Uchaguzi 2020 Rais Magufuli avitaka Vyombo vya Ulinzi kutotumia nguvu pasipostahili wakati wa Kampeni na Uchaguzi

Kabisa Mkuu kanyanyasa, kadhalilisha na kaumiza watu wengi sana kwa miaka mitano. Wengine wamepoteza ajira kama CAG Assad, wengine wamepotea akina Azory na Ben wengi wamekufa, kubambikiwa kesi etc, sasa anataka kujifanya MTAKATIFU!
Anatumia usahaulifu wa watu; na pia, nadhani maneno kwake hayana maana kubwa. Anayatamka tu yasikike bila ya kuwepo na dhamira ya kuyaishi maneno hayo.

Hofu ni kuwa, akishashinda safari hii, hali inaweza kuwa mbaya zaidi kuelekea 2025.
 
Reactions: BAK
Ha ha h ha ha, CCM lazima watoke nduki wakiusoma uzi huu...ati kura wazi wazi kama hizi za kwao za maoni...uwiii.

Hakuna chama cha kisanii Africa kama CCM.
Kwa sababu kimewazidi kete.
 
Uko sawa kabisa Mkuu, awamu ya pili itakuwa ni balaa tupu na ndiyo sababu akataka sheria ya KUTOSHTAKIWA kwa “maovu yake” ambayo bila ya shaka YATAKITHIRI.
Na hizi ndizo ajenda wanazotakiwa wapinzani wazieleze vizuri kabisa kwa wananchi wazielewe vizuri kabisa.

Yaani safari hii wapinzani wana mambo mengi sana ya kuwaeleza wananchi. Hofu yangu ni kuwa hawatakuwa na mpangilio mzuri wa kuziwasilisha hizi kirahisi watu waelewe kabla ya kwenda kupiga kura.

Yeye atatangaza sana vitu anavyojenga, wapinzani wanatakiwa wazungumzie zaidi umhimu wa haki zao na ukiukwaji wa haki hizo.

Kumbukumbu za kutosha kama ushahidi zipo, kwa hiyo haiwezi kuwa kazi ngumu sana kuifanya.
 
Amewaumiza wengi asijivishe wema ili tuwasahau kina Ben Saanane na Azory
 
Reactions: BAK
Nadhani kuna jambo linaendelea huko ndani kwao...
 
Nadhani kuna jambo linaendelea huko ndani kwao...
Nakumbuka pia aliyosema Benjamin Mkapa, 'sponsor' wa Magufuli kuhusu uhitaji wa kuwepo na 'Tume Huru ya Uchaguziwa. Hii inaweza kuwa 'connection' inaweza kuwa imeanzia hapo, kama haya maneno yake ni ya kweli?
 
Nakumbuka pia aliyosema Benjamin Mkapa, 'sponsor' wa Magufuli kuhusu uhitaji wa kuwepo na 'Tume Huru ya Uchaguziwa. Hii inaweza kuwa 'connection' inaweza kuwa imeanzia hapo, kama haya maneno yake ni ya kweli?
Yawezekana yameanzia hapo au juu yake kidogo maana tetesi zasema "wale wakubwa zetu hawatutazami jicho jema!"
 
Lengo ni kuhadaa jumuiya ya kimataifa kwa kauli za aina, hii ila nyuma ya pazia yeye ndio anaweza kutoa maagizo tofauti kabisa.

Tutarajie matumizi makubwa ya dola katika huu uchaguzi na hizi ni kauli tu za kutaka kujiondoa kwenye lawama kuwa sikuwatuma.

Mnaotumwa/kuagizwa tumieni akili zenu.

Magu sio wa kumuamini kabisa.
 
Yawezekana yameanzia hapo au juu yake kidogo maana tetesi zasema "wale wakubwa zetu hawatutazami jicho jema!"
Lakini juu ya yote haya, ni watu kutopoteza umakini kwa kulainishwa na maneno matamu.
Wakati huu ni kukumbuka hatari zinazotukabili kama taifa endapo hali itaendelea kama ilivyoanza 2015 hadi leo hii.

Tupo kwenye hatari kubwa.
 
Lakini juu ya yote haya, ni watu kutopoteza umakini kwa kulainishwa na maneno matamu.
Wakati huu ni kukumbuka hatari zinazotukabili kama taifa endapo hali itaendelea kama ilivyoanza 2015 hadi leo hii.

Tupo kwenye hatari kubwa.
Tunapenda sana soga na maneno ya kuburudisha, majungu na fitna ndo maana UKWELI HATUUPENDI NA HALISI KWETU HAINA MAANA BALI FAKE!!
OGOPA NCHI AMBAYO MTU AKIFIKWA JANGA WATU WANASHANGILIA NA KUFANYA SHANGWE
 
sijawahi kumuamini huyu mtu
 
Unapofungua mdomo kusema lingine huku moyo wako na matendo yako yanafikiria na kutenda vingine. Inaitwa tabia ya ndumilakuwili
 
Reactions: BAK
Kwasababu wewe Ni nafsi lawama
Mzee JK alipata kusema kwamba kikwao kuna msemo Zilongwa mbali, zitendwa mbali..!!"
Kumuamini CCM ni mambo mawili
1. Ama mpaka jambo liwe
2. Au awe Kafa...
Ili kuweka kumbukumbu sawa
1980 Baada ya vita vya Kagera Hayati Mwalimu alisimama uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma akatangaza miezi 18 ya shida wananchi wafunge mikanda... mpaka "anang'atuka" mikanda ilikuwa inataka kukata matumbo na nyonga za watu!!!
Akaja Mzee wa Ruksa tukaambiwa Zanzibar itakuwa kama Dubai mpaka leo hata bandari haijaonesha kiwango achilia mbali "usipowajibika ole wako" iliyomuibua mzee wa kiraracha!!
Nani amesahau Mzee wa Ukweli na Uwazi... kuhusu ubinafsishaji... uwekezaji...
JE Awamu ya nne hatukuambiwa MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA?
JE AWAMU HII HATUKUAMBIWA KILA KIJIJI KITAPATA MILIONI 50!!???
Maendeleo hayana vyama...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…