Rais Magufuli aweka Jiwe la Msingi Mahandaki Reli ya Kisasa

Rais Magufuli aweka Jiwe la Msingi Mahandaki Reli ya Kisasa

Mkuu ufipa hali zao ni mbaya sasa ivyo angalia na nyuzi za kuweka,utawaua na pressure

Kweli nyie ni misukule , huo ni wajibu wa serikali yoyote duniani kujenga miundo mbinu kwa kutumia kodi za wananchi .
Sasa hata baada ya miaka 50 ya uhuru bado unawaza kuzindua mahandaki ya reli.
 
Ni kweli kabisa. Yale matamshi hayakua ya kiungwana kabisa ni udhalilishaji. Na wale kenge wa kijani wakampgia makofi.
matamshi yale ni jadi ya Rais na ni sahihi kupitia taaluma yake ya ualimu Discipline kwanza na hajaanza leo na hatakiwi kuacha utamaduni huo mpya uliotukuka wa kuwachana hadharani anaowatumbua ili wanaoteuliwa kujaza nafasi wajipange! hiyo inaitwa Social Sanction yaani uchafu wa mtu inaambiwa jamii nzima ili wote mumjue nanyi mjipange nayeye mtumbuliwa akome kujitapa mbele ya jamii au kutunga uongo wa kujisafisha! Magu kataja walevi kina Kitwanga, Mabosi kina Gambo nk! yuko sahihi ni Mzungu pure!!

Mimi namuunga mikono na miguu kila anaemtumbua atutangazie uchafu sisi ndio tuliompigia kura anawajibika kwetu si kwa wateule wake!

nchi yetu ilibaki maskini kwa miaka sitini kwa kukosa Rais mwenye ujasiri kama yeye na kwa kukosa uwajibikaji wa viongozi na kwa tabia mbaya ya chama chetu kuficha mambo machafu ya viongozi wake na badala ya kuwatumbua wakawa wanahamishwa vituo!!
 
Kwa tawala zetu za Africa - Rais hakosei na hakosolewi...kauli ya Rais haina rufaa.
 
Ukweli kuaongea pia ni sanaa ni sayansi pia. Wengi tunaongea tu.

Inabidi tukubali wakubwa wakikosea kuongea tuseme alitania tu, amesema ukweli, hazungushizungushi nk.

Hii inatokea hata huku nchi zilizotangulia, hutokea Rais wa Marekani anaongea unaona jinsi raia wa Marekani wanavyomshangaa na kupiga kelele.
 
Wakuu huwa ninamshukuru sana Mungu kwa hatua aliyonifikisha kimaisha. Nashauri pambana uwe boss wewe mwenyewe katikaka biashara yako hata kama ni ndogo. Hata ukiwa umeajiriwa fanya kamradi kaziada ambacho wewe ni boss na ninakuhakikishia hutataka vyeo vya kupewa na kunyang'anywa kwa kuwa kwanza hutavipenda maana vitakufanya busy ushindwe kufuatilia deal zako. Wanasema cha kupewa si Chako ni kama cha kuazima hakisitiri ma ta ko.
 
Kaondoa madawa muhimu katika bima ya afya sasa wanatoa vipanadol tena kwa mashart makubwa. Hafai.
 
Rais Magufuli amemshukia vikali Mkurugenzi wa Kilosa baada ya wananchi kumlalamikia.

Rais Magufuli amesema Mkurugenzi ameuza ardhi ya kijiji kwa Tsh 220 milioni lakini taarifa zinazosikika zinadai alipokea Tsh 400 milioni, amemtaka DED huyo kujirekebisha.

Chanzo: TBC.

My take; Huyu DED ameiaibisha sana CCM

Maendeleo hayana vyama!
 
Ngoja tuone PCCB (PCCM?), nayo itachukua hatua gani. Otherwise Rais wetu ataonekana ni mtu wa kuokota maneno ya mtaani tu. Ati ajirekebishe....please!
 
Anatatua shida za Wananchi kijiji kwa kijiji

Pia ataweka jiwe la msingi ujenzi wa reli ya kisasa kutoka kilosa hadi makutupora
===
​

Rais Magufuli amekwishafika eneo la uwekaji wa jiwe la msingi ambapo amepewa maelezo ya kina juu ya Mahandaki hayo na namna ambavyo yatakavyofanya kazi.

