Rais Magufuli amteua Prof. Sylvester Mpanduji Mkurugenzi SIDO

Bravo Dr. Mmbando. Ukiamua tu kuingia Hosp binafsi una uwezo wa kufanya kazi zako ukapata over 20m a month na ukaishi kwa amani sana. Umefanya maamuzi ya busara sana. Eng Omari imakuwaje tena?
 
Duu hongera ake, bonge la mwalimu asee, idara ya Uhandisi SUA inazidi kuondokewa na walimu wazuri....
Dah! Sasa huko vyuoni tutabakiwa na wahadhiri wenye uwezo wakuitwa wahadhiri?maana naona mkuu wa kaya anatunyanganya ma professor wote wazuri, huu ni mtizamo wangu binafsi
 
Yaani hamuwezi kuamini. Wakati namaliza kusikiluza eng omari bakari, itv dak 45 cha Sam Mahera, nafungja jf nakuta uteuzi umetenguliwa. Itv walitakiwa kuwa makini kurusha kipndi hicho
 
Hongera sana mwalimu wangu, Professor Mpanduji,....ulinifundisha kozi ya Agricultural Engineering katika kampasi ya Sohlomon Mhlangu na sasa nimekuwa mhandisi wa mitambo niliyeiva.

So, unampa hongera kwa kuwa kaula au unafikiri anaweza kuongoza SIDO? Unafikiri namna nzuri ya kumtumia Prof. Mpanduji, ni kumteua kuongoza SIDO? Afadhali hata angekuwa ameomba mwenyewe tungejua hataki tena kufundisha na kufanya tafiti za uhandisi wa kilimo. Zaidi ya kufundisha, hebu tupe uzoefu wa Prof. Mpanduji kuongoza/kusimamia maendeleo ya viwanda? Baada ya kuondoka Prof. Mpanduji, ni maprofesa wangapi wa agricultural engineering wamebaki pale SUA? Rais wetu ana assume kwamba mtu akiwa profesa basi ni kiongozi mzuri. He will be disappointed. Na kuna athari zaidi ya kuteua maprofesa kama anavyosema Mahmood Mamdani:

"The African Universities have now turned out to be places where intellectuals are mainly interested on consultancy, politics and power while forgetting the intellectual roles of universities. Most of them are now individual NGOs and people aspiring to appointed in political positions. They should learn from Prof Mazrui who was only interested on ideas , universalism, knowledge and Public Intellectualism."

When you are aspiring to be appointed by rulers, you are not doing research anymore. You are not speaking research. You are speaking what you think rulers want to hear. You cease being an intellectual.

Magufuli amekaa miezi 6 tu madarakani lakini ameshasababisha athari kubwa sana kwa elimu ya juu hapa nchini kuliko JK katika kipindi chake chote cha miaka 10. Kila siku anateua maprofesa kushika nafasi mbalimbali. Ni kama vile kuna mtu amemwambia wako wengi sana huko vyuoni na hivyo wanahitaji kupunguzwa. It's a shame.
 
Yaani hamuwezi kuamini. Wakati namaliza kusikiluza eng omari bakari, itv dak 45 cha Sam Mahera, nafungja jf nakuta uteuzi umetenguliwa. Its alitakiwa kuwa makini kurusha kipndi hicho
Alikutakiwa asirushe maana uteuzi ulijulikana toka mchana
 
Saizi ukiwa na jina la Kisukuma tu unakamata shavu. Wakuu wa mikoa wasukuma wako tisa kati ya makabila 130 ya Tanzania
Acheni wivu,wasukuma tumepiga shule na tunachaguliwa kihalali kabisa,kama nyie mlikimbia umande poleni
 
'' Sylvester '' Daah. akina ABDUL mtaisoma namba awamu hii. mtaishia kufuturishwa tu huku nchi ikiliwa na mashemasi.

CCM Mbele kwa mbele
hili bandiko lako akiliona yule kamanda wa dares salaam atakushukia kama gwajima kwa uchochezi
 
Magu alisema wametisha ajira serikalini hizi teuzi siyo ajira ?
 
Suala la teuzi kuelemea kanda ya ziwa liko wazi.
 
Mpanduji ni mmoja tu nami alinifundisha Food Engineering (basic Drawing) pale SUA.Watu wakiiambiwa ni Vi.la.za wanafura ila kwa kufuatilia post hii wachangaiji zaidi ya 90% ni vila.za! Afu cha kuongeza,Mpanduji sio Msukuma ila ni bonge la Prof aise,naamini SIDO sasa ndo itashughurika vizuri na uundaji wa mashine ndogo ndogo kwa ajiri ya ujasirimali kwa gharama nafuu
 
Uteuzi bomba ila nafasi kama hizi si hata Waziri wa viwanda na biashara anaweza kuteua, na huyo mwingine hata waziri wa Afya anaweza kuteua!! Madaraka kwa Rais sasa ni kero.

Inatia kinyaa kwa kweli, kila kitu anafanya yeye, sasa hata maafisa wa polisi kupandishwa vyeo nayo ni kazi ya Rais, hili ni taifa la kipuuzi mno.
Kutokuwepo na taasisi imara katika nchi ambazo zinajitegemea ni udhaifu mkubwa kuliko hata ufisadi, maana ni kwamba hata namna gani zifanye majukumu yake ni mpaka Rais atoe maelekezo. Tunafanana na mtoto mdogo ambaye anakunywa uji tu miaka yote na hakui akala chakula cha kawaida wanachokula wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…