Rais Magufuli aongezewe Ulinzi

Rais Magufuli aongezewe Ulinzi

Kungekuwa na haja au umuhimu wa.kufanya hivyo kikwete ndio angefanya hayo huyo jamaa wala usikae ukafikiri anaweza fanya hivyo.hapendi umashuhuri.
 
Mi naona hata TISS aweke sura mpya kama Buhari vile,wale top wote wa JK hawamfai kwa sasa ulinzi wake pia uwe madhubuti kweli kweli maanake vita anayopigana ni kubwa na inaathiri watu wanaoishi peponi wakiwa duniani.Kadri piston za bulldozer zinavyochanganya ndivyo anavyozidi kudhalilisha awamu iliyopita.Anahitaji ulinzi.
 
Haya.....nimekusikia.......nitabadilisha...........
 
bado sielewi,nia yenu ni ipi?mnaanza kuwaza ya JF Kennedy saa hizi?hayawagi kirahisi namna hiyo,usalama wake ni wa kutosha na kama hujui kikao chake cha kwanza kama prezdaa ilikuwa ni TISS,aliwaeleza alichodhamiria kufanya sasa kama wakimgeuka hata Preta usijisumbue kubadilisha.
 
ni kweli Raisi anapaswa kuongezewa ulinzi haraka sana maana mzee wa msoga anachuki sana na yeye pili kuna vigogo ndani ya ccm hawajapenda hata kidogo maamzi anayoyatoa.
 
Unadhani hana ulinzi wa kutosha hadi uweke hayo mapendekezo?

Vita anayopigana ni kubwa ndio, ila hajakurupuka! Wapo watu wakumpa muongozo na njia za kupita! Ile ni taasisi sio maamuzi ya mtu mmoja!

Sijaona wala siwezi kutilia shaka ulinzi wa Rais.
 
asante carter
 
Namkumbuka Lowassa alisema hawamu ya nne kila mtu analamika,wananchi wanalalamika,wabunge wanalalamika,serikali inalalamika sasa nani atafanya maamuzi? Alisema tunahitaji kiongozi anayeweza kufanya maamuzi kwa speed hii ameanza vizuri.
 
chama kilichomteua kuwa mgombea wake kilimjua na kumfavamu, vyema kuliko hata sisi tulikuwa nje ya chama chake, ni ukweli usiopingika CCM inajijenga upya na kur urudisha hadhi yake kwa serikali na wananchi, suala la ulizi tumuache Allah tu
 
Mungu yupo na ulinzi upo pia
 
poor you hujui kua psu ni cocktail ya servicemen mbali mbali, hapo hata jwtz wapo kamanda tulia.
 
Kumpoteza rais Magufuli. Ni wazi kwamba kila anavyopanda juu kuwasaka wahalifu, ndipo maisha yake yanavyokuwa hatarini. Vigogo vya wahalifu wenye pesa nyingi watafanya kila kitu kumwondoa. Ingekuwa anahongeka wangependelea hivyo, lakini ni wazi hilo halipo kwa Thomas Sankara wa Tanzania.

Kwa hiyo: ni juu ya kila Mtanzania mwenye uchungu na nchi yake, na anayependa watoto wake waishi maisha bora zaidi kuliko yeye, kusaidia kwa namna yeyote katika kumlinda rais Magufuli. Usione kuwa wewe ni mdogo sana huwezi kutoa mchango wowote. Kila mtu ni muhimu. Ikiwa mbu alivyo mdogo anaweza kukukosesha usingizi, sembuse wewe jitu kubwa. Fikiria tu- ni mchango gani nitaweza kuutoa kuhakikisha usalama wa rais? After all, wahalifu wote tunaishi nao na twasikia wayasemayo.

Watanzania tusikubali yamfike JM yaliyomfika Sokoine.. Play your part! Watu kama Magufuli hotokea mara moja tu kila miaka 50! Uliza Misri (Nasser), Kongo Kinshasa (Lumumba), Kongo Brazzaville (Ngouabi), Burkina Fasso (Sankara).....

Baada ya Magufuli ni utumbo na jokers!!!!!
 
Ndugu zangu wana Jf Rais wetu kwa sasa ana maadui wengi sana kiasi kwamba kunatakiwa juhudi za ziada kuhakikisha kuwa anaendelea kuwahudumia wananchi wa Tanzania.

Katika hili kunahitajika kuimarisha BRIGEDI YA ULINZI WA RAIS ili kuhakikisha Rais wetu anaendelea kuwa salama. Mimi ni askari msitaafu niliyehudumu Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kikosi cha Jeshi Lugalo ingawa bado nahudumu Serikali hii katika sekta nyingine.

