Uchaguzi 2020 Rais Magufuli avitaka Vyombo vya Ulinzi kutotumia nguvu pasipostahili wakati wa Kampeni na Uchaguzi

Uchaguzi 2020 Rais Magufuli avitaka Vyombo vya Ulinzi kutotumia nguvu pasipostahili wakati wa Kampeni na Uchaguzi

Kabisa Mkuu kanyanyasa, kadhalilisha na kaumiza watu wengi sana kwa miaka mitano. Wengine wamepoteza ajira kama CAG Assad, wengine wamepotea akina Azory na Ben wengi wamekufa, kubambikiwa kesi etc, sasa anataka kujifanya MTAKATIFU!
Anatumia usahaulifu wa watu; na pia, nadhani maneno kwake hayana maana kubwa. Anayatamka tu yasikike bila ya kuwepo na dhamira ya kuyaishi maneno hayo.

Hofu ni kuwa, akishashinda safari hii, hali inaweza kuwa mbaya zaidi kuelekea 2025.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Ha ha h ha ha, CCM lazima watoke nduki wakiusoma uzi huu...ati kura wazi wazi kama hizi za kwao za maoni...uwiii.

Hakuna chama cha kisanii Africa kama CCM.
Kwa sababu kimewazidi kete.
 
Uko sawa kabisa Mkuu, awamu ya pili itakuwa ni balaa tupu na ndiyo sababu akataka sheria ya KUTOSHTAKIWA kwa “maovu yake” ambayo bila ya shaka YATAKITHIRI.
Na hizi ndizo ajenda wanazotakiwa wapinzani wazieleze vizuri kabisa kwa wananchi wazielewe vizuri kabisa.

Yaani safari hii wapinzani wana mambo mengi sana ya kuwaeleza wananchi. Hofu yangu ni kuwa hawatakuwa na mpangilio mzuri wa kuziwasilisha hizi kirahisi watu waelewe kabla ya kwenda kupiga kura.

Yeye atatangaza sana vitu anavyojenga, wapinzani wanatakiwa wazungumzie zaidi umhimu wa haki zao na ukiukwaji wa haki hizo.

Kumbukumbu za kutosha kama ushahidi zipo, kwa hiyo haiwezi kuwa kazi ngumu sana kuifanya.
 
Amewaumiza wengi asijivishe wema ili tuwasahau kina Ben Saanane na Azory
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kwa nini CHADEMA na ACT-Wazalendo wasitengeneze bango kubwa lenye wino wa dhahabu kuhusu maneno haya yaliyosemwa hapa na bango hilo liwe sehemu muhimu ya Kampeni zao hadi Oktoba?

Maneno kama haya anayazungumza kutoka moyoni Rais Magufuli?

Angetawala miaka hii mitano kwa kufuata uamini wake huu tungekuwa tofauti sana na jinsi tulivyo sasa.

Sasa ni wakati wa kuhakikisha kuwa maneno haya sio hadaa tu za kutafutia kura na kusahaulisha yaliyofanyika. Ni kazi ya vyama vya upinzani kunyanyua mabango yao kuwaonyesha wananchi ni jinsi gani maneno matupu yasivyokuwa na vitendo kila mara wanapofanyiwa vurugu na kunyimwa haki.

Kama ndani ya CCM wameweza kufanya uchambuzi wa kuwapata wagombea kwa haki, kwa nini 'Tume' ishindwe kufanya kazi hiyo kwa ufanisi zaidi nchi nzima wakati wa uchaguzi mkuu?
Nadhani kuna jambo linaendelea huko ndani kwao...
 
Nadhani kuna jambo linaendelea huko ndani kwao...
Nakumbuka pia aliyosema Benjamin Mkapa, 'sponsor' wa Magufuli kuhusu uhitaji wa kuwepo na 'Tume Huru ya Uchaguziwa. Hii inaweza kuwa 'connection' inaweza kuwa imeanzia hapo, kama haya maneno yake ni ya kweli?
 
Yawezekana yameanzia hapo au juu yake kidogo maana tetesi zasema "wale wakubwa zetu hawatutazami jicho jema!"
 
