Rais Magufuli asikitishwa na vurugu za mechi ya Simba na Yanga,Sasa zazuiwa kutumia Uwanja wa Taifa

Rais Magufuli asikitishwa na vurugu za mechi ya Simba na Yanga,Sasa zazuiwa kutumia Uwanja wa Taifa

Mageti ya kuingilia Uwanjani kabla ya Pambano yalivunjwa na Mashabiki wote na Mh. Rais kamuagiza Nape asitoe Cent moja mpaka ifidiwe gharama zote za Uharibifu.
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Alichonifurahisha nape kuwapiga simba na yanga kutumia uwanja huo naona kama anamsusia boss mshahara maana bila timu hizo tff haina mapato
 
Lakini kiukweli vile viti vingi vilikwisha haribika kabla ya mechi ya jana, vingi vilikuwa vimekati kwenye kona
 
Alichonifurahisha nape kuwapiga simba na yanga kutumia uwanja huo naona kama anamsusia boss mshahara maana bila timu hizo tff haina mapato
Iwe fundisho kwa TFF ikome michezo ya kupanga matokeo.

Naomba mwenye video clip ya magoli ya jana aitupie hapa.
 
SIMBA SPORTS CLUB
DAR ES SALAAM
2-10-2016

TAARIFA KWA UMMA

Kwa masikitiko makubwa klabu ya Simba imesikitishwa sana na vitendo vilivyofanywa na baadhi ya washabiki wetu,cha kuvunja sehemu ya viti vya Uwanja wa Taifa.kitendo kilichotokea jana kwenye mchezo wetu wa Ligi kuu dhidi ya Timu ya Yanga.

Tungependa kuomba radhi kwa kadhia hii na klabu imekubali kulipia gharama za uharibifu huu.
Klabu itazungumza na wamiliki wa Uwanja huu kuona inalipaje gharama hizo.
Ni mategemeo yeti kuona jambo hili halitajikoze tena.

Lakini mbali na hayo klabu kesho Jumatatu itawasilisha malalamiko rasmi juu ya uchezeshaji mbovu wa waamuzi wa mchezo wa jana,hususan Mwamuzi wa kati Martin Sanya.

Sisi tunaamini vitendo viovu vilivyofanywa na washabiki wetu vilisababishwa na uamuzi wa hovyo kupita kiasi uliosababishwa na waamuzi hao.

Haieleweki ni kigezo gani mwamuzi huyo alitumia kulikubali goli la 'mpira wa pete'la mshambuliaji wa Yanga Amisi Tambwe na kulikataa goli halali la mshambuliaji wetu Ibrahim Ajibu.

Pia tumeshangazwa na kitendo cha kumpa kadi nyekundu nahodha wetu Jonas Mkude.ilhali kama nahodha alimfata kwenda kumlalamikia kitendo chake cha kukubali goli la 'hovyo 'la Tambwe.
Sote tumeona Sanya alijikwaa wakati anarudi nyuma na kuanguka,kisha kuanguka na kutoa kadi nyekundu kwa Mkude.

Tunajua safari hii Tff na bodi ya Ligi zitatoa adhabu kali kwa waamuzi hawa ili iwe fundisho kwa maamuzi ya hovyo ya aina hii.

Pia klabu italalamika kitendo cha vyumba vyetu vya kubadilishia nguo(dressing room)kupuliziwa dawa zilizokuwa na nia ya kuwaathiri wachezaji wetu kabla ya mechi kuanza.

Tutaziomba mamlaka zifanye uchunguzi wa kina kubaini kitendo hiki kisicho cha kiungwana kinachosadikiwa kufanywa na wapinzani wetu.
Tunajua dhamira yao ni kuwafanya wachezaji wetu wachoke,lakini timu yetu ya Matabibu ilichukua hatua sahihi za kuwafanya wachezaji wetu waweze kumaliza dakika Tisini za mchezo kwa uwezo na weledi mkubwa.

Na mwisho klabu itoe malalamiko yake kwa Waziri wa mambo ya nchi,Mh Mwigulu Nchemba.

Waziri huyu bila shaka amesahau majukumu yake yake ya kazi na kugeuka kiongozi wa klabu ya Yanga.

