Rais Magufuli amtuma RC wa Mbeya kusitisha uvunjaji wa Hotel Desderia inayomilikiwa na Joseph Mbilinyi (Sugu) kwa kisingizio cha mazingira

Mimi binafsi nafikiri hao watendaji walipata kiburi toka ‘juu’! Ila aliye huko ‘juu’ kaamua kwa maslahi ya kisiasa, ili kuwaaminisha ‘wadanganyika’ kuwa maendeleo hayana chama; na kuwa anawapenda sana wawekezaji!
 
Looooh Wanikumbusha Shamba la mboga la Mbowe lililofyekwa na kuharibiwa kabisa. Kisa et kalima Kandokando ya mto. Ukipita Nchi hii kuna watu wengi wamejenga na kulima kwenye kingo za MiTo Kwa Raha zao. Pongezi za dhati zimwendee Rais Kwa hiyo Stop Order.
 
Ingebomolewa ungesema ni uonevu sasa haijabomolewa unatukana. Hivi ulitaka nini haswa?
Makamanda ni wazuri sana kwa kuhamisha 'goal post', akiona jambo limeelemea upande huu anabadili gia angani ili apate cha kulaumu au kupinga. Wakati mwingine mpaka najiuliza sijui hawa watu wanatumia nini kufikiri!
 
FUTUHIIII NDIO NI FUTUHI.
 
Baada ya Makubaliano ya Siri kuwa atahamia Kwao kwani hata aliyezuia alishaonyesha Kumkubali wakati wa Kampeni sasa ndiyo tunazugwa mno.
 
Yale yale maigizo ya Kutengeneza tatizo gizani then unaibuka kwenye nuru/mwanga unalitatua na Kupigiwa makofi mengi ya pongezi.
 
Usisahau kuwa Sugu alitumia influence yake kama mbunge kuwarubuni waliompa kibali,au umesahau alivyokuwa akijinasibu kuwa yeye ni raisi wa Mbeya na umeshasahau kuwa Mbeya mjini madiwani karibu wote walikuwa Chadema,nani angemkwamisha Sugu kupata kibali cha kujenga kwenye chanzo cha maji?hapa sio siasa bali ni kufuata utawala wa sheria ,na si hata marehemu Lwakatare nae alijenga kwenye njia ya maji wakati sheria zipo wazi kuhusu ujenzi, hii tabia ikiendelea mwisho wake utakuwa mbaya na basi tufute sheria zilizowekwa kuhusu ujenzi kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi kujengwa. Sheria ni msumeno,kuzembea kwa wasimamizi hakuhalalishi watu kuvunja sheria, kuwa na vibali sio sababu je mazingira ya kutolewa hivyo vibali yakoje? hata marehemu mama Lwakatale alikuwa na vibali ingawa kajenga kwenye mkondo wa maji.
 
Niliwahi kusema JPM is a very considerate person, ni Msikivu, mwenye huruma na anae jali
sana.

P
 
hao waliotaka kubomoboa WAKIWA NA NIO OVU HUKU MKUU WA MKOA AKISEMA KUNA WATU WANATAKA KUGOMBANISHA KISIASA BADO WANAACHWA WAENDELEE NA KAZI?yakimkuta mtu ambaye hana jina la kisiasa kama sugu itakuwaje?hawakutumwa na mamlaka za juu?wafukuzwe kazi haraka ili wasiumize wawekezaji wengine
 
Aiseeee leo umepakia vitu Kichwani??? Umeandika kwa fujo mnoooo
 
Ila Sugu naye bwana,mkuu wa mkoa anamwambia nina maelekezo ya Mh. Rais yeye Sugu ukiisoma kisaikolojia midomo yake na macho yake alitegemea kusikia jambo baya juu yake,anaonyesha ni mtu wa kutaka kushambulia kila wakati lakini kinyume chake akasikia mazuri kutoka juu.
Inaonekana bado ana tabia mbaya.Sasa ajifunze kwamba yeye ni mfanya biashara kama wafanya biashara wengine na abadilike.
Ila kwa upande wa pili namsifu sana Sugu kwa kuwa mbunifu kwani wabunge wengine wengi waliodondoka hawajui hata waanzie wapi.Nilimkuta mmoja anajaza form BRELA online anataka kufungua ofisi ya kuuza vifaa vya stationary,yaani ndiyo anaanza sasa baada ya uchaguzi kwisha .Na wengine ndiyo kama hivyo mlivyosikia wanaona kabisa nje ya ubunge hakuna tena maisha,mtu anaamua kujibeba yeye na familia yake anakimbia nchi anajifanya mkimbizi wa kisiasa.Hapo hakuna,mkimbizi wa kisiasa wala nini ila hali yao mbaya.
 
