Rais Magufuli azindua umeme wa gesi asilia Kinyerezi II, asema ataendelea kushirikiana na wananchi kulinda amani

Rais Magufuli azindua umeme wa gesi asilia Kinyerezi II, asema ataendelea kushirikiana na wananchi kulinda amani

Kuna mama kavaa tisheti ya ccm ila picha ni ya JK na kanuna nadhani hata chai hajanywa
 
Mimi hata kama ningekuwa na chama, kama Mtanzania, nafuatilia mipango na mikakati ya uchumi na maendeleo, kwa mtazamo wa kina. Wewe na wenzio endeleeni na siasa za majukwaani.

Labda nikuulize, hao viongozi wako wakiruhusiwa mikutano ya hadhara na maandamano, ndiyo nchi itaendelea?

Ada ya mwungwana ni vitendo. Serikali inajenga na kuboresha: Elimu na mazingira yake (km madawati shuleni); Afya; Maji; Umeme; Njia za usafiri nk. Mnayaona mabadiliko hayo lakini mnaona demokrasia ya maneno ndio kipaumbele chenu.

Mnajua ukweli jinsi mnavyotengeneza matukio ili nchi isitawaliwe na kudai maandamano kwa nia ya kujenga chuki ndani ya wananchi. Kuthibitisha Serikali iko makini, na inazijua mbinu chafu za CHADEMA, viongozi wake wamekamatwa na sheria itachukua mkondo wake, hilo halina ubishi. Wewe na wenzio endeleeni kujifariji kwa kejeli za matusi humu tu JF.

MNAJIAIBISHA
Ahsaante sana mkuu,

Lakini huko kwenye elimu unafikiri ni kweli kuna cha maendeleo kilichofanywa mpaka sasa au kwa vile sie tupo vijijini ndio maana hatuyaoni, maana tunashuhudia madudu hatujawahi ona (huku kwetu sijui kwenu)
 
tehetehe waziri muhusika yuko wapi?
nashangaa kila siku huyu jamaa anazindua na kutumbua tehetehet
Unge categories miradi anayotakiwa kuzindua rais,makamu rais,Waziri na viongozi wengine ili ijulikane mkuu.
 
CHADEMA roho zinawauma utadhani huo mradi hawatautumia, mijitu mingine hovyo kweli..

siku mkijenga makao makuu mapya ya chama ufipa, mnaweza kumwalika rais aje azindue....
 
Ahsaante sana mkuu,

Lakini huko kwenye elimu unafikiri ni kweli kuna cha maendeleo kilichofanywa mpaka sasa au kwa vile sie tupo vijijini ndio maana hatuyaoni, maana tunashuhudia madudu hatujawahi ona (huku kwetu sijui kwenu)
Inategemea mabadiliko katika elimu unayatazamaje. Kuna la miundo mbinu (km majengo), vifaa vya elimu, mitaala, walimu, utayari na uwezo wa wanafunzi nk. Kama ilivyo katika sekta ya huduma ya jamii (afya, maji, umeme) mahitaji ni mengi. Hilo la kutoa elimu bure, tukubali tusikubali limewapunguzia mzigo familia zenye uwezo mdogo kumudu gharama za kuelimisha watoto wao.
 
Hata JK alizindua vingi na vingine vilizinduliwa na mawaziri wake lakini kura zake ziliendelea kuporomoka.

Issue ni ajira,uchumi,watu kupoteza ajira, biashara kufungwa,mazao ya wakulima kukosa soko,bidhaa kupanda bei,kushindwa kuboresha masilahi ya watumishi,kodi zisizo rafiki kwa wafanyabiashara,n.k

Mengine ni sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii,mafao kwa wastaafu na wanaocha kazi,makato ya asilimia 15 kwa ajili ya Bodi ya Mikopo, manyanyaso kwa watumishi na wapinzani,Ma-DC na Ma-RC kuweka watu ndani hovyo hovyo,n.k.

Vile vile mengine ni kama tuhuma za mauji,utekaji,police brutality,lugha za kebehi, viburi,dharau,doublestandard,bomoabomoa,n.k

Sasa ni maendeleo ya vitu na si maendeleo ya watu na hili ndio tatizo.
Kuna utofauti gani wa maendeleo ya watu na vitu?
Je Kuna maendeleo ya watu bila maendeleo ya vitu?
Hivi inawezekana nchi kuendelea bila ya umeme wa uhakika, miundombinu bora, bila viwanda?
Hata hicho kilimo kitapata vipi soko pasipo viwanda
 
Kamanda yaani kabisa na akili zako zote unamfananisha JK na JPM?!
Japokuwa JPM ana miaka takribani 3 tu madarakani ila hakika JK kaachwa mbaali mno!
Alichomzidi sanasana labda ni uhandsome tuu, ofkoz na lugha nzuri adhimu ya kiswahili!!.
teh teh teh teh.
Jamaa yuko mbali sana kwa JK.
Jk hayawahi sema aembewe,
Jk hajawahia mbiwa atubu.

Kizuri zaidi hata ambavyo amekuwa aki-tend kuvizindua, ni ama vilijengwa na Jk au ni mawazo za JK
 
Mimi sio mhandisi ila kwa ninavyokumbuka huo mradu wa kinyerezi II MW ambazo zilikua zikitangazwaga zilikua hazizidi 150 MW labda ninachanganya na Kinyerezi I, ila kiuhalisia hazifiki 240 MW najua nitaonekana mpinzani ila mwenye kumbukumbu zaidi aje atuambie vizuri nahisi ni kati ya MW 94 na zingine MW 50
Duh!! Sasa mkuu unahisi lakini bado unapinga wahusika wakuu(Serikali).

Nilidhani upo ndani kabisa mkuu.
 
Back
Top Bottom