Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Jana katika maelezo yake kuhusu ugonjwa wa Corona, Rais Magufuri amedai yawezekana masks zinazotoka n'nje zikletwa na virus wa Corona.Kwa kuwa mabeberu wanaleta vitu vingi tu Kutokana kwao.

Sasa kwa kuwachokoza mabeberu hawa haoni kuwa amejiweka kwenye mazingira magumu Sana,maana mwezi huu tu wa never mabeberu wanemfurahisha Mara mbili.

Moja Nchi 25 zilizopewa mkopo kuokoa uchumi usianguke Kutokana na Janga la Corona Tanzania imenyimwa.Pili nchi 27 zilizosamehewa Madeni Kutokana na Corona Tanzania haimo.Sasa mabeberu watamfurahisha Tena sijui kwa staili gani.
 
johnthebaptist,
Ulaya na marekani hawatoi takwimu za wsliopona ila walioambukizwa (ukiambukizwa haina maana unaumwa) na waliofariki (wanaofatiki approx 1% ya walioambukizwa) ndiyo maana tofauti kubwa Tanzania ni takwimu za wagonjwa. Ndiyo sababu unaona namba ya waliofariki kubwa. Takwimu ulizolinganisha haziwiani
 
IMG_20200414_175805.jpg
 
Mkuu hizo takwimu ni kwa mujibu wa vizara ya afya,kiongozi wa malaika mtarajiwa anasema waliopona ni zaidi ya 100 kutoka vyanzo vyake vingine nje ya wizara ya afya
yeye ndiye ana wanausamama, hawa wa wizara wanatisha watu takwimu hazizi kuwa sahihi
 
Hata kama anawachukia mabeberu hakutakiwa kuwaonyesha waziwazi kwenye hotuba zake.

Kiuhalisia Raisi wetu Hana lugha ya kidiplomasia, yeye anaenda mzimamzima tu.
 
Kwa kweli nimeisikiliza hotuba ya Rais imejaa busara na kujiamini sana hakika yeye sio mtu wa kuyumbishwa.

Aliponifurahisha zaidi ni kuomba WB ifute madeni ya nchi maskini ili ziwezi kujisitiri katika kipindi hiki kigumu kinachoambatana na mdororo wa uchumi.

Ningependa kutumia fursa hii kumuomba yeye awe mfano kwa kuomba taasisi zote za fedha hasa mabenki kufuta mikopo ya wananchi maskini wa Tanzania ambao biashara zimeshuka wafanyakazi wa sekta binafsi mishahara imekatwa au kutopokea kabisa nina uhakika Rais wetu ni msikivu akianza yeye hapa nyumbani hata WB na IMF watafurahishwa na hatua hiyo na ombi lake pia litapewa kipaumbele naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom