Rais Magufuli amualika Sultan mpya wa Oman kutembelea Tanzania wakati wowote

Rais Magufuli amualika Sultan mpya wa Oman kutembelea Tanzania wakati wowote

Kwani Gerson Msigwa alishafukuzwa kazi? Maana naona toka subuhi wewe ndio unatoa habari za mkulu
 
Kwanini na yeye asifanye kujenga hizo barabara,vituo vya afya kwa kutumia pesa zake za mfukoni?
Mikedean naona unaweweseka kila akitajwa JPM na CCM ghafra unaona kiwewe inabidi uzoee tu maana atatajwa sana miaka sita na zaidi, Fanya hivi kumkomoa Magu barabara zake anazojenga usizipitie ndege alizonunua usipande vituo vya afya na hospital usiende pitia njia nyingine hata Dodoma alikohamishia serikali usiende kura yako moja usimpe Octoba lakini ataendelea kuwa Rais wako.

dodge
 
Huyo sultani akija amkumbushe habari ya ndugu zetu hasa dada zetu wanaoteseka!! Na wamenyanganywa pasporty !! Ubalozi umenyamaza kimya

Hawana wa kuwasemea ....ma ajent wapo dar wanakula kamisheni zao kila mwezi

Waziri wa mambo ya nje naye hakuna alichofanya atakapokuja zungumzeni tujue !! Hatma yao

sent from toyota Allex
 
Rais Magufuli amemualika Sultan mpya wa Oman kuitembelea Tanzania wakati wowote.

Salamu za Rais Magufuli zimetolewa na Waziri wa mambo ya nje Prof Kabudi aliyeko nchini Oman alikotumwa na Rais Magufuli kutoa salamu za pole kufuatia kifo cha Sultan wa nchi hiyo.

Source: Channel ten
Huyo si beberu? Asije hatarisha mapinduzi matukufu ya Zenji.
 
Ananyoosha kwanza nchi yake, ikishanyooka atakuja.
 
Mikedean naona unaweweseka kila akitajwa JPM na CCM ghafra unaona kiwewe inabidi uzoee tu maana atatajwa sana miaka sita na zaidi, Fanya hivi kumkomoa Magu barabara zake anazojenga usizipitie ndege alizonunua usipande vituo vya afya na hospital usiende pitia njia nyingine hata Dodoma alikohamishia serikali usiende kura yako moja usimpe Octoba lakini ataendelea kuwa Rais wako.
Hivyo vyote ulivosema sivitumii.Namshukuru Mungu aliyenipa afya hata hospitali siijui ikoje hata ndugu yangu hajawahi kuumwa tukampeleka huko.Barabara zote nnazotumia ni za Mabeberu World Bank.Ndege zake sijawapi panda na siji kupanda.Kiufupi mimi siwezi kuweweseka kwa chochote lakin ninyi maccm na Jiwe mkiona comment kama hizi zinawauma maana ni kweli tupu saiz mmebaki mnashikana uchawi tu ndani ya chama.Sisi tunaenjoy life ninyi pamoja na madaraka na power mliyonayo lakin mkiona unyoya tu mnaogooopa utafikiri mmeona jini makata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais Magufuli amemualika Sultan mpya wa Oman kuitembelea Tanzania wakati wowote.

Salamu za Rais Magufuli zimetolewa na Waziri wa mambo ya nje Prof Kabudi aliyeko nchini Oman alikotumwa na Rais Magufuli kutoa salamu za pole kufuatia kifo cha Sultan wa nchi hiyo.

Source: Channel ten
Katika uhusiano wa kimataifa, moja ya kanuni muhimu kabisa ni reciprocity.

Reciprocity maana yake ni uwiano, marejeshano, tit for tat.

Yani, unapopewa, ujue kutoa, unapotaka watu waje kukutembelea, na wewe ujue kutembelea wenzako.

Sasa Magufuli anavyoalika watu waje kumtembelea, yeye atatembelea wenzake lini?

Au anataka kutembelewa yeye tu, yeye hataki kutembelea wenzake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom