Sawa mkuu, lakini pia hii CCM ya Magufuli ilipitisha sheria mpya ya mtu mmoja kofia moja kwahiyo nafasi hiyo inakuwa wazi automatically
Navyofahamu nafasi ya uenezi taifa inakuwa wazi kwa misingi ya kazi ya idara ya uenezi ni ya kiutendaji pia ni kuwa msemaji wa chama. Na majukumu yake ni kazi ya muda wote. Yaani katibu wa NEC wa itikadi, siasa na uenezi anafanya kazi za kiutendaji muda wote.
Sio rahisi kuwa mbunge na katibu (mtendaji) mwandamizi wa chama kwa wakati mmoja.
Kuhusu nafasi mbili-mbili hili hakuna ukweli, as long as hufanyi kazi ya muda wote haina athari kuwa katika chama na kuwa mtumishi wa umma.
Mfano, Magufuli ni Mwenyekiti CCM taifa na ni Rais wa JMT. Uenyekiti sio kazi ya muda wote kama mtendaji (katibu).
Tabia Mwita wa Zanzibar ni makamu Mwenyekiti UVCCM taifa na pia ni mwakilishi na waziri kule Zanzibar. Kazi ya makamu Mwenyekiti sio ya muda wote.
Mwenyekiti UWT Dar-es-salaam pia ni Mbunge.
Mwenyekiti UWT Ilala pia ni Diwani.
Wapo wabunge wengi tu wana vyeo vya kisiasa. Wengine ni wajumbe wa halmashauri kuu na wengine ni wenyeviti wa jumuiya.
Mfano, Jerry Slaa, mbunge wa jimbo la Ukonga, Dsm ni mjumbe wa halmashauri kuu. Kazi ya MJ/H/KUU sio ya muda wote kama ya mtendaji (katibu). Hivyo haina athari ndio maana hajaiachia au kuachishwa.
Ukija kwenye watendaji (makatibu) wa CCM na jumuiya zake ndio huwa nafasi zao zinakoma mara baada ya kuwa wabunge au watumishi wa umma.
Pia kuna mfano wa aliyekuwa katibu wa UVCCM mkoa, anaitwa Asia Halamga. Nafikiri sasa ni Mbunge kundi la vijana. Nafasi yake ya ukatibu (utendaji ) imekoma.
Kwa mifano hiyo itoshe kusema inategemea na nafasi mtu aliyonayo kwenye chama ndio inaamua kama akipata uteuzi aachie.
Japo kuwa kuna nafasi za uteuzi ambazo unalazimika kuhama kimakazi hizi hata kama ulikuwa Mwenyekiti wa chama au jumuiya unaiacha nafasi hiyo mara moja japo sio ya muda wote.
Mfano mkuu wa mkoa wa Morogoro alikuwa Mwenyekiti wa CCM Arusha kama sijakosea. Baada ya uteuzi wake walifanya uchaguzi kiziba pengo hilo.