Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

kavulata,
alichosema Magufuli, literally, ni.... "Mtanzania, chagua ama ufe kwa njaa au ufe kwa Corona".

sasa hivi hapa Dar watu wanapukutika.
soma hapa chini...

Corona inapukutisha watu Dar. Kuna wanaolalamika ndugu zao kuzikwa kinguvu na Mamlaka Dar huko Bahari Beach, Buza na Mbweni - JamiiForums

Wagonjwa wa CORONA wajunja geti hospitali ya AMANA DAR ES SALAAM na KuTOROKA - JamiiForums

marais wenziwe wanaotumia akili za university degree zao halali si za kufoji badala ya mtulinga wamekataa kabisa watu wao kufa kwa Corona.

Nairobi na Mombasa ni economic hubs za Kenya. zimepigwa partial lockdown - bidhaa (si watu) zinaingia na kutoka bila ya shida yoyote.
 
Kamgomoli,
Hawa ni wale watu wenye utani hata mbele ya kifo na ndio wanaotoungoza kazi ipo watanzania. Wameshakimbilia majumbani mwao na hawajali itakuwa vipi kwa wengine. Kuweni makini na corona.
 
kibaravumba,
Mkuu hìi post mpya au ni inputs za post yangu? Asante ila mimi nilichomaanisha atakae niambia nivae barakoa na kuhamasisha unapokohoa kuweka kiwiko cha mkono tu basi.
 
Hii nihatari hata kwenye hili janga ambalo halichagui bado tuna hoja na michango yakiushabiki? nilifikiri hili gonjwa lingetufanya tuzungumze lugha moja lakini wapi, dah!!!
 
Mr worldwide,
Kujivukisha kama Mkuu alivyosema , kama sehem ya njia ya asili binafsi nilimuelewa alimanisha katika vita kila silaha inayoweza kutumika itumike.

Hata ivyo pamoja na mtahalam mmoja kupinga niliona kama anawekeza akili katika vitabu tu ila njia hii sisi tuliokulia vijijin wakati wa mafua makali sana nakumbuka yalichukuliwa majani machanga ya mkaritusi unachemsha then unafunikwa na blanket off and on na kweli ukipiga siku mbili mafua hamna binafsi nimejifukiza sana enzi izo nikiwa kwa bibi.
 
Richard, Mkuu Richard, long time no see bro lakini dah, sikubaliani na wewe bhana!!

Mosi, hata watu wanaopigia upatu lockdown, wote ukiwasikiliza wanasema wazi kwamba lockdown kwa watu lakini usafiri wa mizigo uendelee kama kawaida. That being said, hoja yako ya kukosa kodi, hapo haiingii!!

Magu kajificha Chato?! Mi sijui bhana lakini inakuaje mtu ambae alikuwa Chato kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka na kurudi Dar January 09, leo hii tena awe Chato kwa siku zote hizi?! Kwanini asiji-lockdown Ikulu ya Dar au Dodoma ili aendelee na shughuli zake kama kawaida?!

Yaani Chato kuwe na facility bora kwa ajili ya usalama na afya yake binafsi na familia yake, kuliko Ikulu ya Dar es salaam?

#MagufuliTokaChato bhana!

Marekani walileta vurugu siku nyingi?!!

C'mon Rich, hebu fuatilia zile vurugu na maandamano yamefanywa na nani! Kama utakumbuka, Trump amekuwa akibishana na baadhi ya Magavana huku yeye akitaka lockdowns ziondolewe huku magavana wakisema hapana!!

Trump alifikia hadi kusema yeye anayo mamlaka ya kuingilia maamuzi ya kimajimbo!!

In response to that, ndipo watu wakaandamana ingawaje sio wengi kama inavyovumishwai! Kuona hivyo, Trump akazidi kuwa-encourage. Pitia ukurasa wake wa Twitter siku ya April 17 uone tweets zake za "LIBERATE MINNESOTA", "LIBERATE MICHIGAN", LIBERATE VIRGINIA ambapo alikuwa anawa-pump!

Watu wakaamini kwamba Wamarekani wamechoka, polls ikaendeshwa! Kuja kufanya uchunguzi ikaonekana sio tu majority ya Americans wanahofia lockdown kuondolewa mapema lakini pia ikaja kugundulika walioandamana ni wafuasi wa Trump, ambao kimsingi walitaka kumuunga mkono!

Na kundi lingine linalopigia upatu kuondolewa lockdown ni House of Freedom Caucus! Kama unafuatilia US Politics basi bila shaka utakuwa unawafahamu Freedom Caucus, na kwahiyo haishangazi kuona wao ni miongoni mwa watu wanaopigania sana kuondolewa lockdown!!

Nani waliyarusha sana haya maandamano? FOX...

Kwamba Georgia wanataka ku-unlockdown; sawa! Kwani mliambiwa lockdown ni milele? Kama wanaona hali inaruhusu, haishangazi kusikia wanataka kupunguza makali ya lockdown to partial lockdown! Hata Wuhan lockdown iliondolewa baada ya kuona hali inaruhusu!

Khaaa! Nani huyo kasema Rais anatisha watu?!

JPM haitishi watu bhana sema anawajaza watu ujinga!!

Mkuu Rich hebu kuwa honest ndugu yangu!!! Yaani unasema:-
Halafu, wewe wasema kwamba anatisha watu ni vipi anatisha? Ikiwa watu wanapotosha ukweli wa habari na kutoziamini taarifa za wizara husika ya afya wewe wataka upotoshaji wa taarifa uendelee ama?
Hapo sijakuelewa ujue?! Yaani unamaanisha JPM ndie anaweka rekodi sawa dhidi ya wapotoshaji, au?!

JPM huyu huyu aliyesema coronavirus haiwezi kuingia kanisani na msikitini, au JPM mwingine?!

