Rais Magufuli awachana Kilwa kwa kumchagua mpinzani Bwege. Awataka kutofanya makosa tena uchaguzi ujao

Rais Magufuli awachana Kilwa kwa kumchagua mpinzani Bwege. Awataka kutofanya makosa tena uchaguzi ujao

Mungu ndo analipa Tu.


Tazama wakazi wa bukoba wanavyoteseka kisa walichagua upinzani
images%20(14).jpeg
mgomo%2B%255Bic.jpeg
 
Co hataki matuc huyo hapendi kuambiwa ukwel huku akitoa kashfa kibao kwa wapinzani wake
Hizi kauli ni chafu! Kauli chafu nionavyo mimi ni sawa sawa na matusi, naye alisha tamka hataki matusi. Basi ni vyema tubaki na chama kimoja au lipi jema?
 



Wakuu, MAENDELEO HAYANA CHAMA

Rais Magufuli akiwa safarini kutoka Mtwara, ameombwa na mwanakijiji Jimbo la Kilwa kwamba hawana Stendi ya Magari hivyo anaomba wajengewe. Rais Magufuli amejibu kwamba siku nyingine waangalie wawakilishi wanaowachagua ili waweze kufanya vile yeye anavyowaagiza. Mbunge wa jimbo hili aliyemaliza muda wake ni Seleman Bungara aka Bwege Mzee wa ''Umesikia Wapi'' ambaye alikuwa anatokea chama cha wananchi CUF Habari

Rais amezidi kusema kwamba miradi kama hiyo ni ya wabunge na Madiwani ndiyo wanapaswa kuisimamia hivyo kuwataka wabaki na Bwege wao


Rais Magufuli amesema haya...

Nilikuja hapa nikasema nichagulieni watu nitakaokuwa nawaagiza wanafanya ninayoyataka mkasema hapana, Mkamchagua Bwege basi shauri yenu na bwege wenu mwambie awatengenezee stendi

Kazi ya Stendi ni ya madiwani, wabunge. Ukikosea kuchagua, nafuu ukosee kuoa au kuolewa. Ukikosea kuchagua ni tatizo kubwa.


Na hili ndugu zangu niwaombe, muwe waangalifu katika kuchagua. Mchague watu ambao watakuwa kwa ajili ya watu masikini.

Tunatuma hapa fedha za road fund, tunatuma fedha hapa za halmashauri, zimeshindwa kweli kujenga stendi?

Lakini kwa sababu mnanichagulia, wao wenyewe mastendi unategemea mimi mwenyewe nifanyeje? Huo ndiyo ukweli sitaki kuwaficha mlikosea kuchagua.


Sasa katika uchaguzi wa mwaka huu mjipange vizuri, mchague mtu ambaye mtakuwa mmempa stendi akikataa nitamfukuza hata kwenye chama. Lakini leo nitamfukuza huyo aliyeko kwenye chama sijui hata yuko kwenye chama gani, nitamchukulia hatua gani?


Chama cha ACT Wazalendo kimelaani vikali na kuwahamasisha wananchi kukemea vikali kauli hizi za kibaguzi. Wamedai kuwa kitendo cha kuhamasisha ubaguzi na kuingilia mamlaka ya wananchi katika kuchagua mtu wamtakaye kinakiuka misingi ya Katiba yetu.

Wanakilwa msidanganywe kabisa
Bwege popote ulipo ukiiona video hii ijibu kwahoja, pakuanzia Anza na Jimbo la ndugai

Motomoto
 
Kwahiyo majimbo ambao wabunge wao ni ccm yanamaendeleo ? Mimi natokea jimbo la Ulanga magharibi ambapo kwa sasa ni Wilaya mpya ya Malinyi. Hili jimbo tangu lianze siasa za vyama vingi limetawaliwa na ccm kuanzia Mbunge Ngasongwa na hata Mponda ambaye amemaliza muda wake sasa hakuna kilichofanyika barabara kuanzia mwezi wa kumi na mbili mpaka mwezi sita huwa hazipitiki. Na hiyo hali ni ya muda mrefu yaani hata kabla ya mfumo wa vyama vingi
 
