Rais Magufuli atengua uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dkt. Ave Maria Semakafu

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dkt. Ave Maria Semakafu

Kama yapi?! Ya kumfuta mtu kazi kwa sababu ya kutangaza sera ya serikali yake mwenyewe, au?! Hivi kwa akili yenu mnaamini kabisa Naibu Waziri anaweza kuchukua uamuzi mgumu kama huo pasipo na kuridhiwa na serikali?! Pasipo na kupitishwa na Baraza la Mawaziri?!
Mtu akishayanywa maji ya ukada anapoteza common sense yote.
 
Mimi nilishaona kwamba huyu mama yuko hatarini tangia sera ilivyotenguliwa kwa simu mchana huu na kwenye uzi mwingine nikamshauri Dkt. Semakafu ajiuzulu kuliko kusubiri kutumbuliwa.
Hujawahi anzisha uzi hapa JF wewe

Ahaa

Danganya watoto wako na ndugu zako

Hujawahi anzisha uzi wowote hapa JF
 
Hujawahi anzisha uzi hapa JF wewe

Ahaa

Danganya watoto wako na ndugu zako

Hujawahi anzisha uzi wowote hapa JF
Jifunze kusoma vizuri basi. Sikusema nimeanzisha uzi..nilichangia kwenye uzi mwingine..ule ambao ulikua unaongelea uamuzi wa JPM kutengua sera.
 
Mtu akishayanywa maji ya ukada anapoteza common sense yote.
Na wangekuwa wanatumia akili hapa ndo wangekuwa wanakumbuka yale tunayoambia kwamba endeleeni tu kutetea ujinga kwavile mnadhani haya ni ya wapinga CCM na serikali yake!!

Binafsi sijawahi kumfuatilia huyu mama lakini kwa maoni niliyosoma hapa, inaonekana ni Kada Kindakindaki wa CCM lakini bado katumbuliwa bila sababu!!

Sasa seuze hawa wapiga makofi ambao bado wanaishi nyumba za kupanga kuonesha wazi wapo far away from CCM Insiders!!
 
jambo la muhimu hapo ni kwamba TL kaongeza idadi ya kura ya mhanga huyu...kwenye uchaguzi hata kura moja ni muhimu sana!.
 
ndicho ninacho mpendea Rais Maguflli huwa hana simile anapoona uozo huwa hachelewi hakara anachukua hatua.
lkn ni kiongozi anaye penda kujiridhisha kabla hajachukua hatua dhidi ya mtu, kwa kifupi huwa hakurupuki wala hapendi kumuonea mtu.
viongozi mlio baki mwigeni
 
Na wangekuwa wanatumia akili hapa ndo wangekuwa wanakumbuka yale tunayoambia kwamba endeleeni tu kutetea ujinga kwavile mnadhani haya ni ya wapinga CCM na serikali yake!!

Binafsi sijawahi kumfuatilia huyu mama lakini kwa maoni niliyosoma hapa, inaonekana ni Kada Kindakindaki wa CCM lakini bado katumbuliwa bila sababu!!

Sasa seuze hawa wapiga makofi ambao bado wanaishi nyumba za kupanga kuonesha wazi wapo far away from CCM Insiders!!
Ofcourse semakafu ni kada kindakindaki..yule ukikata mshipa damu inatoka ya kijani. Ila kwa huyu no.1 hiyo siyo kitu..akiona itamsaidia kisiasa..atakutoa kafara tu.
 
Mzee ana hali mbaya sana, Haiwezekani huyo Mtu mmoja Wizara nzima ndo awe ana makosa...Waziri anabakije kwenye nafasi yake? Walimu msipumbazwe
 
Ofcourse semakafu ni kada kindakindaki..yule ukikata mshipa damu inatoka ya kijani. Ila kwa huyu no.1 hiyo siyo kitu..akiona itamsaidia kisiasa..atakutoa kafara tu.

Semakafu leo katumbuliwa ili kupata Kick naye binafsi anatambua na hana wasiwasi na hilo kwani soon atarudi ulingoni kama vile Mwigulu Nchemba alivyorudi
 
Mzee ana hali mbaya sana, Haiwezekani huyo Mtu mmoja Wizara nzima ndo awe ana makosa...Waziri anabakije kwenye nafasi yake? Walimu msipumbazwe
Tena nasema hivi... hili suala lipo tangu zamani! Jiwe anachofanya ni kuwapumbaza walimu!!! Suala la kufutwa certificate lipo tangu 2014!!
 
