Rais Magufuli aongezewe Ulinzi

Rais Magufuli aongezewe Ulinzi

Ndugu zangu wana Jf Rais wetu kwa sasa ana maadui wengi sana kiasi kwamba kunatakiwa juhudi za ziada kuhakikisha kuwa anaendelea kuwahudumia wananchi wa Tanzania.

Katika hili kunahitajika kuimarisha BRIGEDI YA ULINZI WA RAIS ili kuhakikisha Rais wetu anaendelea kuwa salama. Mimi ni askari msitaafu niliyehudumu Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kikosi cha Jeshi Lugalo ingawa bado nahudumu Serikali hii katika sekta nyingine.

Ninapenda kutoa wito kwa Brigedi ya ulinzi wa Rais kuimarisha ulinzi wa Rais Magufuli ili kukabiliana na maadui wa Rais wanaoongezeka siku hadi siku. Nikiangalia walinzi wa Rais ninaowaona akiambatana nao naona kuna haja ya kuangalia vizuri kwani kwa maoni yangu ule ulinzi sio imara sana. Siwezi nikasema wasiwasi wangu uko wapi kwa sababu za kiusalama, lakini nina uhakika watu wa ulinzi na usalama watanielewa.

Kuna walinzi wa ''FEATURES'' fulani ningetegemea kuwaona katika ulinzi wa Rais ninaowaona akiwa nao lakini siwaoni. Vile vile ningependekeza ulinzi wa Rais uwe na Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wengi (waliovua makwanda) si kwasababu mimi nimetoka huko ila kiukweli hawa hawajaathiriwa sana na rushwa na hawawezi kurubuniwa/kushawishiwa kirahisi ukilinganisha na Polisi na Usalama wa Taifa ambao wengi wao wamejikita sana kwenye siasa.

Hata hivyo bado natoa wito kwa Mkuu wa Majeshi (CDF) GENERALI DAVIS MWAMNYANGE na makamanda wengine wa JWTZ kuwa Rais anahitaji ulinzi kwa nguvu zote.

Najua wengi mtaona hoja yangu haina mashiko lakini mimi kama mlinzi wa nchi hii ingawa nimestaafu lazima nitoa tahadhali zangu.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Rais wetu.

Amina.
eh mawazo chanya ila umetoka huko na humfahamu CDF wa sasa
 
Maana mafisadi wamevuta midomo, amevuruga mifumo yao ya ujambazi, amefumua njia zao zote za giza walizokuwa wanatumia kutusua, wana roho mbaya kama wasaga sumu.

Pia nawaomba watu wa system wamtazame JPM kwa jicho la tatu. Wamlinde kama mboni ya jicho aendelee kutumbua damu itembee vizuri mwilini.
 
Maana mafisadi wamevuta midomo, amevuruga mifumo yao ya ujambazi, amefumua njia zao zote za giza walizokuwa wanatumia kutusua. wana roho mbaya kama wasaga sumu. Nimesikia wanataka kukodi majambazi yanayovaa suti kutoka ulaya waje wamuue. Sasa kwa nguvu na uwezo wa Mungu watakufa wao kabla hata hawajamkaribia kamanda mtumbua majipu. Pia nawaomba watu wa system wamtazame JPM kwa jicho la tatu. Wamlinde kama mboni ya jicho aendelee kutumbua damu itembee vizuri mwilini.
umesikia wapi?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
If you are just so much afraid and uncertain kwa nini msimshauri afanye movements zake akiwa ikulu tu? Mpk mtu a rule ukuta atakuwa kefhaonekana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anajitisha mwenyewe ulinzi ameongezewa ila hakuna anaemuwinda!! Vita vya uchumi ni akili na kuminya supply tu atanyooka!! Wawekezaji wana slow down wafanya biashara the same....walipa kodi wakubwa wanapunguza mzunguko na investment......kodi kidogo maana hawana imani ten kuweka pesa mingi.....vita y uchumi ni ngumu sana!! From 1.2T to 700b sio mchezo....atakopa hadi kwa Nkurunzinza akija ziara hapa!!!
 
Na ulinzi wa mungu pia, ulinzi wa dola peke yake hautoshi.Tuzidi kumuombea
 
Rais Magufuli ni mwema kwa vyovyote vile.
Kajitoa kafara, kafala yake Lazima iwe ghari. Anapigania Watanzania majority.

Vita ya kiuchumi ni ngumu Sana, inahitaji Watanzania wachache model ya prisident Magufuli.

Kuna viongozi Wengi mashuhuri duniani kwa Sasa wanakuja kama wenyeji kusapoti juhudu za muheshimiwa Magufuli.
Nahisi Wengi wa hawa viongozi mashuhuri duniani ni maajenti wa mashirika ya kijasusi duniani.

Nafasi walizonazo ni Lazima uwe mshirika wao, Inawezekana wakatumika na haya mashirka kama majasusi.
Watakuja na biology weapons, kwa kushikana na rais mikono huku wakimuangamiza slowly.
Jipangeni kwa Kila hali, hawa watu hawafai wanaposaka njuru.

Nashauri mboreshe kinga before cure madhubiti Kwa Rais Magufuli.

Tunamuhitaji Sana Wengi wetu atuvushe kwenye kadhia hii ya muda mrefu.
Magufuli ni nguzo na icon ya kilio cha Wengi Watanzania.
Kuumia kwake ki hasara hamtaruka lawama za Watanzania, kwa Imani walionayo kwake.

Nawakilisha!

tatizo ninyi wote mnaongea hayo ni washamba, hamjui hata mnachokifanya, mnajifunza kufanya vitu, ni kama mpo maabara hamuamini mnachofanya hadi mkifanyie majaribio. wenye uwezo wametulia tu na hawajapata nafasi. ni kama kumtoa samaki aishi nje ya maji, au kumpeleka msukuma au masai akaogelee baharini. mmeharibu hii nchi, mmefanya watu wanaichukia nchi yao, mmefanya kama ni mali yenu vile. hamna maana wala faida yeyote kwa watz.
 
kwa 'gharama yoyote ile' hili neno unajua uzito wake au kwa kuwa lina 'typika' tu nawe uka type?
 
kwa 'gharama yoyote ile' hili neno unajua uzito wake au kwa kuwa lina 'typika' tu nawe uka type?
Ni vizuri watu wakajenga mazingira ya kujifunza kushauri yale yaliyo ndani ya uwezo wao tu!
 
Rais Magufuli ni mwema kwa vyovyote vile. Kajitoa kafara, kafala yake Lazima iwe ghari. Anapigania Watanzania majority.
Duh, hii sasa hatari, lugha! Kumtetea dikteta uchwara lazima kwanza na wewe ujitoe akili. Bestfruits hebu soma tena ulichoandika halafu jiulize kama unajua kweli maana ya kujitoa kafara...je, kweli anayejitoa kafara anahitaji ulinzi! Kama unamlinda aliyejitoa kafara, lazima na wewe ujitoe kafara...sasa hapa nani anahitaji ulinzi kuliko mwingine?
 
Back
Top Bottom