Rais Magufuli amtuma RC wa Mbeya kusitisha uvunjaji wa Hotel Desderia inayomilikiwa na Joseph Mbilinyi (Sugu) kwa kisingizio cha mazingira

Rais Magufuli amtuma RC wa Mbeya kusitisha uvunjaji wa Hotel Desderia inayomilikiwa na Joseph Mbilinyi (Sugu) kwa kisingizio cha mazingira

Tujiulize je kuna wengine waliovunjiwa kama Mbowe, pamoja na kuwa walikuwa wapangaji wa NHC?

Kama jibu lilikuwa kavunjiwa Mbowe peke yake, inadhibitisha kuwa nchi hii ina "double standards" ya hali ya juu linapokuja suala la utekelezaji wa sheria za nchi hii, wakati huo huo Rais wetu haishi kusema kuwa Maendeleo hayana Chama!

Utawala wa Jiwe una double standards; kuna sheria za wasukuma na genge lake na sheria za hao wengine waliobaki!! Kudhihilisha hilo, ndio maana nyumba za Mwanza hazikivunjwa lakini za Kimara zilivunjwa!! You are asking about double standards?
 
Sasa ungewauliza wakupe data ndipo uje hapa,"No research no right to speak".

Hiyo taarifa ilitolewa na NHC kuelezea moja ya sababu za kuivunja BILLICANAS ,kwani kulikuwa na upotoshaji wa taarifa kuwa jengo lilikuwa mali ya Mbowe!!! Kutokujua Kiasi alichokuwa anadaiwa hakufuti deni linalomkabili!!
 
Huyo unaesema amekimbia anahotel nzuri jirani na lile hekalu la mengi,bado vitu vidogo ikamilike....yule katishiwa maisha sana na kukoswa mara kadhaa sio mjinga kuondoka nchini kwake
Umemaliza.Haijakamilika. Atatoa wapi pesa za kuimalizia akiwa hapa Bongo ?Acha akatafute dola Canada. After 5 yrs atarudi.
 
Lingekuwa na pigo jingine kwa Mr. Sugu. Heri Rais ameamua kuingilia kati. Zimwi likujualo.......!
Pigo kwa sugu?????
Kivipi.
Unajua ameajiri watz wangapi?
Kodi anayolipa sio chini ya mil 10kwa mwezi.

Ni pesa ndogo hio?

Hii serikali ina watu wapumbavu
 
Siasa ni game,ukute mzee ndio aliruhusu jamaa wafanye hivyo huku akijua kuwa baadaye atawazuia ili kujitengenezea umaarufu wa kupendwa na wananchi.Siasa inadeal Sana na kucheza na akili za Watu.
Wabongo tumeisha mshitukia,nafsi yake Haina armani kwa maovu aliyoyatenda tangu aingie Ikulu,nchi imemshinda kuongoza,yaani Swala la hotel,mpaka litatuliwe na Ikulu!!!
Kuna RC,DC,RAS,DAS,Takukuru Mbeya,Polisi,maofisa wa mazingira,Hawa wote walikuwa wapi wakati agizo la kubomoa linatolewa,na ishu ya kubomoa Jengo,ni Swala dogo sana ilibidi liishie ngazi ya mkoa au wilaya,sasa yeye jiwe alijuaje akiwa Ikulu,au ndio kutafuta Kiki nyepesi,
Mashule hayana madawati,Raisi mzima anakimbilia kutatua ka ishu ka wilayani,
Kama sio yeye aliyetoa maagizo,harafu akaandaa Bongo muvi
 
Usanii ule ule!!! Cause the problem and help solve it so that you are praised???
Hayo hayo ya madini!!!Leo wanambakizia Lissu ambaye alipigania haki za watu kuhusu uchimbaji holela wa madini maisha yake yote!
Waliokula rushwa na kusaini mikataba hovyo wameondoka scot free! Mambo ni ujanja ujanja no integrity!!
 
Mbona bilcana ya mbowe aliibomoa ikiwa na vibali vyote,labda roho mtakatifu kamuingia
Ni kweli kuna muda mwingine unaweza kuwa unafanya mambo ambayo hata mwenyewe nafsi inakusuta.
Mwisho unavaa uhusika ingekuwa mimi ndo navunjiwa hiyo hoteli hasara ya mamilioni nimewekeza. Unaamua bora kuacha tu isibomolewe, vinginevyo hayo machozi hayawezi kwenda bure.
 
Sugu amesimama kwa adabu zote, ule umwamba wa rais wa Mbeya wote umepotea. CCM ni balaa.
 
Tunampongeza Rais wetu anayewajali na kuwalinda wawekezaji wa NDANI bila kujali vyama vyao,
Ila sasa ilikuwa inataka kubomolewa kwa mujibu wa sheria au kwa bifu za Kisiasa na kukomoana?

Sasa Rais wetu mpendwa akimaliza muda wake 2025 tunajuaje kama anayekuja hataendeleza hiyo nia mbaya ya kubomoa Hoteli hiyo? Kwa nini Bunge letu tukufu lisitunge sheria KALI ya kuwalinda wawekezaji wa NDANI zikiwepo NGOs, Viwanda au Makampuni na kuwashughulikia watu wenye nia mbaya ya kuwakwamisha wawekezaji?
Mungu alivyo mwema, Wizra ya uwekezaji ipo chini ya Rais na Waziri wake ni Professor-who knows better about investment opportunities in the country.
Hongera RC,
Asante Rais wetu--mtetezi wa wanyonge
Akili za watanzania wengi zimebuma hawawezi kuona wala kuwaza tena! Hivi kweli unaamini kuwa waliokuwa wanataka kubomoa hawajatumwa na huyo huyo anayejitia "kumuonea huruma mnyonge"?
 
Basis tuu wamemlinda dogo lkn wakiamua kuiporomosha wanaporomosha hawaangalii hayo...mbona Mbowe shamba lake lilisambaratishwa akashinda kesi lkn hadileo havieleweki
 
Updates:
RC wa Mbeya Mh. Albert Chalamila amesema kuwa hoteli ya Desderia inayomilikiwa na Aliyekuwa mbunge wa mbeya mjini Mh. Joseph Mbilinyi (SUGU) haitabomolewa maana imefuata taratibu za ujenzi.

"Kwani imepita vyanzo vya maji? Vibali vyote vimefuata mlolongo mzima na maji yanatunzwa vizuri na hayajakauka" aliyasema hayo RC Chalamila.

Hata hivyo RC Chalamila ameeleza kuwa ameagizwa na Rais John Pombe Magufuli, "Hakuna mtu yoyote atakaye kuja kuigusa na kuibomoa kwani Sugu ni mwekezaji kama wawekezaji wengine" ujumbe huo ni wa Rais John Pombe Magufuli.

Sugu ameeleza kuwa ujumbe wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli utasaidia wawekezaji wengine kujiamini pindi wanapopata nafasi kuwekeza mkoa huo.

Source Jamiiforum instagram page.
 

Attachments

  • 20201228_085330.jpg
    20201228_085330.jpg
    26.1 KB · Views: 4
  • 20201228_085419.jpg
    20201228_085419.jpg
    43.6 KB · Views: 4
HAWAWEZI KUIBOMOA KWA SABABU KWANZA AMESHINDWA UBUNGE NA PILI AMEUACHIA UBUNGE ULE KWA AMANI BILA PURUKUSHANI ZOZOTE,NAHISI KUNA MAKUBALIANO YA SIRI KABLA YA KUIACHIA HOTEL HIYO
 
Back
Top Bottom