Tunajua ni haki yake kuwa na mapenzi kwa klabu aliyoichagua lakini vitendo vyake anavyovifanya vinaacha maswali mengi kuliko majibu ukizingatia nafasi yake kama Waziri mwenye dhamana ya kuongoza Wizara nyeti.

Itakumbukwa majuzi waziri huyu alifanya ziara Mkoani Morogoro kuzungumza na vikosi anavyoviongoza.
Na inajulikana pia Refarii wa mchezo wa jana Martin Sanya ni mwajiriwa wa Jeshi la Magereza mkoani Morogoro

Sote tulishuhudia Jana Mwigulu alishangilia goli la hovyo la mwajiriwa wake Sanya.

Pia waziri huyu alitoa kauli tata kuwa angetamani siku moja klabu inayoshangilia wapinzani wa Yanga wakipigwa mabomu ya machozi na Askari wa jeshi la Polisi.
Kauli hii aliitoa wakati wa sherehe za kukabidhi zawadi kwa timu zilizoshinda msimu uliopita zilizoandaliwa na wadhamini wa ligi.kampuni ya Vodacom.

Tunajiuliza yale mabomu ya jana pale Uwanja wa Taifa ndio utekelezaji wa maagizo ya boss Mwigulu?

Lakini pia matumizi ya rasilimali za umma yakiwemo magari ya serikali ktk shughuli za mara kwa mara za klabu ya Yanga napo kunaacha maswali mengi mno.

Wanasimba wanauliza kila Waziri anayeshabikia Simba akiwepo Waziri Mkuu akifanya vitendo hivi kutakuwa na utawala gani serikalini?

Imani yetu viongozi wakuu wa nchi watamuonya mh Mwigulu,vingenevyo atatengeneza chuki baina ya washabiki wa Simba dhidi ya serikali yao.
Mwigulu atambue klabu ya Simba ina mamilioni ya washabiki kama ilivyo klabu yake anayoishabikia.

Hatutarajii kuona 'mahaba'yake yasio na staha yanachochea jambo ovu kwa wanasimba na serikali yao wanayoiamini na kuipenda sana.

IMETOLEWA NA
KLABU YA SIMBA

SIMBA NGUVU MOJA
 
inafurahisha huku simba wanamsema Mwigulu aache unazi wa Yanga , huku Yanga wanasema Nape aache unazi wa Simba.....

Ningekuwa Magu pesa yote ya Jana wasingepata na kuwafukuzia wakachezee huko mkwakwani na morogoro
 
Mageti ya kuingilia Uwanjani kabla ya Pambano yalivunjwa na Mashabiki wote na Mh. Rais kamuagiza Nape asitoe Cent moja mpaka ifidiwe gharama zote za Uharibifu.

Acheni kumhusisha Rais kwa kila jambo...kuna harufu ya uongo hapa...thibitisha kama Rais ameagiza isitoke hata senti mpaka gharama zifidiwe....waliofanya fujo ni Simba kwa maana ya baadhi ya wapenzi wa Simba...Ni wahuni wachache wa samba wakiungwa mkono na baadhi ya viongozi wachache wa Simba ambao wana hulka ya hooliganism na siyo uongozi...walichofanya baadhi ya mashabiki hao wa Simba ni kukosa ustaarabu na kitendo chao cha kuvunja viti ni cha kishenzi bila kumung'unya maneno....Huwezi kuharibu viti uwanjani eti kwa kuwa refa 'amewaonea' kwa maamuzi...Hata kama refa amekosea ikumbukwe kuwa yewye pia ni binadamu....kwa walioangalia mpira leo kati ya Arsenal na Burnley watagundua kuwa goli lile alilofunga Koscielny lilikuwa la utata likiaminika kuwa mpira umemgusa mkononi...lakini hatukuona wapenzi wa Burnley wakivunja viti...Wala hatukuona mchezaji wa Burnley akimsukuma refa na kumdondosha chini....Refa pia ni binadamu na anaweza kufanya makosa....miaka michache iliyopita mchezaji wa Simba madaraka Selemani aliu-control mpira kwa mkono na kufunga goli dhidi ya Yanga lakini Yanga hawakuvunja viti....Huko ulaya mabao ya mkono ni mengi kama lile la Ufaransa la Thiery Henry kwenye michuano ya awali ya kombe la dunia...Maradona pia aliwahi kufunga bao la mkono kati ya Argentina na England kwenye kombe la dunia lakini hatukuona viti vikivunjwa....Wanaopaswa kuadhibiwa hapa ni Simba na siyo Yanga....Tuache siasa za mpira hapa Tanzania...Yanga haihusiki na uhuni wa jana...kuvunjwa kwa mageti ni kosa la uongozi wa uwanja kutokana na utaratibu mbovu wa kuingia uwa jani na siyo vinginevyo....
 
