Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Huyu sijui kama alikuwepo nchini hawezi kuwa na haya mawazo kwamba kwake ni kitu kipya hakuwahi sikia kikifanyika
 
Huyu jamaa a
Anataka kujiuzuru, nini? Corona siyo mchezo! Jamaa anaogopa corona kuliko ukoma. Kwa nje utamsikia: haka kamafua ka kolona...
Anasema nyie mtulie msiogope wakati yeye katoka nduki.
 
Wengi hamuwezi kumuelewa hii ni kutokana na kuzoea kumeza madesa,uvivu wa kufikiri na kutofuatilia mambo.
Jiulizeni maswali yafuatayo:-

1. Daktari wa kwanza kugundua jamii ya kirusi hiki kinachosababisha covid 19 alimgundua virus huyo mwezi November 2019 wakati virus huyo ameshafanya yake.
Swali la kujiuliza,ni lini alianza kushambulia watu?

2. China hawakukubali ugunduzi huo na kumwona daktari huyo kama mzushi,na alifungwa.Je ni watu wangapi waliokuwa free kusafiri muda huo kwani China hata hawakuchukua hatua yoyote wakati huo hadi hapo January?

3. Je mmefuatilia ni wageni wangapi kutoka nchi zilizokuwa zimeathirika walioingia nchini kuanzia mwezi October 2019 hadi March 2020?

4. Je kuna takwimu zozote za wagonjwa waliougua ugonjwa wenye dalili zinazofanana na covid 19 kabla ugonjwa haujatangazwa?Je mnadhani hakuna watu waliokuwa na ugonjwa wenye dalili kama hizo?

5. Tunaambiwa ugonjwa hauna tiba,je hata ukipima watu ambao hawaumwi,na ukawagundua,inasaidia nini?

6. Je kujitangaza kuwa mna wagonjwa wengi,kuna hasara yoyote kiuchumi?Na je wakiugua na kutibiwa hospitali bila kutangazwa kuna mtu atapata hasara?

7. Je ugonjwa huu usipoisha kabisa,unadhani nini kitaendelea?Unadhani maisha yatasimama?

Mwisho naunga mkono maamuzi ya Rais ni ya mtu mwenye hekima sana.Ni vigumu sana kama una akili nyepesi ya kuwaza saa ya kula ugali tu,kuelewa nia ya Mkuu wetu wa nchi.Wengi wanafuata maelezo ya wataalamu wanaokopi tu mambo kutoka kwa watu weupe bila hata kufikiria kwa kina kwa kuangalia mazingira yetu

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilikua sijui kama kianzisha mada JF ni kitu rahisi namna hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Magufuli anatarajiwa kuzungumza mbashara na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhusu ugonjwa wa Corona kutokea Chato saa 9:45 alasiri leo tarehe 22.4.2020

FUATILIA LIVE:



--

HOTUBA YA RAIS MAGUFULI (KWA UFUPI)

Rais ameshauri tuendelee kutumia njia za asili kama kujifukizia ili kupunguza corona.

Watanzania tuendelee kuchukua hatua za tahadhari, ugonjwa huu wa COVID-19 upo na ni hatari

Navipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuchukua hatua mbalimbali za kuilinda nchi yetu hasa katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya COVID-19, nimekubaliana na hatua mnazoendelea kuzichukua katika kipindi hiki”-

Nawapongeza viongozi wa Dini na watanzania kwa ujumla kwa kuitikia wito wa kuliombea taifa kwa siku 3 dhidi ya ugonjwa wa COVID-19, nina amini Mungu wetu ni wahuruma atatusikiliza na siku moja tutalishinda hili gonjwa.

Nawashukuru kwa kuja kunipa 'briefing' za jinsi tunavyoendelea kupambana. Nimekubaliana na hatua mnazoendelea kuzichukua katika kipindi hiki - Napenda kushukuru Watanzania ambao kwa nyakati za maombi tulizotangaza kwa siku 3, wote walishiriki

Nawapongeza Madaktari, Manesi na Wahudumu wote wa sekta ya afya nchini ambao kila mmoja katika maeneo yao ya kazi wameendelea kutoa huduma kwa wagonjwa wa magonjwa mbalimbali na wagonjwa wa COVID-19.

endeleani na moyo huo wa uzalendo, mnafanya kazi ya Mungu ya kuwahudumia Watanzania, msivunjike moyo, Serikali ninayoiongoza ipo pamoja nanyi, ninatambua kazi kubwa mnayoifanya.

Natoa wito kwa watanzania kupuuza taarifa za upotoshaji zinazotolewa kupitia mitandao ya kijamii na watu kutoka nje ya Tanzania kuhusu ugonjwa wa COVID-19”

Tujaribu kutumia njia nyingine za asili kama kujifukiza. Kujifukiza ni scientific kwa kuwa mvuke wa maji, maji yanakuwa vapour yakiwa 100 degree centigrade ambazo zinatosha kumyeyusha hata #CoronaVirus

Wizara ya Afya waeleze namna gani kujifukiza kunakinga dhidi ya #COVID19. Njia za kutumia hata kuchanganya na muarobaini na vitunguu swaumu zitumike

Dar es Salaam ina wagonjwa wengi kwasababu ni ‘great city’ ambayo lazima iwe na wagonjwa wengi. Nimeteua Katibu Mkuu mpya ili takwimu za wagonjwa wanaopona ziwe zinatangazwa ili wananchi wawe na confidence

Lakini pia taarifa zetu ziendane na ukweli hasa katika watu wanaopona. Nina taarifa kwamba mpaka leo tulikuwa na wagonjwa 284, lakini naambiwa karibu 100 ya wagonjwa walishapona. Hizi takwimu za wagonjwa wanaopona nazo zitangazwe ili kuwaondolea hofu wananchi.

