Sote tunashuhudia jinsi Rais wa Cotanza anavyozamisha jahadi kwa kutake advantage ya umasikini wa Cotanza walio wengi na ujinga wao dhidi ya virusi hatari zaidi Corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu kwa ugonjwa COVID_19).
Njia za kupunguza kusambaa kwa maambukizi zilithibitiswa na kutumiwa na mataifa karibia yote ulmiwenguni ni kuzuia mikusanyiko ya watu, matumizi ya masks zilizo sahihi, kunawa mikono mara kwa mara na kubwa zaidi ya yote kujitenga.
Haya yote ni majukumu na wajibu wa kila mmoja wetu pamoja na mamlaka ya nchi na yanawezekana bila shaka yoyote.
Wananchi ama RAIA mmoja mmoja ambao kwa hakika hakuna anayependa kupoteza maisha kwa janga hili wamefanya liwezekanalo katika kunawa mikono kwa kadri wawezavyo na kufuata miongozo itolewayo na mamlaka. Kwa babati mbaya ama makusudi jemedari mkuu ile ya Cotanza amekuwa akipotosha sielewi kwa lengo gani ila ni nia iliyo ovu inayopaswa kuingiliwa kati na mamlaka zingine nitaainisha upotoshaji wa wazi wa jemedari mkuu.
1. Tuendelee kwenda makanisani/misikitini ambako anafahamu wazi watu wataendelea kukusanyika na kusababisha usambaaji wa hali ya juu wa virusi hivi. Licha ya mashule kufungwa ila haikuwa na maana kwa sababu bado watoto walewale wanaruhusiwa kukusanyika makanisani na misikitini. Inasikitisha sana.
2. Mteule wake aliwatangazia watu wa Cotanza kuwa waliopona ni 5 mpk jana, ila yeye kutaka kuzidi kuonyesha hakuna tatizo kubwa LA virusi hivi akatutangazia hizo data za waziri wake siyo kweli waliopona ni zaidi ya 1000. Hii ni kutaka kuwaamninisha watu kwamba hata ukiugua utapona jambo litakalopunguza umakini wa watu walio wengi kuendelea kuchukua tahadhari madhubuti.
3. Bwana yule anadai watu watumie hata masks za vitambaa. Hii anajua kabisa hizi masks hazizuii hata kwa 1% maambukizi ya virus na linapaswa kukemewa mara moja. Anafanya hivi akijua kwamba RAIA wengi hawatamudu masks zenye ubora hivyo wataendelea kuambukizana na kufa kwa wingi, badala ya mamlaka kuhakikisha masks hizi zinapatikana kwa wingi na kwa bei ambazo wataweza kumudu. Hapa ni kukwepa kugaramia uhai wa RAIA wake.
4. Kali zaidi ya yote ni kwamba ukiugua jifukize na sijui majani gani.. Hivi kweli tunajali uhai wa RAIA na kwamba ni tiba tosha ya corona. Mpaka hapa alipaswa kushtakiwa kwa makusudio na kupanga kuuwa RAIA wake ambao anapaswa kuwalinda kwa mujibu wa sheria. Imethibitishwa na mamlaka IPI ya kitabibu kwamba kujipiga mvuke utapona corona na machapisho gani yakutuaminisha hili.
Wito wangu ni kwa watu wa dini, taasisi mbalimbali za kiraia na zile za haki za binadamu, wataalam wetu wa afya kuingilia na kutoa elimu kwa usahihi dhidi ya janga hili. Ikibidi muweze kuzuia uendeshaji wa ibada ama kutafuta njia itakazuia mikusanyiko katika mahala penu pa kazi ili kuokoa wamumini wenu.
Tuliko fika kila mmoja ajiokoe yeye na wale anaoweza kuwasaidia walau kwa kuwapa elimu, kuwazuia dhidi ya mikusanyiko na kama unaweza kuwanunulia masks sahihi endapo kuna ulazima wa kutoka.
Jemedari wa nchi ile ya Cotanza amekwama na yeye kaikimbia nyumba yake inayoungua.
Sent using
Jamii Forums mobile app