Rais Magufuli atoboa siri ya kuteua wanajeshi Serikalini

Rais Magufuli atoboa siri ya kuteua wanajeshi Serikalini

View attachment 441662.."Saa nyingine hata katika uteuzi wangu huwa najisahau kila nafasi inapotokea nateua mwanajeshi, lakini nafanya hivyo kwasababu nina imani kubwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa sababu ukiwapa jukumu wanafanya kwa ujasiri mkubwa na kwa moyo wote na kwa kuitanguliza Tanzania kwanza....''

Shida ipo siku ile ya siku..ya kutumbuliwa. Kama alipata taabu sana wakati anamtumbua Ombaneni Sifui, sijui itakuwaje siku ile ya kumtumbua Meya Jenerali Waitera.
 
Nidhamu ya JWTZ ni hali ya juu sijapata kuiona katoka majeshi.

Na Majeshi yote yanapaswa kupiga mfano huu wa JWTZ ktk kutekeleza majukumu yako na hayo malalamiko ya kila siku yatapungua.

Huwa nikiwakumbuka makamanda wapiganaji Gen Tumaini Kiwelu,Gen Waitara,Men Gen Waiden,Gen Sarakikya,Gen Kiaro,na wengine wengi tu nidhamu zao ktk utendaji ni ngumu kuzielezea.

Kunapokuwa na nidhamu ktk utumishi wowote ule matokeo ya uwajibikaji utayaona.

Hiyo IPO ktk Mashirika ya Umoja wa Mataifa UN nidhamu ni ya hali ya juu sana na matokeo ya kazi zao utaziona tu.

Nadhani ndiyo dhamira kubwa ya Rais ktk utumishi wa umma,Nidhamu Nidhamu

Na Nidhamu ni muhimu ktk kupata matokeo yoyote mazuri kwani utafuata taratibu zote.
 
Ukiona mtu anaamini matumizi ya nguvu na amri ujue kuna mshkeri katika makuzi yake!
Kuna mahali umeona amesema kutumia nguvu. yeye amesema nidhanu. Tatizo watzanaia, nidhamu kwao ni adhabu. Poor them!
 
Sio wote mzee juma wapo wengine hawafai kupewa nafasi serikalini,pitia wakuu wa majeshi waliopita utagundua kitu.
 
TRA na TPA tunahitaji Wanajeshi pia Nchi ya Viwanda sio lelemama
 
View attachment 441662Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amesema siri ya kuteua wanajeshi wengi Serikalini ni kutaka kuingiza Serikali kwenye nidhamu kutoka kwa wanajeshi hao

Magufuli alisema anataka kuichukua nidhamu iliyopo jeshini na kuingiza Serikalini kwa sababu alipoingia madarakani alikuta mambo mengi yako hovyo

Aliyasema hayo wakati wa chakula cha mchana na wanajeshi wapya wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) mwishoni mwa wiki alipo watunuku Kamisheni katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam, ambapo alisema imani yake kwa wanajeshi ndiyo inayomfanya awape kipaumbele

"Saa nyingine hata katika uteuzi wangu huwa najisahau kila nafasi inapotokea nateua mwanajeshi, lakini nafanya hivyo kwasababu nina imani kubwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa sababu ukiwapa jukumu wanafanya kwa ujasiri mkubwa na kwa moyo wote na kwa kuitanguliza Tanzania kwanza."alisema Rais Magufuli

Aidha, Rais Magufuli aliwataka wanajeshi kutembea kifua mbele wakijua yuko nao na anachotaka ni kuchukua nidhamu yao na kuingiza Serikalini.

Chanzo : Dar24

Nimemuelewa sasa, maana nidhamu ya jeshi ni kutii amri bila swali, hivyo na serikali yetu inatakiwa watumishi wake wote watii amri / maelekozo yote bila kuoji chochote na hapo nidhamu ya jeshi itakuwa imejengwa bara bara ndani ya seruikali yetu. Thank you very much for the best move ever in my country.
 
Taifa nidhamu ni jeshi tu? Akutukanaye hachagui tusi. Cry the beloved country.
 
Si dictator,anajiandaa akigoma kutoka madarakani hao hao wamsaidie,unapoona kiongozi anajikosha kwa jeshi ujue anataka msaada pale atakapobanwa.
 
Kikwete hakuwa mwanajeshi? Natania tu nisije shikwa, haka ka NCHI kagumu
 
Kwa hao hamna lolote kwakua enzi na enzi walikuwepo na hakuna jipya.

