Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,746
- 5,772
Mh Rais wewe kama Amiri Jeshi Mkuu huu ndio wakati kulifanyia mabadiliko Jeshi la Polisi. Liwe jeshi la kisasa ambalo lina askari wenye weledi na maadili.
Fanya mabadiliko liwe Jeshi la kulinda raia na mali zao na sio jeshi la kulinda watawala (legacy iliyoachwa na wakoloni).
Fanya mabadiliko liwe Jeshi la kufanya kazi kwa kufuata misingi ya sheria (sio kukaa na watuhumiwa siku kumi bila kuwapeleka mahakamani). Ubambikizaji kesi kwa wananchi uishe na utoweke kabisa.
Mabadiliko haya yafanyike kwa kulifumua jeshi lote. (ondoa makamanda wote ambao wana zaidi ya miaka 55 maana hawa bado wana element za jeshi la mkoloni)
Idara ya upelekezi iwe huru isiwe ndani ya Jeshi la Polisi.
Na haya mabadiliko yafanyike kabla ya uchaguzi. Wale wote ambao wanaonea raia na kuwatesa (wanakusigizia ulitoa amri waue majambazi) unda tume wote uwafute kazi. Maana kuna watu wanabambikiwa kesi za ujambazi hata kama ni wauza gongo.
Wale wanaoua majambazi ya ukweli yakiwa na silaha wabakize na uwaongeze mshahara.
Jeshi la sasa hivi linachafua taswira ya nchi yetu. Tunaonekana hatufuati misingi ya haki za binadamu.
Fumua jeshi lote unda upya jeshi la kisasa.