Nimesoma comments 96 nimeona comments mbili tu zilizokaa ki LUMUMBA KUMBA hii inaonesha hata hao BOOK SEVEN kina mambo yanawakera likilobaki wanalinda UBWABWA wao tuu
 
Duh....ndio maana huyu mzee kupata kura za watu wenye akili ni ngumu sana.
Mambo hayawezi kwenda hivi.
Huyu mama naamini hakuamka mwenyewe na kutoa tangazo hili.
Hivi tujiulize kwa ulimwengu huu bado tunahitaji walimu wa certificate?...
Tukisema haya wengine tunaonekana hatumpendi ila kumbe huu ndo ukweli wenyewe. Watanzania wenye akili timamu ni wengi sana na watanzania wasio na akili timamu ni wachache sana. Sioni mtanzania mwenye akili timamu atakayempa kura yake Magufuli hapo 28 oktoba. Sioni kwa kweli
 
Kama yapi?! Ya kumfuta mtu kazi kwa sababu ya kutangaza sera ya serikali yake mwenyewe, au?! Hivi kwa akili yenu mnaamini kabisa Naibu Waziri anaweza kuchukua uamuzi mgumu kama huo pasipo na kuridhiwa na serikali?! Pasipo na kupitishwa na Baraza la Mawaziri?!

But this sounds good kwa sababu kina-reflect kile kile ambacho mara kwa mara tumekuwa tukisema hapa endeleeni kushangilia udhalimu wa hii serikali kwa sababu mnadhani mkiwa ni wapiga makofi mtakuwa salama but none is safe!!!
Mijinga ya Lumumba hii inajitoa ufahamu. Achana nayo
 
Hii ni kampeni. Jamaa kaona drama za kula mahindi barabarani yanayo uzwa na mwenye bastola zime buma sasa wana watega walimu. Sidhani kama walimunmtakubali kuingia kwenye mtego wa panya.. Kumbukeni ahadi za kuongezewa mishahara alipo kuwa anaomba kura..
 
Kama alivyomtumia Lugola eti Lugola kasign mkataba eti yeye hajui. Wakati ule Kigwangala anagombana na mkenda wizara ya maliasili alijigamba kila taarifa analetewa na wanausalama lakini kwa Lugola eti hakujua. ANATUKERA
Mtu ana muda wa kufuatilia wateuliwa wake wanavyotongozana kwenye simu,ashindwe kujua haya?
Hizi ni kiki za kijinga!
 
Anaanzisha tatizo halafu anaitatua ili aonekane hodari.
Hatujasahau korosho tatizo kubwa alianzisha yeye, sukari, Kwenye afya alifanya hivi hivi kwa Ndugulile na sasa wizara ya elimu.
Nakuambia Magufuli akitoka madarakani kuna wana CCM watamzomea na kumtukana maana hana mamlaka tena.
 
Maamuzi mazito kama yale ni ngumu kuwa maamuzi bila Baraka toka juu, anawatumia wenzake kama mpira
Naomba kiwasilisha hoja....
JamiiForums-1554367852.jpg
 
Kabisa! Huyu mama katolewa kafara. Uamuzi wa kubadili sera usingeweza kufanyika bila ridhaa ya baraza la mawaziri ambapo Rais ni mwenyekiti, wizara inatekeleza tu.

Sasa hapa eti tunaaminishwa kwamba uamuzi huo ulifanya na NAIBU katibu mkuu? Wala sio katibu mkuu au naibu waziri au waziri? Hizi hadaa nyingine hapana..
Mkuu kila kitu kiko wazi. Kwanza kafanya hivyo ili kuwatisha Watendaji wengine wa Serikali kuwa bado ana nguvu na anaweza kufanya lolote dhidi yao. Hivyo basi wawe tayari kupokea maagizo toka juu hasa ktk kipindi hiki cha uchaguzi.

Hii ina maana gani kisiasa? Yaani ninyi Viongozi wa Waalimu hasa Wakuu wa shule za Msingi msipowahimiza Waalimu kunichagua mimi basi jueni hakutukuwa na mtu wa kuwateteeni hasa Waalimu wote wa "Ngazi ya Cheti". Kifupi ni kuwajaza Waalimu wa Shule za Msingi hofu.

Nani asiyejua alivyowahadaa Waandishi wa Habari 2015? Sasa hivi wanafanya kazi zao ktk mazingira gani??

Waalimu amkeni kataeni dhuluma mnazotendewa na wale mliowaamini 2015 kuwa watakuwa kimbilio lenu.
 
Back
Top Bottom