Rais Magufuli amteua Brigedia Jenerali Charles Mbuge kuwa Mkuu wa JKT, aliyekuwepo apelekwa Mgambo

Rais Magufuli amteua Brigedia Jenerali Charles Mbuge kuwa Mkuu wa JKT, aliyekuwepo apelekwa Mgambo

JKT linaongozwa na Brigadia General? Sio Major General?
Hata Isamuyo aliteuliwa kuwa mkuu wa JKT akiwa brigadier general akapandishwa cheo baadaye

Ni wazi kwamba atapandishwa cheo kwasababu hakuna kamandi inayoongozwa na brigadier general.
 
Kambi za Jeshi la Akiba la Mgambo zipo wapi kwa hapa Dar es Salaam? Nataka nikamsalimie mkuu wa jeshi Hilo adhimu
. Kwa tuliokulia Dar miaka ya 90 tunajua namna jeshi hili lilivyokuwa likitamba hapo Msimbazi na Uhuru wakati huo kukiwa na "round about" 😄
 
Duuh kutoka mkuu wa JKT mpaka mkuu wa migambo hii ni hatari aisee, itakuwa amefanya kosa kubwa sana
Mbona Hakuna "Demotion" hapo! CMG ni nafasi kubwa tu katika kamandi ya Kijeshi. Anabakia kuwa miongoni mwa ma "Chief" na wa JWTZ. Si kila mabadiliko ni kwamba sababu ya kuvurunda, hapana. Inawezekana Rais ameona aliyekuwa "Chief" wa National Service (CNS) angeweza kutumika vizuri zaidi kama CMG na huyu mpya kama CNS.
 
Mbona Hakuna "Demotion" hapo! CMG ni nafasi kubwa tu katika kamandi ya Kijeshi. Anabakia kuwa miongoni mwa ma "Chief" na wa JWTZ. Si kila mabadiliko ni kwamba sababu ya kuvurunda, hapana. Inawezekana Rais ameona aliyekuwa "Chief" wa National Service (CNS) angeweza kutumika vizuri zaidi kama CMG na huyu mpya kama CNS.
Sawa mkuu nashukuru kwa ufafanuzi
 
Naona kuna ukweli kwenye hili mkuu , majina ya vijana wa ajira mengi siyo ya wale waliojenga ukuta
Kuto wasimamia waliojenga ukuta wa mereran kuajiri na kupewa ajira vijana wengine na waliojenga ukuta kuludishwa nyumbani.
 
Kumbuka aliyekuwa Inspector General wa Police miaka 90 Mahundi aliteuliwa kuwa IGP kutoka RPC Arusha na cheo cha SSP wakati kulikuwa na makamishna wakubwa makao makuu ya jeshi hilo. Kuteuliwa kwa mtu ni kutokana na utendaji wake mzuri
Hongera kutukumbusha...hata jaji nyalali(km nakumbuka vema) pia alikua so juniour kwa wenzake na hakuamini alipoteuliwa mpaka kwenda kumuuliza rais alihis hastahili na kuna wengine wamekuwa sinior kwake why yeye?
 
Rais wa Tanzania, John Magufuli amefanya mabadiliko ndani ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa kumteua bosi mpya wa jeshi hilo na kumhamisha aliyekuwepo.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Septemba 10, 2019 jijini Dar es Salaam amesema Rais Magufuli amemteua Brigedia Jenerali Charles Mbuge kuwa Mkuu wa JKT.

Jenerali Mabeyo amesema aliyekuwa Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Martin Busungu ameteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la akiba (mgambo).

Busungu aliyeteuliwa kushika wadhifa wa juu ndani ya JKT, Februari 16 mwaka 2018 alichukua nafasi ya Meja Jenerali Michael Isamuhyo ambaye alistaafu.

Aprili 13, 2019 wakati Rais Magufuli akizindua mji wa kiserikali wa Ihumwa Dodoma, alitangaza kumpandisha cheo Mbuge kutoka Kanali na kuwa Brigedia Jenerali kutokana na kazi nzuri aliyoionyesha ya kusimamia ujenzi huo.

Mara baada ya kumtangaza, alimuita mbele Brigedia Mbuge kwenda kukaa kwenye jukwaa kuu sehemu inayotengwa kwa ajili ya viongozi wakuu na siku hiyo hiyo eneo hilo, Mbunge alivalishwa vyeo vya Brigedia Jenerali.

Chanzo - Mwananchi
Leo wote marehemu.
 
Back
Top Bottom