Mkuu, inaelekea huna taarifa kamili.
Kwanza huelewi kwamba BOT pengine ni lazima iwe na watu kutoka idara mbalimbali za serikalini khasa serikali kuu.
Pili, unaonyesha bado huna habari ya kutosha kuhusu Dr Kipilimba na sababu za kuzungukazunguka kati ya BOT, NEC, NIDA na sasa TISS.
Kuna jamaa mmoja wa IT pale NEC anaitwa Madaha nae ni mtalaam ila kuna baadhi ya matatizo ya ujazo wa Data, yalijitokeza katika mfumo mzima wa uwasilishwaji wa matokeo "bottlenecks" labda ndio Dr Kipilimba akaombwa aende pale.
Dr Kipilimba hata humu JF ni active member na anawasoma wale "people of interest" kwa ukaribu, na sidhani kama atachukulia hii "seriously".
Hata hivyo kama hufahamu kuna kitu kinaitwa "baadhi yao" hiki ni muhimu sana kukielewa, sanasana tutaishia kuambiwa hadithi za hapa na pale tu.