Hakuna haja ya kumuweka mtu Magufuli Hostel sijui siku 20, wakati unamuona kabisa hana tatizo - Kumuweka ‘isolation’ mtu ambaye ni mzima unapoteza resources zetu

Kila mwezi tunalipa Bilioni 700 kwa madeni ambayo karibu Bilioni 200 inaenda World Bank. Sasa kwasababu wao wameguswa na ugonjwa huu hasa World Bank watusamehe madeni hata kwa percentage ili hela zitumike kupambana na Corona

Tumesikia kwenye vyombo vya habari maeneo fulani, hata hizi mask zimetolewa kwenye nchi fulani wamezikuta na corona. Vyombo vya ulinzi na usalama waanze kushughulikia vitu vya msaada visije leta madhara. Ukiletewa mask lazima ujue imetoka wapi

Nawapongeza Watanzania walioanza kushona mask zao wenyewe. Shona mask zako zitumie. Usisubiri za kuletewa ambazo hata huwezi kujua aliyekuletea ana misingi gani

Rais Magufuli: Hii fumigation iliyokuwa inafanyika Dar ni upuuzi mtupu kwasababu kwa watalaamu wote wanajua #CoronaVirus hawezi kufa kwa Chlorine. Virus yule ni futa, linapasuka ama kwa kutumia sabuni au kwa kutumia alcohol au joto kubwa, maji moto au mvuke

Hakuna fumigation yoyote inayoweza kuua #Corona na hili Watanzania lazima tuambizane ukweli. Kama pangekuwa panafanyika fumigation na #CoronaVirus wanakufa, basi nchi zilizoendelea zisingeshindwa kutengeneza fumigation na kumwagia nchi yote

Kumekuwa na papara kutoka kwa watu wetu wenyewe. Wizara ya Afya nimeambiwa siku za nyuma walitoa amri ya kufanya fumigation. Mabasi yanatoka wapi yanafanyiwa fumigation yaende wapi yanafanyiwa fumigation. Nililiona hili sana Dar na Mwanza

Nimewaita ninyi vyombo vya Ulinzi na Usalama mfanye uchunguzi hata kwenye hizo fumigation, nani alitoa maagizo?. Lakini pia uchunguzi mfanye katika 'testing kits' na hizo barakoa zinazotoka nje. Jiridhisheni kama ni salama kwa Watanzania


Wakuu mie nimeshindwa kusoma Wala kusikiliza hotuba yote nimeishia tu hapo kwenye mask toka nje sijui sasa naomba kuuliza kwa wanaojua,Je kwenye kipindi hiki cha corona TBC na TFDA sijui wapo rikizo? Maana inaonekana kwa majibu wa Magufuli budhaa toka nje si salama,au hizo mask zinashushwa Tanzania toka hewani?
 
Rudini TBC wamerudi tena.

Amesema siyo kununua barakoa kila nchi kuna barakoa zingine zinakuja na corona.

Amesema kuna watu wanataka Dar iwe lockdown "never haifungwi ni senta ya kila kitu

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
Hajasema barakoa kasema barakola
 
Hii tabia ya kuwadharau wataalamu na kuleeta ujuaji itawachanganya raia sasa. Kuwa rais sio kujua kila kitu.
 
Taarifa iliyotumwa na mseamaji wa Ikulu kuhusu hotuba ya Rais Magufuli kasema"Anataka wizara ya Afya iwe inatoa takwimu sahihi maana ana taarifa waliopona ni zaidi ya 100 na walioambukizwa ni 284


My take,mpaka hapa nilipo binafsi nimeisha changanyikiwa,hii ni siku mbaya sijawahi ona

Hotuba ya waziri mkuu leo amesema waliopona ni 11

Waziri wa Afya wakati akionyesha wale 30 katika mikoa hajasema wamepona zaidi ya 100

Hapa Rais anakosoa wizara kutotoa takwimu sahihi (Which is which?)
IMG-20200422-WA0005.jpg
IMG-20200422-WA0006.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kama hataki watu kuwekwa karantini, watu wasivae mask zile zilizothibitishwa ubora wake badala yake washone vya mitambaa yoyote tu, watu wajifukizie dawa za miti shamba. Kwakweli hii ni hatari sana nawaomba watendaji wasiogope kutoa ushauri wa kitaalamu kwa hofu ya kufukuzwa bila hivyo tutateketea wote kwani hiyo ni sawasawa na mtu mnayesafiri naye kwenye boti moja lakini mwenzenu anapekechua mnamtizama tu lakini mkae mkijua maji yakiingia na boti ikizama mnazama wote
Nashindwa hata kuandika,yaani rais kututangazia kuwa bidhaa toka nje si salama wakati huo hizo bidhaa zikiwemo madukani nchini Tanzania maana yake anasema serikali yake imeshindwa kazi,hakuna udhibiti tena kila mmoja anaweza akaingiza bidhaa yake Tanzania as if anapekeka home kwake Kama nchi hii wangekuwa wanaishi watu hai sentence hii tu ingetosha kuanza maandamano ya kumng'oa maana anachezea maisha yetu
 
Back
Top Bottom