Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unadhani hana ulinzi wa kutosha hadi uweke hayo mapendekezo?
Vita anayopigana ni kubwa ndio, ila hajakurupuka! Wapo watu wakumpa muongozo na njia za kupita! Ile ni taasisi sio maamuzi ya mtu mmoja!
Sijaona wala siwezi kutilia shaka ulinzi wa Rais.
chama kilichomteua kuwa mgombea wake kilimjua na kumfavamu, vyema kuliko hata sisi tulikuwa nje ya chama chake, ni ukweli usiopingika CCM inajijenga upya na kur urudisha hadhi yake kwa serikali na wananchi, suala la ulizi tumuache Allah tu
Ulinzi anao wakutosha achaafanyekazi hapa Nazi tuu
Ndugu zangu wana Jf Rais wetu kwa sasa ana maadui wengi sana kiasi kwamba kunatakiwa juhudi za ziada kuhakikisha kuwa anaendelea kuwahudumia wananchi wa Tanzania.
Katika hili kunahitajika kuimarisha BRIGEDI YA ULINZI WA RAIS ili kuhakikisha Rais wetu anaendelea kuwa salama. Mimi ni askari msitaafu niliyehudumu Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kikosi cha Jeshi Lugalo ingawa bado nahudumu Serikali hii katika sekta nyingine.
Ninapenda kutoa wito kwa Brigedi ya ulinzi wa Rais kuimarisha ulinzi wa Rais Magufuli ili kukabiliana na maadui wa Rais wanaoongezeka siku hadi siku. Nikiangalia walinzi wa Rais ninaowaona akiambatana nao naona kuna haja ya kuangalia vizuri kwani kwa maoni yangu ule ulinzi sio imara sana. Siwezi nikasema wasiwasi wangu uko wapi kwa sababu za kiusalama, lakini nina uhakika watu wa ulinzi na usalama watanielewa.
Kuna walinzi wa ''FEATURES'' fulani ningetegemea kuwaona katika ulinzi wa Rais ninaowaona akiwa nao lakini siwaoni. Vile vile ningependekeza ulinzi wa Rais uwe na Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wengi (waliovua makwanda) si kwasababu mimi nimetoka huko ila kiukweli hawa hawajaathiriwa sana na rushwa na hawawezi kurubuniwa/kushawishiwa kirahisi ukilinganisha na Polisi na Usalama wa Taifa ambao wengi wao wamejikita sana kwenye siasa.
Hata hivyo bado natoa wito kwa Mkuu wa Majeshi (CDF) GENERALI DAVIS MWAMNYANGE na makamanda wengine wa JWTZ kuwa Rais anahitaji ulinzi kwa nguvu zote.
Najua wengi mtaona hoja yangu haina mashiko lakini mimi kama mlinzi wa nchi hii ingawa nimestaafu lazima nitoa tahadhali zangu.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Rais wetu.
Amina.