Wanabodi,
Naangalia bunge live kutoka Dodoma, suala la Jina la Waziri Mkuu kutangazwa leo Bungeni kumepelekea bunge kukumbwa na hali ya Kisebusebu na Kiroho Papo!.Wabunge Roho Juu mcheche wa hali ya juu, PM atakuwa nani?!. Ama Kweli Magufuli Kiboko!.
Tusubiri.
Mimi hapo nilipo nashindwa kutoka home!. Zamani kulikuwa na vile vi mobile vya Star Times, sasa havipo!. DSTV Mobile kupitia Vodacom imesitishwa!. Simu TV naiona kama uzushi tuu, kila saa umestuck, hivyo nimeamua kusubiria tuu hadi hilo jina litangazwe ndipo maisha yaendelee!.
Tusubirie pamoja!.
Pasco