Consultant
JF-Expert Member
- Jun 15, 2008
- 11,653
- 21,307
View attachment 441662.."Saa nyingine hata katika uteuzi wangu huwa najisahau kila nafasi inapotokea nateua mwanajeshi, lakini nafanya hivyo kwasababu nina imani kubwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa sababu ukiwapa jukumu wanafanya kwa ujasiri mkubwa na kwa moyo wote na kwa kuitanguliza Tanzania kwanza....''
2025hivi uchaguzi ni lini jamani?
Hao watulie kwanza hadi msimu wa mavuno 2020hivi kwanini policcm hawateui?
Kuna mahali umeona amesema kutumia nguvu. yeye amesema nidhanu. Tatizo watzanaia, nidhamu kwao ni adhabu. Poor them!Ukiona mtu anaamini matumizi ya nguvu na amri ujue kuna mshkeri katika makuzi yake!
Ukimuona makonda kasimama ujue ni mungu kasimama..... amakweli kijana anajiamini.hivi makonda nae ni mwanajeshi ooh nimesahau kumbe yeye ni mungu.
View attachment 441662Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amesema siri ya kuteua wanajeshi wengi Serikalini ni kutaka kuingiza Serikali kwenye nidhamu kutoka kwa wanajeshi hao
Magufuli alisema anataka kuichukua nidhamu iliyopo jeshini na kuingiza Serikalini kwa sababu alipoingia madarakani alikuta mambo mengi yako hovyo
Aliyasema hayo wakati wa chakula cha mchana na wanajeshi wapya wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) mwishoni mwa wiki alipo watunuku Kamisheni katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam, ambapo alisema imani yake kwa wanajeshi ndiyo inayomfanya awape kipaumbele
"Saa nyingine hata katika uteuzi wangu huwa najisahau kila nafasi inapotokea nateua mwanajeshi, lakini nafanya hivyo kwasababu nina imani kubwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa sababu ukiwapa jukumu wanafanya kwa ujasiri mkubwa na kwa moyo wote na kwa kuitanguliza Tanzania kwanza."alisema Rais Magufuli
Aidha, Rais Magufuli aliwataka wanajeshi kutembea kifua mbele wakijua yuko nao na anachotaka ni kuchukua nidhamu yao na kuingiza Serikalini.
Chanzo : Dar24
Magufuli alisema anataka kuichukua nidhamu iliyopo jeshini na kuingiza Serikalini kwa sababu alipoingia madarakani alikuta mambo mengi yako hovyo
Aidha, Rais Magufuli aliwataka wanajeshi kutembea kifua mbele wakijua yuko nao na anachotaka ni kuchukua nidhamu yao na kuingiza Serikalini.