Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Mshikemshike ulianza wiki iliyopita. Taharuki kila kona, na mwishoni mwa wiki iliyopita RC wa Dar es salaam alipotangaza amri ya kuvaa barakoa kwa wananchi wake. Jumatatu wengi walivaa barakoa za mafundi cherehani kwa hofu aidha ya mkono wa dola au corona.
Jumanne jioni hofu ikaongezeka, Jumatano kauli za Rais zikaleta tumaini, sasa taratibu tunarudi kwenye maisha yetu ya zamani.
Je, kutokuwa na hofu dhidi ya corona ni silaha ya ushindi dhidi yake?
 
Ni Vizuri kutokuwa na Hofu juu ya Ugonjwa,hii inasaidia kujikinga kwa nguvu zote huku ukijiamini na kuendelea kutafuta kipato.
 
nakushauli usiwe na hofu itakusaidia. Disregard all precaution utapenya salama. nami nafanya hivyo!
 


Hofu imepungua sawa jikinge huyoo uliemtaji hanaga huruma ata mfe 100,000
 
Kwasasa watu wamesema hata wakihisi dalili za Covid,hawaendi hospitali maana hakuna dawa so watajifukiza majumbani na kuendelea na maisha!
 
Nenda mbweni ukajionee watu wanazikwa kwa kutupwa kwenye mashimo.
Keeeeenge mweupee wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na kwanini Kenya na South Africa pia yanaendelea? Vipi USA, Italia, Uingereza..... huko kote hawafuati?

Sent using Jamii Forums mobile app
Samahani braza hivi huko ulipopataja kote maambukizi yalikuwaje mwezi March na April yamepanda kwa kiwango gani(namaanisha % ngapi) in comparison to hapa Bongonyooo..?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…