Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Jaji wa Mahakama Kuu wa Kanda ya Musoma, Zephrine Galeba alietuliwa kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufaa kutokana na kuandika Kiswahili katika moja ya hukumu alizowahi kuzitoa.
Leo Rais Magufuli anamuapisha rasmi Dodoma, kuwa nami kukujuza yanayojiri.
===
10:22 Asubuhi: Jaji Galeba anatia saini kwenye viapo vyake
Jaji Zephrine Galeba: Mheshimiwa Rais, leo ni siku kubwa sana kwangu na familia yangu. Ni jambo la kumshukuru Mungu sana kwa kutujaalia kutuumba sisi kama viumbe wa daraja la juu lakini pia kututunuku uhai.
Mheshimiwa pia kwa unyenyekevu mkubwa na wa kipekee sana, nakushukuru sana kwa dhati ya moyo wangu kwa kuniheshimisha kunipa nafasi ya juu katika mahakama. Mimi sina maneno ya kueleza namna ambavyo nimepokea hii nafasi labda niseme tu kwa ufupi kwamba, nakuahidi kutumikia wananchi wa nchi hii kwa kutenda haki vile ambavyo Mungu anataka tutende haki huku duniani.
MWIGULU NCHEMBA: SHERIA INASEMA LUGHA YA SHERIA NA MAHAKAMA IWE NI KIINGEREZA
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Sheria iliyoko sasa imeelekeza kuwa lugha ya sheria na lugha ya Mahakama iwe ni kiingereza.
Kwa kuwa sasa kiswahili kinabidi kutumika kwa kuwa wanaoandika ni watu wanaofahamu kiswahili na wanaoandikiwa ni waswahili basi wameongea na Mwanasheria Mkuu ili kuangalia namna ya kubadili vipengele hivyo.
Dkt. Nchemba amempongeza Rais Magufuli kwa hotuba yake kuhusu Sheria na Kiswahili aliyoitoa siku ya maadhimisho ya miaka 100 ya mahakama nchini Tanzania.
Ameyasema hayo katika hafla ya kumuapisha Jaji Zephrine Galeba ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa jijini Dodoma.
RAIS MAGUFULI: KISWAHILI KINA MSAMIATI WA KUTOSHA
Rais Magufuli amesema kuna baadhi ya watu huwa wanakosoa juhudi za Kiswahili kutumika wakidai kuwa kina uhaba wa msamiati
Amesema hoja hiyo haina mashiko kwa kuwa Kiswahili kina msamiati ya kutosha ndio maana kinatumika hata kwenye baadhi ya taasisi za kimataifa na vyomb vya habari vya kimataifa kama BBC na DW
Pia amesema Kiswahili ni lugha ya 10 kwa kuzungumzwa duniani, akisisitiza kuwa hata kama wakisema lugha haina msamiati wa kutosha, wataje lugha moja ambayo imejitosheleza kwa msamiati
Rais amesema kutumia Kiswahili katika hukumu yatakuwa ni mapinduzi makubwa
====
RAIS MAGUFULI: NIMEMTEUA JAJI GALEBA MAKUSUDI ILI AKAENDELEZE KISWAHILI
Rais Magufuli amesema aliamua kumtunuku Jaji Zepharine Galeba Ujaji wa Mahakama ya Rufaa kutokana na uthubutu na ujasiri aliouonesha kwa kutumia lugha ya Kiswahili katika kuandika hukumu
Amesema “Ninajua hata kwenye Mahakama Kuu alikuwa ‘very junior’ ni Kijana na inawezekana wale nguli wa Mahakama Kuu Majaji wanajiuliza kwanini Kijana huyu amechaguliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa”
Amefafanua “Nimemteua makusudi ili Kiswahili akakiendeleze kwa Majaji wa Mahakama ya Rufaa. Ili hiki kilichomsaidia kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa asikiachie huko kikawa tu kisingizio cha kupatia kazi, akawe chachu ya Kiswahili kuanza kutumika.”
Aidha, amesema tumeshindwa kutumia Kiswahili Mahakamani kwa kukosa utashi na ujasiri na pia ni ishara ya kuendelea kwa kasumba ya kuendelea kupenda vitu vya nje na kudharau vya kwetu