Rais Magufuli: Benki ya Dunia wanatoa pesa wakijua Tanzania tuna msimamo gani na tunafanya nini, wapiga kelele wapuuzwe

Rais Magufuli: Benki ya Dunia wanatoa pesa wakijua Tanzania tuna msimamo gani na tunafanya nini, wapiga kelele wapuuzwe

Nawaza kwa kutumia vidole kwa muda

World Bank sio watoto, ni mabeberu wenye ofisi zao nchini.

Wanajua, wanaona na wanasikia vinavyoendelea.

Mtazamo kuwa ni watu wa ajabu walio mbali wasiojua chochote hadi mtu mimosa msaliti awavijishie siri kwa mambo yaliyowazi au atuchonganishe sio sahihi.

Nadhani mjadala utoke kwa Zitto na uzito wake urudi kwa WB na sababu zao kama zina mashiko.

Dunia ni familia tuanze kujadili mambo na hoja zake sio watu na itikadi zao.

WB watakuwa wajinga sana ikiwa nao wanapelekeshwa na mawazo ya mtu na sio facts zilizotafitiwa.
 
Mimi kama Beberu Nasema Pesa Sitoi mpaka mtakapoingia Heat
 
Ni kweli wapiga kelele wapuuzwe tu hakuna namna, wewe unapiga kelele na bado serikali hiyo hiyo inakuhudumia,unaishi kwa amani pamoja na njaa yako na shida zako lakini bado tu unapiga kelele,usaidiweje sasa?

nitarudi baadae
Matured Crap
 

Rais Magufuli akiwa katika hafla ya kuwaapisha mawaziri na mabalozi Ikulu leo, amesema kwamba kuna mambo mengi yamezungumzwa na tuyapuuzie. Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia alikuja hapa, mwaka jana, kwahiyo wanatoa pesa wakijua sisi Tanzania tuna misimamo gani na tunafanya nini, hao wengine ni wapiga kelele tu, wala msiwajibu kwasababu watu wa namna hiyo hawaishi duniani.

Awali wiki iliyopita, zilikuja taarifa kwamba Benki ya Dunia WB imesema inafikiria uwezekano wa kuikopesha Serikali ya Tanzania mkopo wa dola za kimarekani milioni 500 sawa na Trilioni 1.152 za Kitanzania kwa ajili ya kuboresha sekta ya Elimu, mkopo uliokuwa umesimamishwa na benki hiyo kutokana na Rais Magufuli kutangaza kuzuia wanafunzi wanaopata mimba wakiwa shuleni kutoendelea na masomo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, benki ya Dunia imedai kuwa ilipokea barua kutoka wanaharakati kutoka nchini Tanzania ambao walieleza kuwa, Benki ya Dunia kuendelea kutoa mkopo huo ni kuendelea kuwabagua wanafunzi kwa kigezo cha waliojifungua, wenye ujauzito na wasio Wajawazito.

Hivyo walitaka benki hiyo kusitisha mkopo huo tangu mwaka 2018, mpaka serikali itakapobadili sera yake ya kumzuia mwanafunzi aliyepata mimba kuendelea na masomo.

Pia soma > Tanzania yaweza kukosa Mkopo wa Dola Milioni 500 kutoka Benki ya Dunia
Alifikiri ni sawa na anavifanya kuwa kila kitu akisema ni sawa. Akili yake ikamtuma kuwa ukishaongea na makamu basi ela inatoka. Nakujua kuwa kwa wenzetu lazima wakae na wataalam na kupitia kila kipengele. Alijua kapata pesa za uchaguzi. Imekula kwake wamebaki kutoa kafara (Moshi)
 
Taratiibu ...what called makelele yatajibiwa tu - haya mambo bana huwa hayarukwi ama kukwepeka!!
 
Back
Top Bottom