GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,880
- 11,134
Rais Mzalendo na anayejali wawekezaji leo kupitia Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila ametoa tamko au salamu kuwa SUGU au Mbunge mstaafu wa Mbeya Joseph Mbilinyi ni muwekezaji hivyo atalindwa na hotel yake haitabomolewa na mtu yeyote.
Kulikuwa na uzushi mitandaoni kuwa hotel imejengwa kwenye uoto wa asili yaani pembezoni mwa mto hivyo kulikuwa na mpango wa kuibomoa.
Kwa ufupi Rais amesisitiza hilo eneo limepimwa na linafahamika,Watu wa mazingira yaani NEMC wanalifahamu vizuri.
Mkuu wa mkoa ameonyesha jinsi Sugu anavyolinda mazingira ya mto huo huku maji yakitiririka na kumiminika.
Aidha Bwana SUGU amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuhakikishia hilo na kujenga imani kwa wawekezaji wengine.
Maendeleo hayana chama