Rais Magufuli amtuma RC wa Mbeya kusitisha uvunjaji wa Hotel Desderia inayomilikiwa na Joseph Mbilinyi (Sugu) kwa kisingizio cha mazingira

Rais Magufuli amtuma RC wa Mbeya kusitisha uvunjaji wa Hotel Desderia inayomilikiwa na Joseph Mbilinyi (Sugu) kwa kisingizio cha mazingira

Haya ndiyo mambo ya kutufanya sisi kama hatuko timamu .

Sugu anamiliki eneo alilo jenga hotel kihalali, ana hati ambayo imetolewa na serikali.

Sugu amejenga hotel hiyo kwa kuzingatia taratibu zote za ujenzi ikiwa ni pamoja na kupewa Building Permit na serikali.

Baada ya ujenzi,amepewa leseni ya uendeshaji wa hotel na serikali.

Serikali inachukua kodi/ ada/ushuru kupitia TRA na Halmashauri na mamlaka nyingine za serikali kutoka kwenye hotel ya Sugu.

Katika mazingira kama hayo,unadhani Sugu ana kosa gani hadi hotel yake ibomolewe?

Yawezekana kweli ipo kwenye chanzo cha maji, lakini hotel hiyo imezungukwa na hotels nyingine pamoja na nyumba za serikali.Sasa inakuaje hotel ya sugu pekee ndio iwe kwenye chanzo cha maji?.

Kama kweli hotel ya Sugu iko kwenye chanzo cha maji, itatakiwa kubomolewa, lakini yote hayo yakifanyika basi, Sugu alipwe kila anacho stahili kama fidia kwakua alimilikishwa eneo kihalali,amejenga kihalali,anaendesha hotel kihalali na analipa kila kinacho stahili kulipwa serikalini kutokana na mapato yanayo tokana na hotel hiyo.

NB,Mashamba ya Mbowe yaliharibiwa vibaya mno, Watanzania wakapoteza ajira,Tanzania ikapoteza fedha za kigeni tulizo kuwa tukipata kupitia mauzo ya mazao hayo nje, hakuna anaye jali, tunajali kuumiza wanao tukosoa.

Kama hicho ndicho kipaumbele chetu, tuendelee kubomoa tu,sidhani kama ni Sugu pekee kutoka upinzani aliye wekeza ndani ya miaka 10,wapo wengi, bomoeni tu kama ndio njia ya kujenga nchi.
 
CLEVER BOY, SIO WALE WENGINE WALIOWEKEZA KWENYE MASHINE ZA KUSAGA . UMETUMIA UBUNGE WAKO VIZURI HUTAKUFA NJAA
Usidharau biashara,Kuna watu wako na mashine za kusaga kwa siku anapata faida zaid ya mwenye hotel
 
Anaejenga ni mwananchi mzalendo ila anaetoa kibali sio mzalendo. Huenda anaetoa kibali ni yule mwenye vyeti vya kugushi, anatakiwa awajibike ipasavyo .
 
Umesahau mkasa wa Billcanas?
Msikivu mwenye kujali ?🤣🤣
Si vema kulinganisha na issue ya Billcanas. Ya mmiliki wa club aliyeshindwa kulipa deni la pango NHC kwa miongo. Issue iliyoamuliwa kisheria na Mahakama Kuu.
 
Rais Mzalendo na anayejali wawekezaji leo kupitia Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila ametoa tamko au salamu kuwa SUGU au Mbunge mstaafu wa Mbeya Joseph Mbilinyi ni muwekezaji hivyo atalindwa na hotel yake haitabomolewa na mtu yeyote.

Kulikuwa na uzushi mitandaoni kuwa hotel imejengwa kwenye uoto wa asili yaani pembezoni mwa mto hivyo kulikuwa na mpango wa kuibomoa.

Kwa ufupi Rais amesisitiza hilo eneo limepimwa na linafahamika,Watu wa mazingira yaani NEMC wanalifahamu vizuri.

Mkuu wa mkoa ameonyesha jinsi Sugu anavyolinda mazingira ya mto huo huku maji yakitiririka na kumiminika.

Aidha Bwana SUGU amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuhakikishia hilo na kujenga imani kwa wawekezaji wengine.

Maendeleo hayana chama

View attachment 1659613
Kuna muwekezaji alikuwa mmiliki wa hotel iliyopo kitonga kwa sasa imekufungwa naye NEMC ilimfungia sababu yupo karibu na chanzo cha maji, naye aruhusiwe kuendeleza biashara yake.
 
Asiyeelewa! Angekataa ombi la kutaka amsugue,Hotel ingebomolewa tu! CCM Oyeee!
Kwa kweli JPM ni muungwana saanaa.
Tengeneza kesi, afu itatue mwenyewe; unajitekenya na kucheka mwenyewe! Uungwana gani hapo zaidi ya kutafuta sifa za kijinga tu?
 