Kinana Mwenyewe si anatokea huko?
Kafanya lipi zaidi ya kupeleka nanii huko korea ?

Magufli anaweza kuwa zaidi ya Captain Thomas Sankara wa Burkinafaso mwana mapinduzi wa kweli aliye badili jina la Nchi hiyo toka Upper Volta Hadi Burkinafaso, alipiga marufuku vigogo wasiendeshe magari ya kifahari, aliwapiga vita wakwepa kodi, wala rushwa alipambana nao hadi pale alipouliwa kwa mapinduzi 15th october 1987 , akiiga harakati za mwana mapinduzi wa Argentina Ernest Che Guevra , nae aliuliwa huko Bolvia mwaka 1965 , Magufuli anaweza kulikombo Taifa hili lilozorota uhujumu uchumi kila kona.
 
Magufuli alisema anataka kuichukua nidhamu iliyopo jeshini na kuingiza Serikalini kwa sababu alipoingia madarakani alikuta mambo mengi yako hovyo

Je, nidhamu ya jeshini inaletwa na kitu gani yaani factors gani zina-influence hiyo discipline ya army? Kwa tuliopitia JKT mwaka mzima tunajua kuwa jibu lake ni rahisi kuwa jeshini kuna polisi wake (military police), MPs hawa kazi yako ni kama ya polisi wa uraiani; mfano, usipo vaa vizuri beret basi una kesi na adhabu yaki haihitaji mahakama ni moja kwa moja kituoni=quarter guard na kupigwa drill kwa muda wa dakika 45 mfululizo ikiwemo kukwepa ndege, n.k. sergeant major na OC wanasweka wanajeshi kwenye rumande yao na kuamuru adhabu. Halafu kuna mahakama za kijeshi (court martial) katika ngazi ya kikosi, na watuhumiwa wakikutwa na makosa wanafungwa kwenye magereza ya raia lakini katika utaratibu wa army.

Kwa nini jeshini nidhamu hii inatakiwa? kwa sababu kazi yao kubwa ni vita hivyo kwenye kupambana na adui hakuna mjadala ni kupokea tu amri, na endapo kamanda anaisaliti nchi au jeshi basi wapiganaji wanamtwanga risasi na kuendelea kupambana au mpiganaji anaposhindwa kutii amri utwangwa risasi mara moja.

Aidha, Rais Magufuli aliwataka wanajeshi kutembea kifua mbele wakijua yuko nao na anachotaka ni kuchukua nidhamu yao na kuingiza Serikalini.

Kwa maelezo ya siri ya nidhamu ya jeshini na madhumuni yake, je itawezekana kwa wanajeshi kuipeleka nidhamu hiyo kwenye public adminisration yaani utumishi wa umma? Kama wakiipeleka basi tutashuhudia push ups, vichura maofisini. Je, hilo haliwezi kuwa kosa la kisheria kwa mujibu wa sheria za kazi kwa raia?
 
Habari za wakati huu wanabodi,
Raisi wa JMT Dr. John Pombe Magufuli ameeleza sababu za kufanya kazi mbalimbali na jeshi la wananchi, JWTZ pamoja na kufanya teuzi mbalimbali kwa wanajeshi.

Sina takwimu vizuri kwenye teuzi hizo kwasababu hakutoa mfano katika hotuba yake ya jana huko mkoani Ruvuma lakini alitoa mfano WA kazi zilizofanywa na jeshi ni pamoja na zoezi la ukusanyaji wa korosho, ujenzi wa ukuta Mirerani ambapo alieleza kuwa alitegemea kazi hiyo ingefanyika Kwa miezi sita lakini ilikamilika ndani ya miezi mitatu na hivyo kulipongeza jeshi hilo na kueleza sababu za kupenda kufanya nao kazi ni utendaji.

Nchi hii kuna wasomi wengi ila usomi wao ni wa vyeti kwenye utendaji ni sifuri jambo ambalo limeonekana hasa kwa Vijana walio wengi wana elimu ya kwenye vyeti ila siyo ya kupambana na mazingira. Yamkini unakuta mtu kasoma hadi ana Master's tena ya human resource ila hajui hata rank ya uongozi hivyo elimu yake kama inaishia kwenye vyeti akishahitimu.

Je sababu ya utendaji inatosha? Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mitaala haina shida, shida ni sisi kubadili mentality yetu ya kuwa kusoma ni kwa ajili ya vyeti
 
Back
Top Bottom