Rais ameshiriki katika uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Mahandaki katika reli ya kisasa pamoja na kupiga picha ya pamoja kwa ajili ya kumbukumbu ya tukio hilo.

Rais ameshafika tayari kwa ajili ya kuongea na Wananchi kuhusu tukio la uwekaji wa jiwe la msingi la Mahandaki reli ya kisasa ambapo Wimbo wa Taifa na Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimeimbwa.

Viongozi wa Dini ya Kiisalamu na Kikristo wamekaribishwa ili kufungua tukio hili kwa dua ambapo kwa pamoja wamemshukuru Mungu pamoja na kumuombea mafanikio Rais Magufuli na taifa kwa ujumla.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro amepata nafasi ya kuwatambulisha viongozi waliohudhuria katika tukio hili pamoja na kumshukuru na kumkaribisha Rais katika tukio hilo. Zaidi ya hayo Mkuu wa Mkoa ameeleza baadhi ya miradi na mafanikio yaliyotelekezwa na awamu ya tano.

Mhandisi na mtendaji Mkuu wa TANROADS Mfugale amepata nafasi ya kuzungumza na kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu ujenzi huu wa SGR. Ameeleza kuwa Mradi huu unatarajiwa kukamilika Mwezi januari mwaka 2021.

Zaidi ya hayo, Viongozi mbalimbali Wabunge na Mawaziri wamepata nafasi ya kuzungumza ambao wote kwa pamoja wameendelea kumpongeza Rais Magufuli kutokana na maendeleo na miradi mbalimbali aliyoifanikisha katika mkoa wa Morogoro.

Rais Magufuli: leo ni siku muhimu sana. Nimeweka jiwe la msingi la ujenzi wa Mahandaki manne yenye urefu wa km 2.7 ukijumlisha barabara ya juu ya aina yake ya nusu kilomita itakayojengwa hapa, sasa barabara za juu haziko Dar es Salaam tu hata Kilosa zipo

Amesema mara yake ya kwanza kuona barabara ya kupita chini ya Mlima aliiona Uingereza alipokuwa anasoma, lakini amefarijika sasa kuna reli ya hivyo Tanzania

Amesema wapo waliomuona anaota wa kuwa aliposema nataka kujenga reli. Amewapongeza viongozi wote wa dini na wanachi kwa ujumla kwa juhdui zao za kufanikisha reli hiyo iliyogharimu Tsh Trilion 6.05

Amesisitiza kutumia fedha za ndani, kutumia cash kukamilisha ujenzi huo

Amesema anatambua matatizo yanayowakumba watu wa maeneo hayo kuwa ni migogoro ya mashamba, ambayo ni kwa kuwa mashamaba mengi yamechukuliwa na matajiri na wameshafuta mashamba zaidi ya 40,

Alichotaka kifanyike kwa wilaya ya Kilosa, wajadili jinsi ya kuyagawa bure mashamba yaliyofutwa, mashamba hayo yatagawiwaw kwa wananchi masikini. Amesema kuwa migogoro hiyo inawahusisha kwa kiasi kikubwa viongozi

Magufui aagiza ndani ya siku sabab mashamba mengine yaliyobaki wayafute na kisha kuyagawa kwa raia


RAIS ATAJA SABABU ZA KUWAFUKUZA VIGOGO MTERA
Amesema viongozi walikuwa wanafungulia maji bwawa la Mtera ili waseme kina cha maji kimepungua, ili umeme uwe wa mgao ili waweze kuuza majenereta

Pia amezungumzia matatizo mengine ikiwemo kuuza vitu ghafi na kuagiza vitu kama tomato sauce, kwenye upande wa pamba tulikuwa tunauza pamba ikiwa ghafi ambayo walionunua walitengeneza nguo na kuvaa kisha kuturudishia mitumba

Nipo na wafuasi wa Chadema wamezima Tv. Wamaenza kunywa konyagi wanachukia kama hawana akili. Lijualikali anasalimia wanavunja konyagi wanatoka nje.
 
Back
Top Bottom