Uchaguzi 2020 Rais Magufuli asema soko la Mabibo, maarufu kama Mahakama ya Ndizi kumilikiwa na wananchi

Watu walio karibu na Lissu wamfikishie mawazo haya.

,CC: Molemo
 
Hii ni rushwa ya wazi kabisa lakini NEC watakaa kimya kama hawajaona wala kusikia. Hizi ni kampeni za uchaguzi.

Pili ni kwamba hapa wamepigwa changa la macho kwa sababu wamiliki wa hilo eneo wapo na je watamilikiwa kwa namna gani?
Je, kuongeza mishahara nk kwa Anti ni rushwa au.
 
tuliambiwa na aliye kuwa mkuu wa mkoa kuwa tutajengewa soko letu la kisasa ktk eneo la kulivya bwawani....sasa hatujui maendeleo.
bora tujengewe eneo hilo..na kuna eneo lenye nafasi kubwa
Kujenga soko jingine la kisasa haliondoi umuhimu wa soko la Mahakama ya ndizi.
Maadamu mwenye ardhi ametoa kibali basi ni heri.
 
Hakuna Kipindi ambacho huwa nakipenda kama cha wakati wa Kampeni kwani mnaweza hata kuambiwa 'Kunya' Getini Magogoni ni rukhsa tu 24/7.
 
Naweza kusema kwasababu ya aliyekuwa mbunge mpinzani hakutaka Maendeleo yafanyike,hakusimamia vyema majukumu yake na ndio maana tunatakiwa tuchague mafiga Matatu, Rais ,Wabunge na madiwani wa CCM,

Alafu pia Rais hawezi kujua shida za kila sehemu ndo maana pakawa na wawakilishi wa wananchi, kama mbunge hatasimamia na kuelezea shida za wananchi wake huwezi kumlaumu Rais.

Kwa kuangalia tu Rais anaupendo wa dhati kwa wananchi wake, amefika ubungo kapewa shida zilizopo na leo hii hii katatua wananchi sasa wamepata hako zao.
Ndugu usitake kupambana na wana CCM , ni jeshi kubwa
 
'Naweza kusema kwasababu ya aliyekuwa mbunge mpinzani hakutaka Maendeleo yafanyike'.

Kwa hio majimbo yaliyo chini ya wabunge wa CCM kama kule Kongwa kwa Ndungai kuna maendeleo sana sio?
 
Walikuwa wamelala? Wameamushwa na TL? Walikuwa wapinzani miaka mitano iliyopita? Watapata taabu sana!
 
Hii ni rushwa ya wazi kabisa lakini NEC watakaa kimya kama hawajaona wala kusikia. Hizi ni kampeni za uchaguzi.

Pili ni kwamba hapa wamepigwa changa la macho kwa sababu wamiliki wa hilo eneo wapo na je watamilikiwa kwa namna gani?
Ndugu zangu ni mgombea lakini bado ni rahisi, ana mamlaka ya kufanya chochote, haimaanishi kuwa kwenye kampeni basi shughuli za kiserikali zisimame,
Kwahvy fahamu kuwa hiyo siyo rushwa bali ametekeleza miongoni mwa majukumu yake kama raisi.
 
'Naweza kusema kwasababu ya aliyekuwa mbunge mpinzani hakutaka Maendeleo yafanyike'.

Kwa hio majimbo yaliyo chini ya wabunge wa CCM kama kule Kongwa kwa Ndungai kuna maendeleo sana sio?
We unaonaje, au unafikir tukizungumzia Maendeleo unaielewaje....
 
Jimbo likiwa la upinzani ndo rushwa zinapatikana kweli kweli, vikundi vya kinamama, vijana mikopo njenje na maendeleo juu, yaani kuhongwa nje nje Kama mwanamke mweupe akiwa anatongozwa, soko unapewa mwananchi ulimiliki Sasa kwanini nisiendelee kuchagua upinzani ili nile mema ya nchi?
 
Alikuwa wapi miaka hii 5? Aache kuhadaa wananchi kama alivyowadaa watumishi wa serikali mwaka 2015?
 
Sidhani Kama hilo soko litajengwa Urafiki.Nilisikia kulikuwa na kesi na Unafiki walirudishiwa eneo lao Watu wa soko waliamuliwa kutolewa.Eneo jipya la kujenga soko lipo Kata ya Kwembe na eneo lilishatengwa
 
Unaweza kudhani kuwa mtawala aliyemaliza muda wake siyo CCM kwamba sasa CCM wamechukuwa nchi ndiyo wanasafisha safisha uozo kumbe wapo wao kwa miaka 60 sasa. Ukiisha uchaguzi yanarudiwa yaleyale 🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…