Mwandishi unanitisha inamaana hujui kuwa nape ni yanga pure hata hapo anashindwa kushukuru kocha kufanya alichotumwa ila chini ya kiwango
 
Nape unatakiwa kutoa maamuzi ya haki na sio ushabiki. Unapozuia mapato ya Yanga kwa sababu zipi!!! Unapo generalise kuwazuia Simba na Yanga kwa makosa ya mashabiki wa Simba sio tu unaonyesha ushabiki wako Simba bali chuki yako dhidi ya Yanga. Acha TFF watumie kanuni zao zilizopo. Kama NAPE ataendelea kuwaadhibu Wana Yanga kwa kosa la Wan Simba. Naomba viongozi wa Yanga watangaze kwa wana yanga nchi nzima kuwa NAPE NI ADUI NAMBA MOJA WA YANGA. Yeye NAPE asipotezee matatizo yaliyojitokeza kwa kushindwa kwa mitambo ya elektroniki kufanya kazi siku ya mechi.
Kwani hukuona fujo za jezi za njano kuharibu mageti??
 
leo simba wanalalamikia hujuma, akat wao na wenzao yanga n magwiji wa hujuma na kupanga matokeo toka zaman. kwel mkuki kwa nguluwe kwa binadam mchungu
 
Mbona serikali inahukumu kisela namna mechi ya simba na yanga haitaki jazba, mbona watu walishakula kitasa wakatulia mikia wao wakifungwa wanarusha ngumi.
Waliong'oa viti ni mashabiki wa simba sasa Yanga wanahusikaje.waache wabebe dhamana Nape anatengeneza mazingira sababu Yanga ndio anamechi away nyingi kuliko Simba.
 
Nape unatakiwa kutoa maamuzi ya haki na sio ushabiki. Unapozuia mapato ya Yanga kwa sababu zipi!!! Unapo generalise kuwazuia Simba na Yanga kwa makosa ya mashabiki wa Simba sio tu unaonyesha ushabiki wako Simba bali chuki yako dhidi ya Yanga. Acha TFF watumie kanuni zao zilizopo. Kama NAPE ataendelea kuwaadhibu Wana Yanga kwa kosa la Wan Simba. Naomba viongozi wa Yanga watangaze kwa wana yanga nchi nzima kuwa NAPE NI ADUI NAMBA MOJA WA YANGA. Yeye NAPE asipotezee matatizo yaliyojitokeza kwa kushindwa kwa mitambo ya elektroniki kufanya kazi siku ya mechi.
....................na sisi tutamtangaza Mwigulu kuwa adui yetu Namba 0 yaani ni hatari kuliko hatari yenyewe.
 
Lakini kiukweli vile viti vingi vilikwisha haribika kabla ya mechi ya jana, vingi vilikuwa vimekati kwenye kona
Nyiendiootunawatakaa afandee Nanii atusaidie uchunguzi huyu
 
Hii timu ikiwezekana ifutwe maana inaonekana kuwa sio raia wa Tanzana kwani sijawawi kuona upuuzi kama huu bongo. Mona wenzo hawavunja viti? ilitokea tena wakati TP MAZEMBE walipokuja wakanunua jezi zao wakaingia na kufanya fujo kama hizi !!!!!!!!!!!!!!!!!!!ifutwe tuu sasa maana hatuna jinsi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Umeonyesha hisia zako, ila hujaongea kisoka, timu kama timu haina tatizo ispokua mashabiki wake, na mashabiki sio wanaendesha timu.
 
Back
Top Bottom