Rais Magufuli futa Halmashauri za Wilaya zinafuja pesa na kurudisha nyuma maendeleo. Report ya CAG ya 2018-2019 inaonesha wazi hili

Mathanzua

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2017
Posts
17,251
Reaction score
22,929
Tumekuwa tukishauri kwa muda mrefu sasa kwamba Halmashauri za Wilaya zifutwe kwa kuwa hazina tija kwenye maendeleo ya wananchi. Hii haitakuwa mara ya kwanza kuzifuta halimashauri hizo, kwa kuwa huko nyuma kitu kama hicho kilishafanywa na Mwalimu Nyerere, ambapo alizifuta mwaka 1972 na kuzirejesha tena mwaka1982.

Hata hivyo ushauri wetu has fallen on deaf ears, huku matumizi mabaya ya fedha za Watanzania katika halimashauri ukiendelea anabated na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi. Tatizo la matumizi mabaya ya fedha katika halimashauri zetu limekuwa sugu miaka nenda miaka rudi.Tafadhali fuata link ifuatayo ulione hili.

Historia ya Serikali za Mitaa Tanzania – hitimisho

Naomba ikumbukwe kwamba halmashauri ndiyo immediate stakeholders wa maendeleo ya wananchi, halmashauri zikiyumba, maendeleo ya wananchi nayo yanayumba.

Rais Magufuli amepokea ripoti ya Control and Auditor General ya 2018-2019. Pamoja na upokeaji wa report hiyo, Rais ameongeleo mambo mengine ya msingi ambayo yanaihusu nchi yetu. Amesema kwa mfano kwamba amesikitishwa na duru ambazo zilitegemea kwamba shuhuli kama chaguzi zingesimama kwa sababu ya COVID-19.

Amesisitiza kwamba hata katika nchi ambazo zimeathiriwa zaidi na ugonjwa huo, shughuli kwa mfano za Bunge bado zinaendelea. Amesema kazi ni lazima ziendelee na Bunge litaendelea na ratiba zake kama kawaida kama ilivyopangwa. Aliongeza kwamba uchaguzi nao utaendelea kama ilivyopangwa come November, hautaahirishwa.

Report aliyowakilisha CAG pamoja na mambo mengine inaonyesha kwamba upo ubadhirifu mkubwa katika serikali za mitaa,ambapo Billioni 14 zimetumika kwenye miradi ambayo haikukusudiwa.

Mr Kichere said that about Sh1.13 billion was swindled by unscrupulous officials. He further said that about Sh1.52 billion was used without the approval of procurement boards in various districts. He also indicates that Tanzania missions abroad have been using a lot of money to pay rent.
 
Rais Magufuli futa Halimashauri za Wilaya wanafuja pesa
Umeongea bila kufikiri nadhani, azifutaje Halmashauri, zisiwepo au ziunganishwe na nyingine? Hilo litasaidiaje hela kurudi au kutofujiwa?
 
Mfumo unaweza kuwa na Mkuu wa Wilaya,DAS na maofisa wengine wa ngazi za juu za Wilaya.Majukumu yote kuhusu Wilaya yawe chini yao.Narudia tena,it has been done before,it can be done now.Watu hawawezi kuendelea kufuja pesa za wananchi kiasi hicho.Halimashauri zineshindwa ku-deliver kabisa,they should go.

.
 
Kwamba wakuu wa wilaya ni waaminifu sana kuliko Halmashauri?
 
Mfumo wa serikali kuu ni rahisi zaidi kuuthibiti kuliko wa serikali za mitaa mkuu.Serikali za mitaa ni soko huria katika kila jambo,weledi na uaminifu sio mambo ya msingi sana kwao,it's know me,know who that is important.This is obvious,mbona haya yako wazi.

Ipo case moja ya jamaa mmoja wa darasa la tatu ambaye alitoroka shule akajingiza kwenye kukwapua mali za wasafiri kwenye mabasi na kufanya uovu mwingi.Mtu huyu somehow kwa kutumia mbinu chafu leo ni diwani,halafu mbaya zaidi ni msaidizi wa Mwenyekiti wa Halimashauri.Hivi realistically mtu kama huyu anaweza kuwa muadilifu kweli?Mkuu let's be serious.Hivi unategemea nini kutoka kwa mtu kama huyo,kama sio ukwapuzi tu kweli kwenye halimashauri alipo,and that is exactly what is happening.This guy has created alliances and networks ambazo zina husika na wizi wa fedha za halimashauri.

Ni halimashauri ngapi zina mambo ya namna hii sijui,lakini kwa jinsi Rais na Waziri wanavyolalamika, inaelekea tatizo ni kubwa sana.
 
