Watanzania wengi wamefurahishwa na hatua ya Rais Magufuli ya kusimamisha nia ovu waliyokuwa nayo watendaji wa serikali ya kutaka kubomoa hotel I ya aliyekuwa mbunge wa Mbeya mjini kwa tiketi ya Chadema, Joseph Mbilinyi, maarufu kwa jina la Sugu.
Kwa bahati nzuri huyo Sugu ameeleza kuwa hoteli yake hiyo ilikuwa na vibali vyote vya mamlaka zinazohusika za kukamilisha ujenzi huo.
Swali linakuja hao watendaji waliotaka kuibomoa hotel I hiyo, walipata wapi kiburi hicho cha kutaka kuibomoa hoteli hiyo, wakati wakijua fika kuwa mwekezaji huyo ana vibali vyote vya mamlaka husika?
Kama hao watendaji hawajapata kiburi hicho kwenye mamlaka za juu za nchi, basi tunategemea hao watendaji waliokuwa na nia hiyo ovu watumbuliwe mara moja.
Kinyume cha hapo tutakuwa tunajenga nchi ambayo baadhi ya watendaji wanaweza kujiamulia mambo yao kwa lengo la visasi tu kwa ajili yakuwakomoa baadhi ya wananchi.
Kama kweli Rais Magufuli ameitoa hiyo kauli bila unafiki wowote, basi tunamtegemea awatumbue haraka hao watendaji wa serikali waliotaka kuibomoa hiyo hoteli, kinyume cha taratibu kwa lengo tu la kutaka kumkomoa Bwana Sugu.
Kwa kuwa sisi wananchi tunamjua Rais wetu kuwa ni mtu asiyetaka masihara hata kidogo na ni mwepesi sana wa kuwatumbua watendaji wake hata kwa "vijikosa" vidogo, basi tunatarajia kwa hawa watendaji wake ambao walitaka kubomoa hiyo Hoteli ya mamiloni ya shilingi za mwwkezaji mzawa wa kitanzania, ambaye amefiata taratibu zote za uwekezaji, basi tunatarajia atawatimbua mara moja ili kuondoa fikra za wananchi wengi kuwa huyo Sugu alitaka kukomolewa kwa kuwa ni kiongozi wa Chadema, hasa tulitilia maanani usemi maarufu wa Rais wetu Magufuli kuwa MAENDELEO HAYANA CHAMA