Rais Magufuli atoboa siri ya kuteua wanajeshi Serikalini

Kweli kabisa... Unakuta mtu ana vyeti, ila kazi sifuri kubwa...!! Sbb vyeti sio utendaji, watu wengi wanafikiria ukiwa na vyeti umeshamaliza kazi, kumbe ukiwa na vyeti ndio KAZI INAANZA.. and you have to prove ur competencies beyond any doubt to be recognized wherever you go...
HARD WORK BEATS TALENT

 
Hiyo nakubaliana nae kwasababu kuna watu Wengi humu Tanzania wana vyeti mpaka vya Master's lakini kiutendaji anazidiwa na mtu mwenye elimu ya mitaani!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
acha porojo, anaogopa wasimpindue. Hakuna mtoto hapa! Akiwavuruga wamemvuruga! hayo mengine ni mastory ya watoto wadogo wa ccm, huku pinzania jua janja yake yote
 
Nyinyi watu hamjamuelewa Raisi wetu mpendwa, anaona hawa jamaa wanakula salary bure tu wakati ambako hakuna vita au machafuko, hivyo basi anaona ni vyema awatumie ila lugha anayotumia ni ya akili nyingi tofauti na anavyokomaa na wafungwa
 
Asitake kuleta hadithi nyingi, anawatumia wanajeshi maana ndio nguvu yake halisi ya kimadaraka, kwanza hana uwezo wa ushawishi wa hoja zaidi ya maguvu.
 
Uteuzi wa bwana mkubwa hasa akiangazia kambi za jeshi, hutua kwa Brigedia Jenerali. Mbona anawapenda sana hawa watu? Kuna Maluteni jenerali, Makapteni, maluteni, major, major jenerali nk.

Kulikoni Mabrigedia jenerali?
 
Unataka kusema muheshimiwa ni muoga wa coup detat? Usizunguke! Hapana..ni mgawanyo tu wa madaraka..hakuna kingine!
 
Unataka kusema muheshimiwa ni muoga wa coup detat? Usizunguke! Hapana..ni mgawanyo tu wa madaraka..hakuna kingine!
Sijasema hivyo, Brigedia General ni wachache sana ukilinganisha na hawa wa chini. Ni kuomba tu amani iendelee kuwepo na hatutarajii chochote kibaya kutoka jeshi letu hata siku moja.
 
Sijasema hivyo, Brigedia General ni wachache sana ukilinganisha na hawa wa chini. Ni kuomba tu amani iendelee kuwepo na hatutarajii chochote kibaya kutoka jeshi letu hata siku moja.
Nimekuelewa kaka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…