Rais Magufuli awachana Kilwa kwa kumchagua mpinzani Bwege. Awataka kutofanya makosa tena uchaguzi ujao

Rais Magufuli awachana Kilwa kwa kumchagua mpinzani Bwege. Awataka kutofanya makosa tena uchaguzi ujao

ILANI ya ccm inatekelezwa na wana CCM,,, ukimchagua mbunge wa chama cha Jahazi Asilia au Tadea basi atatekeleza ILANI ya chama chake
Mbona kuna majimbo wapo wabunge wa ccm lakini hali ni mbaya tu
 
Kwa maneno ya Rais Magufuli andai kama Bwege angekuwa CCM angemfukuza uwanachama ana uwezo wa kumuadabisha.Lakini kwa sasa hawezi walimalize wao wenyewe.
Tafsiri pitofu. Magu ana roho mbaya. Halafu ana jificha nyuma ya kivuli cha kumuomba Mungu. Wakati Mungu hadhihakiwi. Awaukize watumishi wa Mungu maana hata kwenye huu msiba wa Ben haja jifunza kitu
 
Upuuzi mtupu,jimbo la Bukoba mjini,limekuwa chini ya ccm kwa miaka mingi,lakini hakuna stendi ya mabasi,tangu IPO hovyo tangu 1995,
 
Katiba ya Tanzania inampa Rais mamlaka ya kumuagiza mbunge afanye kile atakacho Rais! Si mipango iliyoidhinishwa wala maamuzi ya Bunge. Hapo ndipo ujinga mkubwa ulipo.

Halafu wajinga kibao wa chama tawala hawaelewi kuwa ilani ya chama cha siasa iwe tawala au upinzani hutekelezwa kupitia mipango na maamuzi ya Bunge na si yote kama ilivyo automatically. Bali ni yale yaliyokubaliwa na Bunge tu. Hayo “maagizo ya Rais” ni mambo ya nchi za kikomunisti modeli ya North Korea. Hata China wamepiga hatua kubwa kuachana na ujinga wa aina hii.

Sijui lini tutaachana na hizi tabia za banana republic.
 
Tupambaneni upinzani tushike dola.
Tusisahau kuwa Jpm ni mwanachama wa ccm lazima avute kwake, hiyo wa si chuki
 
Wakuu, MAENDELEO HAYANA CHAMA

Rais Magufuli akiwa safarini kutoka Mtwara, ameombwa na mwanakijiji Jimbo la Kilwa kwamba hawana Stendi ya Magari hivyo anaomba wajengewe. Rais Magufuli amejibu kwamba siku nyingine waangalie wawakilishi wanaowachagua ili waweze kufanya vile yeye anavyowaagiza. Mbunge wa jimbo hili aliyemaliza muda wake ni Seleman Bungara aka Bwege Mzee wa ''Umesikia Wapi'' ambaye alikuwa anatokea chama cha wananchi CUF Habari

Rais amezidi kusema kwamba miradi kama hiyo ni ya wabunge na Madiwani ndiyo wanapaswa kuisimamia hivyo kuwataka wabaki na Bwege wao

Rais Magufuli amesema haya...

Nilikuja hapa nikasema nichagulieni watu nitakaokuwa nawaagiza wanafanya ninayoyataka mkasema hapana, Mkamchagua Bwege basi shauri yenu na bwege wenu mwambie awatengenezee stendi

Kazi ya Stendi ni ya madiwani, wabunge. Ukikosea kuchagua, nafuu ukosee kuoa au kuolewa. Ukikosea kuchagua ni tatizo kubwa.

Na hili ndugu zangu niwaombe, muwe waangalifu katika kuchagua. Mchague watu ambao watakuwa kwa ajili ya watu masikini.

Tunatuma hapa fedha za road fund, tunatuma fedha hapa za halmashauri, zimeshindwa kweli kujenga stendi?

Lakini kwa sababu mnanichagulia, wao wenyewe mastendi unategemea mimi mwenyewe nifanyeje? Huo ndiyo ukweli sitaki kuwaficha mlikosea kuchagua.

Sasa katika uchaguzi wa mwaka huu mjipange vizuri, mchague mtu ambaye mtakuwa mmempa stendi akikataa nitamfukuza hata kwenye chama. Lakini leo nitamfukuza huyo aliyeko kwenye chama sijui hata yuko kwenye chama gani, nitamchukulia hatua gani?

Chama cha ACT Wazalendo kimelaani vikali na kuwahamasisha wananchi kukemea vikali kauli hizi za kibaguzi. Wamedai kuwa kitendo cha kuhamasisha ubaguzi na kuingilia mamlaka ya wananchi katika kuchagua mtu wamtakaye kinakiuka misingi ya Katiba yetu.

Kauli ya rais ni kinyume na sheria na ni ya kibaguzi na ya kuua demokrasia. Kauli hii ilaaniwe kote nchini.
 
Sisi Mbunge wetu ni Bwege full stop!
 
Kuna hii clip inatrend mitandaoni rais Magufuli akiwananga wananchi Jimbo la Bwege kuwa walifanya Makosa kuchagua upinzani. Kama Ni kweli ametamka hayo Basi ameonyesha kuwabagua wananchi wake. Amethibitisha kuwa medani ya siasa huru hawezi na hataki. Anaamini kwenye siasa za mlengo moja usio na ushindani wa hoja.
Tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu hapaswi kuongea maneno hayo. Nani asiyejua kuwa mtwara, Lindi na kusini Kuna korosho na gesi inayochangia katika Pato la taifa. Iweje kupewa huduma rais aingilie watu kunyimwa kisa mbunge ametoka upinzani. Na vipi mwananchi apewe adhabu kwa kutumia haki yake ya kimsingi. Basi Kama rais anaona pale palipo na upinzani maendeleo yadipelekwe Ni Bora abadili katiba tuwe na chama kimoja tu Cha siasa.
Ni haki ya kila Mtanzania kulipa Kodi na kufaidi matunda ya Kodi yake. Niwatake watanzania kuwa makini na hotuba za viongozi wao kusoma kauli na matendo yao ili watumie turufu ya kura kuwaondoa ili wakae pembeni wajifunze. Umoja wetu na mshikamano wetu ndio silaha ya amani na utulivu.
 
Back
Top Bottom