Rais Magufuli amteua Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania

Rais Magufuli amteua Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania

Heshima kwa Magufuli kwa kutunza siri za serikali.....ingekua kwa JK sasa hivi akina Riz wangekuwa wameshavujisha!
 
Magufuli leo anacheza karata muhimu itakayoamua hatima yake ya miaka mitano ya utawala wake.

Ni ale au aliwe. Ngoja tuone kama Rimoti itafanya kazi toka Msoga.
 
Wanabodi,

Naangalia bunge live kutoka Dodoma, suala la Jina la Waziri Mkuu kutangazwa leo Bungeni kumepelekea bunge kukumbwa na hali ya Kisebusebu na Kiroho Papo!.Wabunge Roho Juu mcheche wa hali ya juu, PM atakuwa nani?!. Ama Kweli Magufuli Kiboko!.

Tusubiri.

Mimi hapo nilipo nashindwa kutoka home!. Zamani kulikuwa na vile vi mobile vya Star Times, sasa havipo!. DSTV Mobile kupitia Vodacom imesitishwa!. Simu TV naiona kama uzushi tuu, kila saa umestuck, hivyo nimeamua kusubiria tuu hadi hilo jina litangazwe ndipo maisha yaendelee!.

Tusubirie pamoja!.

Pasco
 
Muhongo anafaa sana lakıni uteuzi wake utamfanya Magufuli aanze kuandamwa na media mapema sana tena wakiongozwa na Mengi.
 
Back
Top Bottom