peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 14,255
- 23,949
PSSSF na NSSF wana pesa ya kufanya miradi, lakini pesa ya kumlipa mfanyakazi aliyetumikia Taifa na kchangia mifuko hiyo kwa miaka Mingi na badae kupoteza ajira na kuendelea kuteseka na familia yake, Hawana..!!Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akifungua kiwanda cha bidhaa za ngozi Mkoani Kilimanjaro ambacho kimejengwa na PSSF.
Amesema kuwa mifuko hiyo ya hifadhi ya jamii iwekeze zaidi kwenye viwanda badala ya kujenga majengo. Akitoa ufafanuzi wa kauli yake, amesema unakuta jengo limejengwa kwa mabilioni halafu wapangaji wapo nusu ya jengo huo ni opotevu wa fedha.
Akaongeza kuwa ukijenga kiwanda unakuwa umetengeneza ajira, mfano kiwanda hicho cha ngozi kitaajiri watu 3000 ambao watakuwa waajiriwa wa kudumu achilia mbali wale wa kupeleka bidhaa kuuza nk.
Ametoa wito kwa mifuko ya jamii kujenga viwanda vingine.