Rais Magufuli: Benki ya Dunia wanatoa pesa wakijua Tanzania tuna msimamo gani na tunafanya nini, wapiga kelele wapuuzwe

Nini chanzo cha mzozo wa huu mkopo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..lakini kununua ndege cash halafu kwenda kukopa kwa ajili ya elimu siyo busara hata kidogo.
NANI AMEKUAMBIA QAMWNUNUA NDEGE CASH? WAMEKOPA KULE WAKA LIPA HUKO CASH. THAT MEANS DENI JUU YA DENI. NA MANDEGE YENYEWE NI KAMA PICHA HAYAINGIZI ANY INCOME AMA KWELI SIFA ZINAUA
 
Ni kweli wapiga kelele wapuuzwe tu hakuna namna, wewe unapiga kelele na bado serikali hiyo hiyo inakuhudumia,unaishi kwa amani pamoja na njaa yako na shida zako lakini bado tu unapiga kelele,usaidiweje sasa?

nitarudi baadae
Serikali ina-exist kwa hisani ya wananchi na wala wananchi hawa-exist kwa hisani ya serikali.

Ukilielewa hilo ndio utakuwa walau na akili kidogo.
 
Ila sasa ule mchezo wa kutudanganya kuwa miradi inafanywa kwa hela za ndani ndio wakome kutwambia uongo kama huo.

Hii nchi ni 100% Donor Dependent, kama hata vitu muhimu kama elimu ambayo mnaiweka mbele kwenye orodha ya vipa umbele vyenu kumbe hamna hata mkakati wa kuushughulikia ni wananchi gani watawapigia kura kuwarejesha madarakani, lazima tu ma-DED wawaokolee jahazi, make hamna namna.
 
Serikali ina-exist kwa hisani ya wananchi na wala wananchi hawa-exist kwa hisani ya serikali.

Ukilielewa hilo ndio utakuwa walau na akili kidogo.

Kushea uraia na akili nyingine ni mzigo. Kuna Mtanzania mahali ana uwezo wa kurusha satellite lakini hatofanikiwa kwa vile tu yuko kwenye nchi moja na Fred mwakitundu
 
Daah Hawa world Bank haya Sasa wameshawasikia wapiga kelele! No mkopo
 
wamesema Tanzana ni donner country sasa mbona bado wananyoosha mkono?
 

Sasa kama ni wa kudharauliwa, basi hasingelisema. Yeye mwenyewe angenyamaza. Sasa yeye anawajibu alafu anawaambiwa watu wasiwajibu.
 
Serikali yetu inajichanganya, inachanganya washirika wetu wa maendeleo, au watendaji wake wamezoea kauli za uongo na unafiki?
1. Inajinasibu kuwa nchi hii ni tajiri ina inakusanya pesa za ndani za kutosha kutekeleza miradi ya maendeleo bila kutegemea ufadhili kutoka nje ya nchi, na
2. Tunasahau kazi za mabolozi nchini, kama ilivyo kwa mabolozi wetu wanaowakilisha Tanzania nchi za nje, ni zipi.
Hata hivyo viongozi wakuu wa nchi wanaposimama majukwaani na kudai kuwa hakuna ubaguzi katika elimu, wanadanganya na kufurahisha nani?
Waziri wa mambo ya nchi za nje alinukuliwa akidai eti "wanafunzi waliozaa wamewekwa kwenye utaratibu ulio nje ya mfumo rasmi wa elimu"!
 
Mara Oooh hatubabaishwi na mabeberu, Mara Oooh hatutaki pesa za mashoga!

Shwaini.Mbona mnaulilia huo mkopo sasa?
 
wamesema Tanzana ni donner country sasa mbona bado wananyoosha mkono?
Tanzania bado sana!
Shida ni hz:
1. Uongo na unafiki,
2. Kujisifia kupita kiasi, na
3. Kuishi kwa matumaini.
Uongo na unafiki ni tabia za watanzania karibu wote hata viongozi wanazo. Wanasema yasiyo ya kweli na wasiyoyaamini.
Watanzania pia wanapenda wasifiwe kwa mambo madogo madogo na wasiyohusika nayo moja kwa moja.
Siasa za malipo kutokana na fidia za makenikia zilipelekea uchumi wa nchi kutikisika na kutufikisha pabaya tulipodhani tungezipata; tungeamka tumetajirika. Hatukujua kuwa yalikuwa ni matarajio tu kama ya "mateja" wanaojikuta "peponi" ghafla. Tulianza kutumia fedha za mikopo na zisizokuwepo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…