Rais Magufuli atoboa siri ya kuteua wanajeshi Serikalini

Rais Magufuli atoboa siri ya kuteua wanajeshi Serikalini

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,277
1480584077541.jpg


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amesema siri ya kuteua wanajeshi wengi Serikalini ni kutaka kuingiza Serikali kwenye nidhamu kutoka kwa wanajeshi hao

Magufuli alisema anataka kuichukua nidhamu iliyopo jeshini na kuingiza Serikalini kwa sababu alipoingia madarakani alikuta mambo mengi yako hovyo

Aliyasema hayo wakati wa chakula cha mchana na wanajeshi wapya wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) mwishoni mwa wiki alipo watunuku Kamisheni katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam, ambapo alisema imani yake kwa wanajeshi ndiyo inayomfanya awape kipaumbele

"Saa nyingine hata katika uteuzi wangu huwa najisahau kila nafasi inapotokea nateua mwanajeshi, lakini nafanya hivyo kwasababu nina imani kubwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa sababu ukiwapa jukumu wanafanya kwa ujasiri mkubwa na kwa moyo wote na kwa kuitanguliza Tanzania kwanza."alisema Rais Magufuli

Aidha, Rais Magufuli aliwataka wanajeshi kutembea kifua mbele wakijua yuko nao na anachotaka ni kuchukua nidhamu yao na kuingiza Serikalini.
 
Tutalielewa somo haina haja kunung'unika (Hapa kazi tu)hivi amuelewi?
 
hivi kwanini policcm hawateui?
Wanateua ila ni wachache nadhani wengi wao vetting inawatoa kutokana na matatizo mbali mbali pia viongozi wa polisi na magereza wamelalamikiwa kwa kutokupeleka majina ya watu wanaofaa wakati wa uteuzi ili wafanyiwe vetting.
 
atangaze hali ya hatari tu wapo watu weredi wengi tu sema hakuwa na option wakati anagombea hakuanda timu ya kumsaidia kazi ndomana anababaika tu,
 
Ni mwendo wa mchakamchaka, hii nzuri sana hongera Mh rais kwa kuwaamini wanajeshi. Kiukweli wanajeshi wananidhamu, utii na uwajibikaji
 
Ukiona mtu anaamini matumizi ya nguvu na amri ujue kuna mshkeri katika makuzi yake!

Ukiona mtu anashabikia uzembe, ufisadi, dhuluma ya viongozi na vitendo vya aina hiyo, ujue kuna mshkeri katika makuzi yake na kafikia kuwa mpumbavu na lofa
 
Back
Top Bottom