Sidhani kama kuna watu wanaoeleweka kama hawa wanaofanya kazi kwa kufurahisha korido zao pale Lumbumba.
.
.
.
Wanampa kazi nzito mzee mkubwa (JPM) kuingilia na kutolea maamuzi issues ambazo kimsingi hazitakiwi kuwapo... Nadhani ni wakati wa mzee mkubwa kutimua hawa majamaa wanaozidi kupandikiza chuki na migawanyiko ya kitoto katika jamii zetu kwa kutumia ofisi za umma na siasa uchwara.
.
.
.
Sasa kwa kupitia nia yao ya kishetani wamesaidia kutangaza hoteli ya kaka mkubwa bure kabisa... Hopeful baada ya huu upupu kuna watu wamejua kuwa Mbeya kuna hotel ya Sugu na kutamani kufika.
 
Hata Dr. Shein huku Zenji alikuwaanasifiwa sana kwa utekelezaji waIlani ya CCM,
lakini leo kaingia Dr. mwinyi anasema serikali iliyopita ilikithiri kwa ubadhirifu wa mali za umma na rushuwa,
CCM Oyeee,
Create problem + Solve problem=Herro
 
Sasa kama ni hivyo kwanini itumike njia ndefu katika Kumshawishi ajiunge huko unakokuunga Mkono hadi muwafanye Watanzania Wapumbavu?
Njia ndefu ni Ile wanayotumia Tundu na lema kutafuta ukimbizi kwa kisingizio cha siasa
Mwacheni mzalendo Joseph Mbilinyi aka Sugu afanye uwekezaji kwa maslahi ya nchi yake
Na sasa ndio mtajua Sugu 98% ni bora kuliko Tundu
 
Rais Mzalendo na anayejali wawekezaji leo kupitia Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila ametoa tamko au salamu kuwa SUGU au Mbunge mstaafu wa Mbeya Joseph Mbilinyi ni muwekezaji hivyo atalindwa na hotel yake haitabomolewa na mtu yeyote.

Kulikuwa na uzushi mitandaoni kuwa hotel imejengwa kwenye uoto wa asili yaani pembezoni mwa mto hivyo kulikuwa na mpango wa kuibomoa.

Kwa ufupi Rais amesisitiza hilo eneo limepimwa na linafahamika,Watu wa mazingira yaani NEMC wanalifahamu vizuri.

Mkuu wa mkoa ameonyesha jinsi Sugu anavyolinda mazingira ya mto huo huku maji yakitiririka na kumiminika.

Aidha Bwana SUGU amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuhakikishia hilo na kujenga imani kwa wawekezaji wengine.

Maendeleo hayana chama

View attachment 1659613

nikimuangalia huyu RC na matamko yake ya siku za nyuma,mmh.Yaani viongozi wanaotegemeaboss kaamkaje!!RC alishindwa kutoa tamko kabla Rais hajaingilia?
 
Njia ndefu ni Ile wanayotumia Tundu na lema kutafuta ukimbizi kwa kisingizio cha siasa
Mwacheni mzalendo Joseph Mbilinyi aka Sugu afanye uwekezaji kwa maslahi ya nchi yake
Na sasa ndio mtajua Sugu 98% ni bora kuliko Tundu
Kwa Mbinu zenu za Kutishia Uhai wa Mtu au Kumtia Umasikini wa Kudumu kama asipokubaliana nanyi hata ingekuwa Mimi ningekuwa Mpole pia.
 
Nchi sadikika ....MTU anaanzisha ukorofi na kutaka kuvunja hotel....then heeeee anawazunguka kufuta hilo tamko aliloliasisi yeye !!! Jiwe acha tu !! Ubunge chukueni jela mtieni hotel muachieni na madeni yake bank ! Roho mbayaaaa tu hakuna lolote eti kamshukuru !!! Unafiki
 
CLEVER BOY, SIO WALE WENGINE WALIOWEKEZA KWENYE MASHINE ZA KUSAGA . UMETUMIA UBUNGE WAKO VIZURI HUTAKUFA NJAA
Hatakufa njaa kivip mkuu fikiria ilo swala lingetimia na hotel ikavunjwa???, dunia Ina mambo meng imeyaweka kwa jili yetu na siku zinavyo zid kwenda inaenda inatukabidh
 
Bora ilivyoachwa tu ingebomolewa ilibidi mnyororo mzima wa watendaji walioiidhinisha vibali vya ujenzi wote watolewe/watumbuliwe.
Kwani haingii akilini usemi leo anahatarisha chanzo cha maji na wakati toka mwanzo wewe ndo umeweka saini yako kwenye nyaraka kuidhinisha ujenzi ufanyike.
 
Mbona bilcana ya mbowe aliibomoa ikiwa na vibali vyote,labda roho mtakatifu kamuingia
 
Back
Top Bottom