Usiwe na wasiwasi mkuu.
Msalika anakuwa naibu na "understudy" na Dr Kipilimba ndio anatengeneza masuala mbalimbali ya kiutawala.
Kiufundi inaonekana Msalika ndie mtendaji wa masuala muhimu zaidi.
Tumwache mheshimiwa raisi apige kazi, achague watu anaowaamini na baadae awe na timu nzima aliyoiteua yeye.
Hiyo ipo kila mahali.
Hata kule Uingereza tulisikia yule mama Thereza May baada tu ya kuapishwa akamwita George Osborne na kumtimua siku hiyohiyo na baadae kusafisha watu wengi waliokuwa chini ya David Cameron na sasa ana timu yake anayoiamini itafanya kazi nae.
Tuwe tunaenda pia na kwa kuangalia mifano halisi, na hukumu ya haya anayofanya raisi kwa sasa ingoje siku yake atakapoachia ngazi kama alivurunda au la.
lakini kwa jinsi nchi hii inavyosukwa kwa sasa, inabidi tumpongeze mheshimiwa raisi kwa kuanza na ujenzi wa utawala wake kwanza.