Rais Magufuli atengua uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dkt. Ave Maria Semakafu

Ofcourse semakafu ni kada kindakindaki..yule ukikata mshipa damu inatoka ya kijani. Ila kwa huyu no.1 hiyo siyo kitu..akiona itamsaidia kisiasa..atakutoa kafara tu.
Yah! Alichofanya hapa ni kutafuta kura za walimu... in short, anawahadaa!!!
 
Hivi huyo ana kosa gani Kama ametekeleza kile ambacho wizara ilikwishaamua Sasa kateleza wapi? Waziri si yupo
 
Hahahaaaa ama kweli .JPM atoke kivigine.sisi siyo wajinga. Zamani Sana kipindi tuna Soma kidato Cha pili.katka SoMo la historia mwalimu alikuwa akileta test Kama swali lakuandika maelezo likiwa gumu .tulikuwa tuna weka swali lingine ambalo kwa wakati huo lilikuwa kwangu au kwetu na kulijibu vyema .eti tukidanganyana kuwa mwalimu anaweza akachanganya na ukaeeza kupata maks. Sasa utaratbu anao tumia JPM naufananisha na hayo .
 
Maamuzi mazito kama yale ni ngumu kuwa maamuzi bila Baraka toka juu, anawatumia wenzake kama mpira
Ila mimi binafsi niliposoma press release ya KM nikajua kinachofuata ni kutumbua
 
Aliahidi ajira 13.000 za walimu. Akajikuta uwezo wa kuwalipa na kampeni hizi ni mdogo. Aliamua kutoa kisingizio cha kutoajiri walimu wa vyeti baadae akaona itamharibia kisiasa ná uchaguzi huu.


uamuzi wa kutangaza kufutwa certificate ulitolewa mwaka 2014
 
Naibu Karibu mkuu alikuwa sawa ,hai walimu kwa Sasa ili kukuza na kuimarisha elimu panatakiwa mabadiliki makubwa kuendana na sayansi na teknologia Ila kwa sababu anategemea kura ambazo hatapewa kutoka kwa walimu ameamua kumtumbua.naye asubuhi tar 28 October atatumbuliwa . Tanzania wanafanya elimu ni siasa Ili kuzalisha vilaza mwishowe wawe wajumbe.
 
Nimekuelewa sana
 
Tengeneza tatizo, tatua tatizo, wajinga oyeeeeee. Naamini wazee wa chama wanajuta sana kuja na hili jina.
Mfumo wa chama chao ni wa hovyo Sana mwenyekiti ni mungu kamili akosolewi haojiwi awajibishwi ni fully dikteta
 
Ushabiki wa kitoto. Ukishaandika taarifa yenye au, au ujue unabahatisha. Ulizeni walioko wizarani badala ya kusema au. Wapo watendaji wengi ambao ni bigheaded na wanajiona ni wataalamu sana! Huyo Ave mwenyewe unamjua?
 
Awamu ya tano hakika ni ya uwajibikaji.
 
Mfumo wa chama chao ni wa hovyo Sana mwenyekiti ni mungu kamili akosolewi haojiwi awajibishwi ni fully dikteta
Mbona wote wako hivyo? Mbowe kuna anayebisha mbele yake? Zitto kuna anayebisha mbele yake, Unamkumbuka Cheyo na amri za OUT! Uliona akina Lipumba walivyofukuzana? Nani mbishi mbele ya Mbatia? Munachosha tu na comments za kizembe!
 
Katibu mkuu! Alisimamia PERMANENT HEAD DEMAGE(,PHD) ya MKUU WA "GINING" Nothing more nothing else🤣🤣🤣🤣🤣
 
Mbona wote wako hivyo? Mbowe kuna anayebisha mbele yake? Zitto kuna anayebisha mbele yake, Unamkumbuka Cheyo na amri za OUT! Uliona akina Lipumba walivyofukuzana? Nani mbishi mbele ya Mbatia? Munachosha tu na comments za kizembe!
Lakini si umeona mgombea wao ni chaguo la wanachama na sio la mwenyekiti, tofauti na kule walipoprint fomu moja tu ili kubeba visivyobebeka
 
Nafasi za uteuzi ni Bora kwenda kuchunga mbuzi. Yule Prof Adolf mkenda aliyekuwa karibu mkuu wizara ya maliasili na utalii aliona uteuzi ni kazi ya hovyo na elimu aliyonayo akaamua kukimbilia ubunge kule Rombo Kilimanjaro mungu ampe Kura nyingi.
 
Pamoja na kua ilani yao inataka mwalimu wa primary awe na diploma.. kufuta certificate ji upuuzi.

Kinacho takiwa ni kuboresha mafunzo , mfano badala ya miaka 2 ya mafunzo waende miaka 3 na mkazo uwe kwenye vitendo zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…