Maneno Meier
JF-Expert Member
- May 12, 2013
- 2,467
- 1,697
Nianze moja kwa moja na mada yangu,
Kwa mara yangu ya kwanza napenda kumshukuru Mh Tundu Antipati Lissu kwa mawazo mazuri aliyo yatoa jana katika ziara yake ya kutembelea mitaa ya kariakoo kuhusu mobility kwenye jiji letu la Dar.
Nikilinganisha mawazo haya na hotuba ya Rais Magufuli leo kwenye uwanja wa Mkapa, nasikitika kusema, hapa nadhani Rais wetu hajajua nini maana ya mobility katika jiji kubwa na lenye watu wengi kama la Dar es salaam. Rais Magufuli bado una fikra za kudhani kuwa mabasi ya mwendo kasi ndiyo ufunguo wa kutatua tatizo la usafiri wa watu jijini.
Kwa hotuba yako hiyo naona kweli bado hujajua tatizo linalo ikabili jiji letu. Na nathubutu kusema tena kuwa Rais Magufuli hujui nini maana ya mobility katika jiji kubwa kama la Dar. Rais Magufuli nafikiri huoni kitu kingine zaidi ya barabara, Flyovers, madaraja na majengo. Nafikiri unapenda sana kusikia harufu ya maconcret na betumen.
Katika hotuba yako ya leo nimesikitika kutosikia exactly concept yako ya kuondoa tatizo linalo wakabili vijana wengi jijini la ajira. Kwenye mawazo yako ya ku-create ajira kwa vijana naona umemung'unya tu maneno.
Rais Magufuli chukua mawazo ya wenzako. Wewe huwezi kuwa Mungu wa kujua kila kitu. Hata Mungu aliwaumba malaika kabla ya kumwuumba binadam, kwani alijua kuwa malaika watamsaidia katika kummpa ushauri wa kutatua matatizo yanayo wakabili binadam duniani.
Mtu akizungumzia uzalishaji wa ajira hamaanishi makandarasi na maengineer wakutengeneza mabarabara, madaraja, ma-flyover na majengo pia melanika na madereva wa kutengeneza na kuyaendesha mabasi ya mwendobkasi tu, bali anamaanisha uzalishaji wa ajira zenye skils na creativity. Katika hili naona katika sera zako na CCM yako bado mko mbali sana.
Rais Magufuli naomba nikuulize swali, hivi lile swala la Commuter trains limeishia wapi? Na lile la bonde la Msimbazi je? Mbona sikusikia ukiyazungumzia tena?
Rais Magufuli nakuomba tafadhali sana kupiga akili ya kufikiria na kutekeleza miradi ya kimkakati ambayo kweli italeta ajira za kudumu na maarifa ya kuliendeleza jiji letu na taifa letu kwa ujumla.
Ili kudumisha miundo mbinu ya uhakika ya jiji la Dar es salaam sambamba na mabarabara na Flyovers uliyokusudia kuyajenga na kuyasambaza jijini Dar es salaam, achana na fikra zako za kueneza mabasi ya mwendo kasi kwenye routes ulizo zitaja kama:
Route ya Kariako mpaka Mbagara Kuu kwenye awamu ya pili na nyinginezo ulizokusudia kwenye awamu za tatu, nne, tano na sita badala yake nikuombe kuweka trams kama Lissu alivyo sema au kupendekeza kwenye hiyo clip yake.
Mabasi ya mwendo kasi yanatakiwa yawe kiunganishi cha vitongoji vya mbali na mji kama Goba na mwenge au kawe au maeneo yasiyo kuwa na Trams.
Maeneo kama Mkuranga, Bagamoyo, Kibaha, Kisarawe na kadhalika mpaka Mainstation Commuter trains zilitakiwa ku-operate. Usafiri wa aina hii unaleta teknolojia mpya na kuzalisha ajira nyingi. Sambamba na hayo upeo wa maarifa unapanuka na hivyo kupunguza idadi ya vijana wasio weza kujiamini na kuwaza vizuri.
Zaidi ya hayo Rais Magufuli kama bonde la Msimbazi nalo utalifanyia kazi ili liwe kivutio cha utalii, kama Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam aliyepita, RC Makonda, alivyo tuhabarisha, ingekuwa safi sana.
Na kama hospitali zetu za Dar es salaam Mwananyamala, Muhimbili, Magomeni, Mnazimmoja na Amana ukaziunganisha kwa sky trains ku cross bonde la msimbazi, duh!Yaani hapo ungekuwa umemaliza kila kitu.
Kingine ambacho ni cha umuhimu sana jijini Dar es salaam na pia fursa kubwa ya kutengeneza ajira ni sewage systems na Sewage Water Purifying Plants na pavements. Haya mambo ya kujenga mitaro ambayo iko wazi kandokando ya barabara za mijini au kwenye makazi ya watu ni upuuzi wa hali ya juu.
0Mifereji ya maji taka mijini mara nyingi hupitishwa chini ya ardhi na serikali inatakiwa kuwa na kampuni ya uendeshaji wa mradi huu ambao unatoa ajira za kudumu kwa vijana.
Bila kukusanya wanadiaspora na wenyeji wenye utaalam wa kutengenza SGR ili tupige SGR yetu tukianzia Dar mpaka Bagamoyo na tukifanikisha tupige High speet train yetu wenyeww kutoka Dar kwenda Mtwara na kadhalika.
Vijana wa leo wanataka pia free access ya internet. Sambaza WiFi Technology nchi nzima na hasa mashuleni. Samabaza Laptop au Tabletts za kusomea kwenye shule zote ili wanafunzi wapanue maarifa na kugundua talents zao na ahidi kutoa chakula shuleni bure. Mwanafunzi ataelewa nini wakati ana njaa?