Rais Magufuli, awashushua TAKUKURU na Watendaji wote wanajipendekeza kwake na kupeleka miradi ya Maendeleo Chato

Amka wewe. Kwa nini hakukataa pendekezo la kujengwa uwanja wa ndege Chatto wakati Geita uwanja upo?

Kwanini hakukataa kuitwa hifadhi Burigi Chato?

Kwanini hakukataa ujenzi wa TRA Chatto? CRDB Chato?

Huu ni mwaka wa uchaguzi bwashee watu watavaa ngozi zote za kondoo wakati ndani ni Chui.

Huyo Mkurugenzi wa Takukuru kafeli kwenye kushindwa kutengeneza kesi dhidi ya Chadema basi.

Hakuna lolote hapo
 
Ameona miradi imefurika Chato anazuga kukataa.

Miradi ya mabilioni imetekelezwa huko, halafu anakataa kaofisi ambako hakazidi hata milioni 100 danganya toto hiyo.
 
Uwanja wa ndege Geita upo sehemu gani?
 
It's obvious. Ofisi ya TAKUKURU, tena Chato!! Ulitarajia asemeje?
 
Hukuona bungeni walipitisha ujenzi wa uwanja wa ndege geita?? Au walikuwa wajinga wabunge???
Kwa nini hakukataa pendekezo la kujengwa uwanja wa ndege Chatto wakati Geita uwanja upo? (HAPA UMEMAANISHA TAYARI GEITA KUNA UWANJA WA NDEGE)
 
Watu hawajamsoma tu, ila jamaa ameshaimudu ile nafasi, tutarajie mengi ya kutushangaza, ukitaka kujua hilo angalia hata body language yake.
 
Brigedia jenerali aliposikia kwamba zile nyota zinaweza punguzwa aliweweseka masikini dah..Magu anamisifa sana
 
Dah kapate Bapa kwa bili yangu, unafiki wa kiwango cha lami
 
Ila Magu sometimes anazingua sana,jana kamchamba mbamba wa watu Major General Jonh Mbungo.. Hivi huyu mzee mbona hatabiliki? Last time alimsifu Dkt Mwinyi,kua anaongea vizuri na wanajeshi,ila yeye kampasua Major General tena mbele ya makamera! Mzee Magu kuna siku utavuka mipaka utamsema General Mabeyo!

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
Watu hawajamsoma tu, ila jamaa ameshaimudu ile nafasi, tutarajie mengi ya kutushangaza, ukitaka kujua hilo angalia hata body language yake.
Point mkuu, jamaa ameikamata Ile nafasi ipasavyo...Angalie Ile kauli "nisije nikajiuliza hizo nyota nilikupaje" ....Kujiamini kumepitiliza Sana.

Naona ameshapachika chawa wake kila sekta, ndio maana viongozi wa Taasisi wanakua na nidhamu ya woga Sana.
 
Sijui nani anaamini kuwa rais hapendi watu kujipendekeza tena anataka wamwabudu na usipofanya hivyo unapigwa chini. Huu ni unafiki mkubwa sana na anafanya haya kwani anajua anaongoza malimbukeni wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…