Lengo ni kuhadaa jumuiya ya kimataifa kwa kauli za aina, hii ila nyuma ya pazia yeye ndio anaweza kutoa maagizo tofauti kabisa.

Tutarajie matumizi makubwa ya dola katika huu uchaguzi na hizi ni kauli tu za kutaka kujiondoa kwenye lawama kuwa sikuwatuma.

Mnaotumwa/kuagizwa tumieni akili zenu.

Magu sio wa kumuamini kabisa.
 
Yawezekana yameanzia hapo au juu yake kidogo maana tetesi zasema "wale wakubwa zetu hawatutazami jicho jema!"
Lakini juu ya yote haya, ni watu kutopoteza umakini kwa kulainishwa na maneno matamu.
Wakati huu ni kukumbuka hatari zinazotukabili kama taifa endapo hali itaendelea kama ilivyoanza 2015 hadi leo hii.

Tupo kwenye hatari kubwa.
 
Tunapenda sana soga na maneno ya kuburudisha, majungu na fitna ndo maana UKWELI HATUUPENDI NA HALISI KWETU HAINA MAANA BALI FAKE!!
OGOPA NCHI AMBAYO MTU AKIFIKWA JANGA WATU WANASHANGILIA NA KUFANYA SHANGWE
 
Rais Dk John Magufuli amevitaka vyombo vya ulinzi kutotumia nguvu mahali ambapo hapastahili kutumia nguvu wakati wa kampeni na uchaguzi wa mwaka huu, huku akiamini kuwa kampeni zote zitafanyika kistaarabu kwa amani.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo hii leo wakati akizindua Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jijini Dodoma.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo hii leo wakati akizindua Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jijini Dodoma.

"Ndugu zangu wanasiasa wenzangu kama ambavyo imekuwa kawaida yetu, niwaombe uchaguzi huu uwe wa kipekee kwa kufanya kampeni zetu kwa upole, kumtanguliza Mungu, kwa kujua sisi ni Taifa la Tanzania na kwa kujenga umoja wa Taifa letu" amesema na kuongeza kuwa;

"Ninaamini vyama vyote vitafanya kampeni kistaarabu, basi tukawe wavumilivu na ni viombe vyombo vya dola visitumie nguvu pasipostahili, lakini hata nyinyi wanasiasa msiwachokoze wale walinda amani, msiwafanye watumie nguvu nawathibishie nitatoa ushirikiano kwa vyama vyote ili twende na maadili yetu kama tulivyofundishwa na Baba wa Taifa, Haya Mwl. Julius Kambarage Nyerere,”

sijawahi kumuamini huyu mtu
 
Unapofungua mdomo kusema lingine huku moyo wako na matendo yako yanafikiria na kutenda vingine. Inaitwa tabia ya ndumilakuwili
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kwasababu wewe Ni nafsi lawama
Mzee JK alipata kusema kwamba kikwao kuna msemo Zilongwa mbali, zitendwa mbali..!!"
Kumuamini CCM ni mambo mawili
1. Ama mpaka jambo liwe
2. Au awe Kafa...
Ili kuweka kumbukumbu sawa
1980 Baada ya vita vya Kagera Hayati Mwalimu alisimama uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma akatangaza miezi 18 ya shida wananchi wafunge mikanda... mpaka "anang'atuka" mikanda ilikuwa inataka kukata matumbo na nyonga za watu!!!
Akaja Mzee wa Ruksa tukaambiwa Zanzibar itakuwa kama Dubai mpaka leo hata bandari haijaonesha kiwango achilia mbali "usipowajibika ole wako" iliyomuibua mzee wa kiraracha!!
Nani amesahau Mzee wa Ukweli na Uwazi... kuhusu ubinafsishaji... uwekezaji...
JE Awamu ya nne hatukuambiwa MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA?
JE AWAMU HII HATUKUAMBIWA KILA KIJIJI KITAPATA MILIONI 50!!???
Maendeleo hayana vyama...
 
Back
Top Bottom