JPM huyu huyu aliyesema baadhi ya barakoa zina coronavirus, au JPM mwingine?

JPM huyu huyu aliyewahi kusema barakoa ni "mavitambaa ya puani" tu na hayasaidii kujikinga na coronavirus except imani kwa Mungu, au JPM mwingine!!

Unamaanisha huyu huyu ambae jana kaja na mpya kwamba mvuke na wenyewe ni tiba (au kinga?) ya coronavirus, au kuna JPM mwingine?!

Hebu ngoja... si ndo huyu huyu ambae mwaka 2015 alisikika akisema ni namna ilivyo rahisi kufanya uchenjuaji wa makinikia cuz' it's a matter of raising the temperature in the furnace, na metal with a lower melting point, itaanza ku-melt na kuiacah nyingine na hivyo kufanikisha ku-separate gold from copper concentrates!!!!

Ndo huyo anayeweka rekodi sawa dhidi ya upotoshaji, au kuna mwingine?!
 
Saint Ivuga, Too sad... yaani tunashindwa kukabiliana na janga socially, medically na hata kiuchumi! Matokeo yake, aftermath inaweza kuwa mbaya kweli kweli, hasa ukizingatia tayari sekta binafsi ilikuwa inahangaika ku-recover lakini ghafla, janga hili hapa!!
 
"Most important thing we can do for the health of our ECONOMY is to protect the health of our PEOPLE”

Quote hiyo hapo juu inatupa nafasi ya kujiuliza, jee maamuzi ya Rais kuwa KAMWE Dar haitafungiwa hata kwa muda tuu kwa sababu ndio kiini cha uchumi na mapato makubwa ya nchi yako sawa?

Ushauri wa kuifunga Dar kwa hizo wiki mbili au tatu ili watu wasitoke nje ya mkoa au kuingia ni kuzuia kuongezeka maambukizi na kutokomeza ugonjwa, sasa bila kufanya hivyo baada ya muda Dar itakuwa ni ugonjwa mtupu na jee penye Afya mbovu kuna uchumi wenye Afya?
Nani mshauri wa hili Rais wetu? Au anashauriwa na hataki kusikia?

Sheria/katiba inasemaje kama Rais anashauriwa jambo lenye ulinzi wa maisha ya raia na hataki kufuata na maisha yanapotea?

Wajuzi watueleze!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kila kitu cha mzungu ni kizuri ,hizo barakoa mnazoshangilia za msaada nchi nyingi tu wamezikataa hazina viwango, sisi tumekuwa dampo tukubari tu Kila takataka inayoletwa na ngozi nyeupe, tuacheni kuwahusudu hao watu ambao kwa namna moja ama nyingine wanahusika na huu ugonjwa,

Baba yetu wa juu hawezi ruhusu matatzo yatupate kama anajua hatuwezi kuyadhibiti, anajua sisi hatuna nguvu ila ni wajuaji sana, japo anajua Tanzania tunaishi na mashetani ambayo yanaombea matatizo yatupate ili nafsi zao zifurahi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona humalizii mmeambiwa pia muwe mnajifukisha na mvuke, na pia mkaambiwa coronavirus haiingii kanisani, na kwamba mkaambiwa mkajazane misikitini na makanisani kama kinga na tiba ya corona, mbona umesahau kusema kwamba mliambiwa msitegemee barakoa kwa sababu ni mavitambaa tu yale ya puani?!
Mko brain washed kiasi hiki?
Jiulize wewe... yaani Wanasiasa wanawafanya muondokewe na unafahamu namna hii?! Huku unapiga marufuku Sunday Schools na Madrasa kwa watoto, huku unawaaambia wazazi wao wandelee kujazana misikiitini na makanisani!!!
Nchi zetu hasa hizo unazozisifia hazina record ya kusema ukweli siku zote. Takwimu zao sio za kuaminika sana Kama unavyotaka kuwaaminisha watu.
Lini Tanzania ya Mgufuli imekuwa ya kusema ukweli?! Au ukumbushwe kwamba jana asubuhi PM kasema 10 wamepona, jana hiyo hiyo saa kadhaa baadae JPM anasema watu zaidi ya 100 wamepona!!

Hivi kwa akili yako unaweza kulinganisha seriousness iliyopo Rwanda na Uganda na hii ya Tanzania?!

Acheni kutetea ujinga nyinyi wakati tayari madhara ya kupigia kwenu makofi kila kitu yameshaanza kuonekana! Magufuli leo hii haogopi kufanya chochote kwa sababu anajua tu, hata leo hii akibadili kauli akasema "kuanzia sasa hakuna mtu kutoka nje nje", nyinyi mtageuka tena kama vinyonga!

In short haumtumii ufahamu wenu kusema mnachosema bali always mtasema na kushabikia kitakachosemwa au kufanywa na JPM hata kama ni cha hovyo!!
 
Hawa ni wale watu wenye utani hata mbele ya kifo na ndio wanaotoungoza kazi ipo watanzania. Wameshakimbilia majumbani mwao na hawajali itakuwa vipi kwa wengine. Kuweni makini na corona.
Ukiona kwenye familia Baba anaongea lake,mama nae lake,ujue hiyo familia ndani ni vurugu tupu. Km kuna vitu usalama wanavijua inakuaje waziri mkuu haambiwi mpaka anaenda kuongea na viongozi wa dini? Kuna watu mihemko imewajaa kuliko kufikiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
LIKE, Rais huwa akosei..? Think again man. Anakosea sana tu. Kama jana kaongea baadhi ya mambo ambayo ni trash.

Ummy na majaliwa ndio watu ambao wako field kwa sasa.. yeye yuko chato. Nani anajua namba haliso kama sio wale walioko field?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…