Ipo case moja ya jamaa mmoja wa darasa la tatu ambaye alitoroka shule akajingiza kwenye kukwapua mali za wasafiri kwenye mabasi na kufanya uovu mwingi.Mtu huyu somehow kwa kutumia mbinu chafu leo ni diwani,halafu mbaya zaidi ni msaidizi wa Mwenyekiti wa Halimashauri.Hivi realistically mtu kama huyu anaweza kuwa muadilifu kweli?Mkuu let's be serious.Hivi unategemea nini kutoka kwa mtu kama huyo,kama sio ukwapuzi tu kweli kwenye halimashauri alipo,and that is exactly what is happening.This guy has created alliances and networks ambazo zina husika na wizi wa fedha za halimashauri.
Diwani sio mwajiriwa wa Halmashauri
 
Tumekuwa tukishauri kwa muda mrefu sasa kwamba Halmashauri za Wilaya zifutwe kwa kuwa hazina tija kwenye maendeleo ya wananchi. Hii haitakuwa mara ya kwanza kuzifuta halimashauri hizo, kwa kuwa huko nyuma kitu kama hicho kilishafanywa na Mwalimu Nyerere, ambapo alizifuta mwaka 1972 na kuzirejesha tena mwaka1982.

Hata hivyo ushauri wetu has fallen on deaf ears, huku matumizi mabaya ya fedha za Watanzania katika halimashauri ukiendelea anabated na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi. Tatizo la matumizi mabaya ya fedha katika halimashauri zetu limekuwa sugu miaka nenda miaka rudi.Tafadhali fuata link ifuatayo ulione hili.

Historia ya Serikali za Mitaa Tanzania – hitimisho

Naomba ikumbukwe kwamba halmashauri ndiyo immediate stakeholders wa maendeleo ya wananchi, halmashauri zikiyumba, maendeleo ya wananchi nayo yanayumba.

Rais Magufuli amepokea ripoti ya Control and Auditor General ya 2018-2019. Pamoja na upokeaji wa report hiyo, Rais ameongeleo mambo mengine ya msingi ambayo yanaihusu nchi yetu. Amesema kwa mfano kwamba amesikitishwa na duru ambazo zilitegemea kwamba shuhuli kama chaguzi zingesimama kwa sababu ya COVID-19.

Amesisitiza kwamba hata katika nchi ambazo zimeathiriwa zaidi na ugonjwa huo, shughuli kwa mfano za Bunge bado zinaendelea. Amesema kazi ni lazima ziendelee na Bunge litaendelea na ratiba zake kama kawaida kama ilivyopangwa. Aliongeza kwamba uchaguzi nao utaendelea kama ilivyopangwa come November, hautaahirishwa.

Report aliyowakilisha CAG pamoja na mambo mengine inaonyesha kwamba upo ubadhirifu mkubwa katika serikali za mitaa,ambapo Billioni 14 zimetumika kwenye miradi ambayo haikukusudiwa.

Mr Kichere said that about Sh1.13 billion was swindled by unscrupulous officials. He further said that about Sh1.52 billion was used without the approval of procurement boards in various districts. He also indicates that Tanzania missions abroad have been using a lot of money to pay rent.
Bunge linapopangiwa mambo na rais.
Mbadala wa Halmashauri ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Diwani sio mwajiriwa wa Halmashauri
Sio,lakini yupo kwenye system ya Halimashauri.Halimashauri isipokuwepo na Diwani hayupo.

Hata hivyo naomba nisisitize,hata kwa waajiriwa wengine,system ya ajira ni ya kujuana,weledi sio issue kihivyo.Kama wewe uko karibu na Mkurugenzi,Diwani,Mwenyekiti wa Halimashauri au bosi wa kitengo,ajira is certain, tena kwenye kitengo nyeti,ili ufanikishe issues.Tunajua mkuu,mbona hata wenyewe wanahakikisha haya.
 
Tatizo la Nchi yetu lipo kwenye mfumo wa uendeshaji wa Serikali. Huu mfumo tulio nao ni wa enzi ya Hayati Baba wa Taifa Mwl Nyerere. Ulikuwa based on trust zaidi kuliko kuwa wa wazi ulio na check and balance.
Pili, Serikali yetu imekuwa na upungufu wa Watendaji kwani kwa sasa ili uweze teuliwa nafasi yoyote ni lazima uwe wa kutoka chama tawala. Sio kila Mtanzania ni mwanachama wa chama cha Siasa....kuna Watz wengi tu na wazuri wala hawana kadi ya chama chochote...Serikali ipanue wigo wa teuzi zake kigezo kiwe utendaji kazi bora na uadilifu
Tujiulize kwenye ofisi za chama waru wake wanafanya kazi gani kila siku?
Bila mabadiriko hayo ya msingi tutaemdelea kusikia madudu kila uchwao
 
Back
Top Bottom