya tafiti ambapo ilionekana kwenye sample za zilizochukuliwa kwa baadhi ya watu kuna vimelea vya vijidudu vinavyosababisha ugonjwa wa zika.

Tusiwe wendawazimu wa kujifanya tunaelewa kila kitu. Na wala tusiwe wapumbavu wa kudanganywa na maneno ya wanasiasa laghai.
Haswaaa
 
Hivi Tanzania mamlaka huwa zinafanyaje kazi?

Mathalani kama kuna mlipuko wa ugonjwa mkubwa kama Zika, si kwamba kabla ya kujulikana kwa wananchi Rais inabidi afahamishwe na waziri husika?

Ilikuaje Mwele kutangaza tamko kubwa kama lile pasipo kuwa na backup ya waziri wake?
Kwa akili yako unaamini hakuambiwa?

Je unakumbuka lile sakata la kikokotoo kwa wastaafu? unadhani alikua hajui kama kuna kuna swala la kikokotoo mpaka baadae akafunika kombe kwa kumtumbua yule mama?
 
Sometimes it needs to be smart or intelligent enough to understand the intelligent person.

Pia,wakati mwingine inahitaji uwe expert kumuelewa expert.
Pole mgonjwa wa Zika wa mwele malecela mbona hukujitokeza kudai kuwa unaumwa kipindi kile.
 
Mzee ana chuki na kila mtu, kumfuta kazi kwake ndo alitegemea na Mungu afute ridhiki yake ama,yaan utadhani yeye ndo mtoa ridhiki
Yaani badala ya kujisikia aibu kuwa yeye alimshusha SAA 7.30 usiku Mungu akampandisha chati SAA 4.00 asubuhi?
Hivi Mwale na Magu kwenye hilo nani mshindi? Riziki ingekuwa anaigawa yeye kuna watu wangekuwa wameshakufa kwa njaa
 
Akielezea ni kwa namna gani humpelekea kufanya kazi hadi usiku Rais Magufuli amesema katika vita hasa ya kiuchumi adui mbaya zaidi hutoka ndani kwa maana ndiye huwa kiungo wa maadui wa nje.

Ametolea mfano wa aliyekuwa Mkurugenzi wa NIMR TANZANIA Bi Mwele Malecela alilazimika kumfuta kazi baada ya yeye kutoa taarifa za uongo kwamba wakati ule kulikuwa na ugonjwa wa Zika ilhali haikuwa kweli.'Je huo ugonjwa wa Zika ulionekana tena!?'alihoji Mheshimiwa Rais!

Amesema hali hiyo ya Mwele kuutangazia uongo Ulimwengu kuhusu uwepo wa zika Nchini Tanzania ilimkwaza sana na dhahili alionekana kutumiwa na washindani wa vita ya kiuchumi na Nchi yetu.

'Na ndiyo maana baada ya kumfuta kazi wiki moja baadae waliomtumia walimpa kibarua kingine'alisema Mheshimiwa Rais.
Jiwe amesoma Chemistry lakini hajaelimika. Sikutegemea Mwanasayansi kama yeye aje na argument ya uharo namna hii.

Kwanza kabisa NIMR ndiyo chombo cha juu nchini kinachotambulika kisheria katika utafiti wa magonjwa. Yeye kama Rais alitumia vigezo gani kujua ugonjwa upo au haupo?

Kwa mujibu wa Sheria na protocol za NIMR, wakiona dalili ya ugonjwa kutokana na Epidemiology report inayotayarishwa na idara ya kinga ya wizara watafanya utafiti kwa kuchukua sampuli. Na wakijiridhisha watatoa taarifa kwa ajili ya kutahadharisha wananchi.

Jiwe anasema eti ugonjwa haukuwapo wakati yeye ni mbumbumbu kwenye sayansi ya binadamu na magonjwa.

Watumishi wa Afya waliogopa sana kusema ukweli kwa kuwa wagonjwa wa zika walikuwapo. Na uwoga huo ukaendelea hadi kwenye dengue. Ugonjwa wa homa ya Dengue umeua watu zaidi ya 2000 tangu ulipoingia katikati ya 2018 hadi June 2019.

Watumishi wa afya wameamua kukaa kimya na kazi wamemuachia Waziri na Rais ndiyo wawajibike.
 
Sijui dr Mwele alimkosea nn mh Raisi?! Dr Mwele atumwe na mabeberu ili iweje ? Kwa uchumi upi tulionao adi hao mabeberu waweke vita na Tanzania? [emoji27][emoji27]

Hisije ikawa Lemutuz alimfitinisha dada yake wa kufikia kwa Mh Raisi kwa kupitia Bashite

Lemutuz na watoto halali wa Malecela hawaelewani kwa Sababu ya tabia zake
Ni chuki tu hata leo akiulizwa jiwe hataleta sababu ya msingi kuhusu Dr Mwele
 
Akielezea ni kwa namna gani humpelekea kufanya kazi hadi usiku Rais Magufuli amesema katika vita hasa ya kiuchumi adui mbaya zaidi hutoka ndani kwa maana ndiye huwa kiungo wa maadui wa nje.

Ametolea mfano wa aliyekuwa Mkurugenzi wa NIMR TANZANIA Bi Mwele Malecela alilazimika kumfuta kazi baada ya yeye kutoa taarifa za uongo kwamba wakati ule kulikuwa na ugonjwa wa Zika ilhali haikuwa kweli.'Je huo ugonjwa wa Zika ulionekana tena!?'alihoji Mheshimiwa Rais!

Amesema hali hiyo ya Mwele kuutangazia uongo Ulimwengu kuhusu uwepo wa zika Nchini Tanzania ilimkwaza sana na dhahili alionekana kutumiwa na washindani wa vita ya kiuchumi na Nchi yetu.

'Na ndiyo maana baada ya kumfuta kazi wiki moja baadae waliomtumia walimpa kibarua kingine'alisema Mheshimiwa Rais.
anapigana vita nanani huyo hata mabomba ya SINDANO anapewa msaada. atwambie kwenye bajeti kuna shiling ngapi za kuhudumia watoto (child protection)
 
Back
Top Bottom