Rais Magufuli atengua uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dkt. Ave Maria Semakafu

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dkt. Ave Maria Semakafu

Kabisa! Huyu mama katolewa kafara. Uamuzi wa kubadili sera usingeweza kufanyika bila ridhaa ya baraza la mawaziri ambapo Rais ni mwenyekiti, wizara inatekeleza tu. Sasa hapa eti tunaaminishwa kwamba uamuzi huo ulifanya na NAIBU katibu mkuu? Wala sio katibu mkuu au naibu waziri au waziri? Hizi hadaa nyingine hapana..
Kama alivyomtumia Lugola eti Lugola kasign mkataba eti yeye hajui. Wakati ule Kigwangala anagombana na mkenda wizara ya maliasili alijigamba kila taarifa analetewa na wanausalama lakini kwa Lugola eti hakujua. ANATUKERA
 
Kama alivyomtumia Lugola eti lugola kasign mkataba eti yeye hajui. Wakati hule kkigwangwala anagombana na mkenda wizara ya maliasili alijigamba kila taarifa analetewa na wanausalama lakini kwa Lugola eti hakujua. ANATUKERA
Amechelewa mno!
 
Wananchi kuna mambo mnayasema humu kwa kujiamini lakini hayana ukweli wowote. Semakafu siyo daktari wa tiba ya binadamu. Alikuwa mwalimu wa somo linaitwa DS, mambo ya Gender. Muhimbili ina wafagiaji, wahasibu, wafamasia, manesi, watawala nk. Siyo kila mtu Mhumbili ni daktari.
Kile kimama ni kikada cha CCM chenye njaa kali. Kikiwa pale Muhimbili kilikuwa hakiwezi kutibu watu kutwa kiko busy kusuka majungu ya umbea ili wakubwa serikali wakipe cheo. Yaani kutumbuliwa kwake kuna watu pale wizara ya Elimu watashangilia.
 
Wanawake kuweni na akili. Alichofanya Magufuli hapa si tu kutengua uteuzi bali pia kumdhalilisha Semakafu kwa kumuita mpumbavu hadharani. Wanawake mna jambo na Magufuli 28/10/2020. Mmedhalilishwa mno
 
Kiki at the expense of an innocent person, scapegoat, pole SANA Dr Ave.
Ila werevu tunatambua walichokufanyia ni.katika kutafuta huruma ya walimu, wapiga kura.

Everyday is Saturday............................. 😎
 
Wanatuona mazuzu yaani anamwacha waziri na katibu anakuja kumtwanga red card naibu katibu?

Hii red card ina macho sana? Apige chini wizara nzima maana naibu katibu hawezi ibuka na jambo lenye masilahi mapana ya Taifa yeye peke yake.
Kabisa! Huyu mama katolewa kafara. Uamuzi wa kubadili sera usingeweza kufanyika bila ridhaa ya baraza la mawaziri ambapo Rais ni mwenyekiti, wizara inatekeleza tu.

Sasa hapa eti tunaaminishwa kwamba uamuzi huo ulifanya na NAIBU katibu mkuu? Wala sio katibu mkuu au naibu waziri au waziri? Hizi hadaa nyingine hapana..
 
Ujinga mtupu, kamtoa kafara katibu.
Waziri kaachwa kivipi wakati nae alishiriki na hata Rais mwenyewe atakua kajulishwa kabla ya kutoa tamko.
Isitoshe hilo halisaidii walimu kumpa kura.
Maamuzi mazito kama yale ni ngumu kuwa maamuzi bila Baraka toka juu, anawatumia wenzake kama mpira
 
Hilo baraza la mawaziri wanapata wapi taarifa/nyenzo/inputs za kujadili sera kwenye baraza hilo? (Nawaza juu ya huyo Naibu Katibu Mkuu na TOR zake)
Job Description ya Deputy PS nadhani kwa ujumla ni kuwa msaidizi mkuu wa katibu mkuu. Ofcourse baraza linapata inputs kutoka kwenye wizara husika maana wizara inapeleka policy changes kama mapendekezo. Ila hata kupeleka mapendekezo kwenye baraza la mawaziri ni lazma waziri aridhie maana yeye ndio anaenda kuwasilisha pendekezo kwenye baraza. Naibu Katibu mkuu hapo kaonewa tu plain and simple
 
Ndalichako ndio ilitakiwa atumbuliwe hapo.

Huyo bibi hakuamka kutoka usingizini na kutoa hilo tangazo.

Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
Labda kama utaratibu ulikiukwa na hawakupata ridhaa ya baraza la mawaziri kabla ya kutangaza mabadiliko ya sera (uwezekano wa hiyo ni mdogo sana). Lakini kama baraza liliridhia..hakuna aliyetakiwa kutumbuliwa.
 
Kwa nini hawakusoma alama za nyakati...!?
Shida ya wasomi wa Tanzania wajinga wengi Sana wamekariri hawajui kupambanua mda sahihi wa kufanya Jambo.Wanasiasa wametoa tangazo la ajira tena linawahusu Hawa wa cheti hapo hapo unakuja na hili tangazo automatically watu watajua hakuna kazi Ila ni usanii.

Tangazo hili kwa wanafunzi lingewakutia chuoni na walimu walioko kazini wangepata waraka tena baada ya uchaguzi hakuna mtu angetumbuliwa.

Hawa hawawajui wanasiasa huku wanajifanya wasomi hii mambo nawasikia na TRA wanapita na matangazo yao wakati mgombea mwingine anadai atapunguza utitiri wa kodi na ndio mshindani mkubwa lakini hawajui kujiongeza namna ya kufanya kazi zao kulingana na mazingira,wakitumbuliwa eti wameonewa.Hata Mimi ningekuwa mwanasiasa nakutumbua vizuri tuu
 
Back
Top Bottom