Jimbo la Kongwa, kuna mbunge sijui katokea chama gani yule. Na kama katoka ccm mbona hakuna la maana pale. Wananchi shida ya maji ni ya

Jimbo la Kongwa sijue walichagua wa chama gani maana shida ya maji haijawahi kutatuliwa na wananchi wana shida kweli kweli. Nadhani angetoka chama cha kijani angefukuzwa.
Miccm imejaaa na inazeeka na unafki wao
 
Katiba ya Tanzania inampa Rais mamlaka ya kumuagiza mbunge afanye kile atakacho Rais! Si mipango iliyoidhinishwa wala maamuzi ya Bunge. Hapo ndipo ujinga mkubwa ulipo.

Halafu wajinga kibao wa chama tawala hawaelewi kuwa ilani ya chama cha siasa iwe tawala au upinzani hutekelezwa kupitia mipango na maamuzi ya Bunge na si yote kama ilivyo automatically. Bali ni yale yaliyokubaliwa na Bunge tu. Hayo “maagizo ya Rais” ni mambo ya nchi za kikomunisti modeli ya North Korea. Hata China wamepiga hatua kubwa kuachana na ujinga wa aina hii.

Sijui lini tutaachana na hizi tabia za banana republic.
Zito aliwahi kusema washamba na malimbukeni wameshika hatamu za uongozi.

The worse is yet to come
 
Kuna hii clip inatrend mitandaoni rais Magufuli akiwananga wananchi Jimbo la Bwege kuwa walifanya Makosa kuchagua upinzani. Kama Ni kweli ametamka hayo Basi ameonyesha kuwabagua wananchi wake. Amethibitisha kuwa medani ya siasa huru hawezi na hataki. Anaamini kwenye siasa za mlengo moja usio na ushindani wa hoja.
Tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu hapaswi kuongea maneno hayo. Nani asiyejua kuwa mtwara, Lindi na kusini Kuna korosho na gesi inayochangia katika Pato la taifa. Iweje kupewa huduma rais aingilie watu kunyimwa kisa mbunge ametoka upinzani. Na vipi mwananchi apewe adhabu kwa kutumia haki yake ya kimsingi. Basi Kama rais anaona pale palipo na upinzani maendeleo yadipelekwe Ni Bora abadili katiba tuwe na chama kimoja tu Cha siasa.
Ni haki ya kila Mtanzania kulipa Kodi na kufaidi matunda ya Kodi yake. Niwatake watanzania kuwa makini na hotuba za viongozi wao kusoma kauli na matendo yao ili watumie turufu ya kura kuwaondoa ili wakae pembeni wajifunze. Umoja wetu na mshikamano wetu ndio silaha ya amani na utulivu.
Dawa ya mtu mbaguzi na mkabila ni kumpiga chini kwenye uchaguzi ujao.
 
Mtu akishakuwa mtu wa kubagua hata kikiwa chama kimoja ataanza kuangalia waliompa kura nyingi na chache.
Huyu jamaa msamiati 'Demokrasia' umemshinda kabisa.
Tatizo kubwa ni kukosa elimu, kujielewa na kukosa exposure.
 
Pesa za maendeleo ni pesa za walipa kodi si Hisani za CCM iweje CCM watake kuchaguliwa ndipo wapeleke maendeleo? huo ni wizi wa pesa za eneo husika hawawezi kulipa kodi kisha pesa zao zikatumike sehemu ingine kisa waliyemchagua siyo wa CCM hii ni dharau kubwa
Jamaaa anadhani watz wa leo bado hawajielewi,kama wale wa miaka hiyo, anatakiwa ajue kwamba pamoja na elimu mbovu inayotolewa, watu wameweza kupata uelewa wa kujua kipi sahihi na kipi sio sahihi.
 
Back
Top Bottom