Rais Magufuli awaambia Waandishi wa Habari wawe makini, hawako huru kihivyo...

Rais Magufuli awaambia Waandishi wa Habari wawe makini, hawako huru kihivyo...



​

Habari waungwana, leo Rais John Magufuli anaapisha watu kadhaa na miongoni ni teuzi iliyozua rapsha ya wizara ya habari, sanaa, utamaduni na michezo ambayo ilimuondoa Nape Nnauye kwenye nafasi yake huku timing ikileta mjadala. Nafasi hio inachukuliwa na aliyekuwa waziri wa katiba na sheria, Dkt Harisson Mwakyembe huku Palamaganda Kabudi akiiziba nafasi yake anapotoka.

Pia Leo anaapishwa katibu mkuu wa Ikulu ila kwa sasa wanaoapishwa ni mabalozi mbalimbali wanaowakisha nchi zao.
===========

Mawaziri Dkt Harisson Mwakyembe na Palamaganda Kabudi wameshaapa, wanaoapa kwa sasa ni mabalozi wanaonda kuwakilisha katika nchi mbalimbali.
======

Anaeongea kwa sasa ni Rais Magufuli na kuwapongeza wote walioteuliwa. Amewaambia wasitegemee mazuri sana kwa kazi huwa zina lawama hasa kwa Tanzania ambapo kuna grupu la watu wao siku zote ni kulalamika.

Amedai Mwakyembe mitandao ilisema asingekuja kuapishwa pia wapo walioposti kuwa Kinana angeongea leo ilhali yeye kamtuma India kwa matibabu.

Hahaha eti "kamtuma India kwa matibabu"
 
Leo shughuli za IKULU ziko FULL LIVE TBC & AZAM TWO!!!

Fwatilia
Siku hizi uapishwaji umekuwa ni tukio kubwa sana kuliko tulivyokuwa tukijua. At the same time umuhimu wa bunge umepunguzwa. Ndiyo maana tonaonyeshwa LIVE wanapoapishwa, Uzinduzi au kuweka jiwe la Msingi wakati bunge halipati hiyo coverage.
 
Wanaoapishwa ni mabalozi wa Tanzania wanaoiwakilisha Tz huko ughaibuni hao ndio huwa wanaapishwa na rais.
Balozi wa nje huwa wanawakilisha hati za utambulisho

Kumbe hata mabalozi wa nchi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao Tanzania wanaapishwa na rais Magufuli? Wanaapishwa au wanapeleka hati za utambulisho?Nimeshindwa kukuekewa au wewe umekosea kuripoti?
 
kila siku teuzi sijui atarekebisha uchumi lini.....rais gani ukitofautiana tu na mtu kimtazamo una msitepisha down unateua mwingine.
Hamna maendeleo pasipo mawazo tofautitofauti
Pasipo mawazo tofauti hakuna maendeleo na huo ndio ukweli. Nakupongeza kwa kuliona hilo!!
 
Leo katika hafla ya kuapisha mawaziri, Rais amesema alikuwa anasubiri kuona kama Mwakyembe atawasili au la, kama alivyosoma kwenye mitandao ya kijamii.
Mytake : kumbe mzee naye anashinda kwenye mitandao ya kijamii.
 
Nimecheck Clouds, ta tv zingine naona wako na vipindi vingine kabisaaa....itv ndio kwanza naona mwalimu wa chekechea anafundisha

Yaani walichotakiwa kufanya ni kuacha kumuonyesha JPM,maana anafikiria zile sinema tunazifurahia
 
Anaitaja taja mitandao. Anajua uwepo wake. Sijui kama anajua influence yake

Lakini bila shaka anaifuatilia ndo maana haishi kuitaja
 
Na huko ndo anakosema kuna watu wanamkwamisha shughuli zake hapo tu ndo nachoka zaidi ,tumuombee
 
Yani hii katuni imencheksha sana,namuona bashite mkubwa anavyowatwanga na nyundo hao wapinzani na media![emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Hahhahahahah nimeipenda hii Bashite Mkubwa
 
Yaani walichotakiwa kufanya ni kuacha kumuonyesha JPM,maana anafikiria zile sinema tunazifurahia
Sasa hio mkuu ilokua haifai manake TBC pekee ndio walikuwepo pale tuuu...saa zingine tunaona picha tuuu hamna sauti ya kaz kweel kwel
 
Kashasoma huku hataki kuzungumza Leo, ila Mwakyembe ameongea anatia huruma hana jinsi

Naona akitoka huko arudi kuwa Mwandishi wa Habari maana wenzie wameshamfuta huku
 
Back
Top Bottom