kwa hiyo hadi kamera zimewashwa sugu alikuwa hajui nini kinaongelewa? is that your point?aliongea kwa kujiamni akisema yeye hakuwa na wasiwasi sababu vibali vyote anavyo(AKA CHUCKLE)akasema unless otherwise..(maagizo toka juu)
hao waliokuwa wanatishia wakaambiwa na mkuu wa mkoa wanataka kugombanisha watu kisiasa ni kina nani?what if sugu asingekuwa na nguvu ya kisiasa ina maana angevunjiwa hata kama enviromental impact study ilifanyika?HUU NI UTOTO SANA YAANI HATA KAMA KWELI YUKO CHANZO CHA AJI KAAMUA MTU MMOJA BASI YAMEISHA?
WALIOTAKA KUVUNJA HIYO HOTEL WAFUKUZWE KAZI HARAKA SANA IWE FUNZO KWA WANAFANYA WATU HADI KUKIMBIA NCHI KUWEKEZA NA KUKIMBIZA HELA ZAO BANKS
 
Kwahiyo hapo inabidi amwabudu sana Magu, kwamba bila yeye hotel inabomolewa.

Hii nchi ni takataka, imejaa vibwengo wanaopenda kuabudiwa sana.

Tumieni akili; Sugu alikuwa na vibali vyote halali vya kujenga hiyo Hotel na vibali hivyo ndio vimemuwezesha kupata mikopo benki. Sasa kama hiyo hiyo serikali waliompa vibali vya kujenga wangeivunja hiyo hotel ,wao ndio wangekuwa liable kulipa hilo deni kama hiyo hotel ndio iliwekwa kama collateral ya mkopo!!

Hapo wanacheza mchezo wa kumtisha Sugu ili Jiwe aonekane kuwa mtu wa huruma kumbe yeye ndiye aliyewatuma kupeleka order ya kutaka kuvunja!!
 
Ingebomolewa ungesema ni uonevu sasa haijabomolewa unatukana. Hivi ulitaka nini haswa?

Rais wetu ni wa kila chama, kila kabila, kila dini, kila rangi, kila mkoa

Nchi yetu sio takataka mkuu ila mawazo yako uliyoyaandika hapa ndio takataka
Rais hakuwa na sababu ya kuruhusu ibomolewe sababu ujenzi wa Hoteli ulifuata taratibu zote. Kama ingebomolewa ingekuwa ni dhulma kubwa sana kwa Sugu.
 
Niliwahi kusema JPM is a very considerate person, ni Msikivu, mwenye huruma na anae jali
sana.

P

Acha kujitoa akili hapo pana huruma gani? Huyu bwana alikuwa na vibali vyote vya serikali vilivyomruhusu kujenga hotel; hawa NEMC wanatakiwa awachukulie hatua kwa kukiuka taratibu za serikali kwa kumuonea na kumsumbua muwekezaji!!

Angekuwa amekiuka sheria na Jiwe akajitokeza na kumtetea hapo ndio mgekuwa na hoja ya kusema ni mtu wa huruma!!!
 
Hivi mnafahamu gharama za walau nyumba ya ghorofa moja ya uhakika?Siyo chini ya TZS300M.Rais ameguswa na hiyo hasara.
I don't think so! Bro, investments zinadrop na hivyo soko la ajira + kodi vinaporomoka.

Rais lazima alishauriwa kupima faida ya kubomolewa Hoteli ya Sugu kwa sababu za kisiasa na Hasara itakayotokana na kuibomoa kwa sababu za siasa hizo hizo(sio kuvunja sheria ya NEMC) akaamua kutumia busara kuzuia kuivunja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…