Uchaguzi 2020 Rais Magufuli asema soko la Mabibo, maarufu kama Mahakama ya Ndizi kumilikiwa na wananchi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amesema soko la Mabibo, Maarufu kama Mahakama ya Ndizi litakuwa chini ya wananchi.

Ameyasema hayo alipokuwa katika mkutano wa kampeni, akiwa anawaomba kura wananchi wa Ubungo.

Ameyasema hayo baada ya mgombea Ubunge wa Ubungo kupitia CCM, Kitila Mkumbo kusema kuwa, soko lile lilikuwa na changamoto kwa kuwa halikuwa rasmi kutokana na eneo hilo kuwa chini ya kiwanda cha Urafiki hivyo kushindwa kufanya uwekezaji.
 
Kwanini soko hilo linaonekana leo linatakiwa kumilikiwa na wananchi? Awali lilikuwa linamilikiwa na Nani? Kodi zilikuwa zinatozwa na kukusanywa na Nani? Hao wananchi wataunda kikundi Cha umiliki, wataunda kamati, wataunda seriakali au watamiliki kwa njia zipi?
 
Dah sijui hata nani atajibu hili swali ila naenda kutafuta kitambulisho cha 20k nizame pale nikauze.
 
Tuliambiwa na aliye kuwa mkuu wa mkoa kuwa tutajengewa soko letu la kisasa ktk eneo la kulivya bwawani. Sasa hatujui maendeleo.
bora tujengewe eneo hilo na kuna eneo lenye nafasi kubwa.
 
Hii ni rushwa ya wazi kabisa lakini NEC watakaa kimya kama hawajaona wala kusikia. Hizi ni kampeni za uchaguzi.

Pili ni kwamba hapa wamepigwa changa la macho kwa sababu wamiliki wa hilo eneo wapo na je watamilikiwa kwa namna gani?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amesema soko la Mabibo, Maarufu kama Mahakama ya Ndizi litakuwa chini ya wananchi.

Ameyasema hayo alipokuwa katika mkutano wa kampeni, akiwa anawaomba kura wananchi wa Ubungo.

Ameyasema hayo baada ya mgombea Ubunge wa Ubungo kupitia CCM, Kitila Mkumbo kusema kuwa, soko lile lilikuwa na changamoto kwa kuwa halikuwa rasmi kutokana na eneo hilo kuwa chini ya kiwanda cha Urafiki hivyo kushindwa kufanya uwekezaji.
Hivi leo ndio ana omba kuwa rais au anaomba kuongezewa muda? Kwamba haya anayo zungumza leo hakuyaona miaka mitano iliyo pita au yametokea leo?

Yaani CCM na mgombea wao wana wafanya Watanzania wajinga sana. CCM kama CCM hamkutkiwa kutoa ahadi maana mmetawala miaka 60. Sasa mnatakiwa mtushawishi kwa mema mliyo tufanyia ili tuwakubali. Acheni wehu.
 
Kwanini soko hilo linaonekana leo linatakiwa kumilikiwa na wananchi? Awali lilikuwa linamilikiwa na Nani? Kodi zilikuwa zinatozwa na kukusanywa na Nani? Hao wananchi wataunda kikundi Cha umiliki, wataunda kamati, wataunda seriakali au watamiliki kwa njia zipi?
Muda mrefu soko hilo lilipaswa kujengwa ktk eneo la kiluvya bwawani, lkn nadhani kama kawaida ya baadhi ya watendaji wetu mpaka wasukumwee ndio wafanye kazi vinginevyo wana chapa usingizi.
 
Kitila aomba soko, Magufuli ampa hapohapo.
Rais John Magufuli amewapa wafanyabiashara wa Soko la Ndizi Mabibo umiliki wa soko baada ya kuombwa na mgombea ubunge wa Ubungo, Profesa Kitila Mkumbo, leo.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Barafu, Mburahati, Rais Magufuli alisema kuanzia sasa soko hilo ni mali ya wafanyabiashara na taratibu za kisheria zitafuatwa kufanikisha hilo.

Awali, Rais Magufuli aliuliza ni kitu gani anaweza kukifanya kwa wafanyabiashara wa soko hilo.

Kitila alitumia fursa hiyo kumweleza Rais kwamba tatizo kubwa ni umiliki tu kwa sababu eneo lilipo soko ni mali ya Kiwanda cha Urafiki na hakuna uwekezaji wowote unaoweza kufanywa kuliboresha.

"Kuanzia sasa soko hili litakuwa mali ya wafanyabiashara wa soko hilo na watatakiwa kulipia shilingi 20,000 za kitambulisho tu. Taratibu za kisheria zitafuatwa, alisema Rais huku akishangiliwa na umati wa watu waliohudhuria mkutano huo wa kampeni.
IMG-20201013-WA0018.jpg
 
IMG-20201013-WA0163.jpg
 
Kwanini soko hilo linaonekana leo linatakiwa kumilikiwa na wananchi? Awali lilikuwa linamilikiwa na Nani? Kodi zilikuwa zinatozwa na kukusanywa na Nani? Hao wananchi wataunda kikundi Cha umiliki, wataunda kamati, wataunda seriakali au watamiliki kwa njia zipi?
MaCCM yamechanganyikiwa. Utafikili yana mgombea Mpya.
 
Kasema Vitambulisho viendelee kulipiwa 20000 ambayo ni haramu

Hili la Vitambulisho linamrudisha Chatu
Lissu akandamize hapo kwenye hiki Kitambulisho cha wizi, halafu amrarue kwenye Fao la Kujitoa kwamba akiingia tu madarakani anaifuta hii sheria kandamizi halafu aahidi wananchi anarudisha Bunge live cc Salary Slip yani hapo tunamchana Meko msamba vibaya anarudi chato.
 
Back
Top Bottom