Ninapenda kutoa wito kwa Brigedi ya ulinzi wa Rais kuimarisha ulinzi wa Rais Magufuli ili kukabiliana na maadui wa Rais wanaoongezeka siku hadi siku. Nikiangalia walinzi wa Rais ninaowaona akiambatana nao naona kuna haja ya kuangalia vizuri kwani kwa maoni yangu ule ulinzi sio imara sana. Siwezi nikasema wasiwasi wangu uko wapi kwa sababu za kiusalama, lakini nina uhakika watu wa ulinzi na usalama watanielewa.

Kuna walinzi wa ''FEATURES'' fulani ningetegemea kuwaona katika ulinzi wa Rais ninaowaona akiwa nao lakini siwaoni. Vile vile ningependekeza ulinzi wa Rais uwe na Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wengi (waliovua makwanda) si kwasababu mimi nimetoka huko ila kiukweli hawa hawajaathiriwa sana na rushwa na hawawezi kurubuniwa/kushawishiwa kirahisi ukilinganisha na Polisi na Usalama wa Taifa ambao wengi wao wamejikita sana kwenye siasa.

Hata hivyo bado natoa wito kwa Mkuu wa Majeshi (CDF) GENERALI DAVIS MWAMNYANGE na makamanda wengine wa JWTZ kuwa Rais anahitaji ulinzi kwa nguvu zote.

Najua wengi mtaona hoja yangu haina mashiko lakini mimi kama mlinzi wa nchi hii ingawa nimestaafu lazima nitoa tahadhali zangu.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Rais wetu.

Amina.
 
Unapaswa ukajieleze maadui hao ni kina nani wakati kuna kauli kuwa Rais anapendwa sana na Watanzania? Acheni kutuchanganya!
 
Kwa nchi ambayo Shetani amejenga himaya yake, anapotokea mtu wa mungu hugeuka kuwa adui. Naunga mkono hoja.
 
Ndugu zangu wana Jf Rais wetu kwa sasa ana maadui wengi sana kiasi kwamba kunatakiwa juhudi za ziada kuhakikisha kuwa anaendelea kuwahudumia wananchi wa Tanzania.

Katika hili kunahitajika kuimarisha BRIGEDI YA ULINZI WA RAIS ili kuhakikisha Rais wetu anaendelea kuwa salama. Mimi ni askari msitaafu niliyehudumu Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kikosi cha Jeshi Lugalo ingawa bado nahudumu Serikali hii katika sekta nyingine.

Ninapenda kutoa wito kwa Brigedi ya ulinzi wa Rais kuimarisha ulinzi wa Rais Magufuli ili kukabiliana na maadui wa Rais wanaoongezeka siku hadi siku. Nikiangalia walinzi wa Rais ninaowaona akiambatana nao naona kuna haja ya kuangalia vizuri kwani kwa maoni yangu ule ulinzi sio imara sana. Siwezi nikasema wasiwasi wangu uko wapi kwa sababu za kiusalama, lakini nina uhakika watu wa ulinzi na usalama watanielewa.

Kuna walinzi wa ''FEATURES'' fulani ningetegemea kuwaona katika ulinzi wa Rais ninaowaona akiwa nao lakini siwaoni. Vile vile ningependekeza ulinzi wa Rais uwe na Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wengi (waliovua makwanda) si kwasababu mimi nimetoka huko ila kiukweli hawa hawajaathiriwa sana na rushwa na hawawezi kurubuniwa/kushawishiwa kirahisi ukilinganisha na Polisi na Usalama wa Taifa ambao wengi wao wamejikita sana kwenye siasa.

Hata hivyo bado natoa wito kwa Mkuu wa Majeshi (CDF) GENERALI DAVIS MWAMNYANGE na makamanda wengine wa JWTZ kuwa Rais anahitaji ulinzi kwa nguvu zote.

Najua wengi mtaona hoja yangu haina mashiko lakini mimi kama mlinzi wa nchi hii ingawa nimestaafu lazima nitoa tahadhali zangu.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Rais wetu.

Amina.

wwww,

Asante. Kwani kafanya nini kikubwa cha kumfanya atengeneze maadui au achukiwe?

Kuminya Demokrasia au kutotimiza ile ahadi yake ya kutoa vielelezo vya mshahara wake hadharani au ni sakata la kuegemea sheria inayochukiwa na wananchi inayomfanya asilipe kodi katika kipindi ambacho Taifa linahitaji kuondokana na mifumo ya kifisadi na pia kila mtu alipe kodi?

By the way,na wewe ili tukuchukulie serious na kama ungekua makini na muadilifu kiasi hicho usingeweka hiyo avatar

Hiyo Picha inayodhalilisha wanawake haioneshi uadilifu na umakini wako kama askari

Sana sana inatoa taswira ya nakisi ya uadilifu uliyo nayo na pia kuchafua taswira nzuri ya jeshi letu ulikopitia

Ibadilishe kwanza
 
Back
Top Bottom